Habari za weekend?
Leo nimeona nizungumze kidogo! Unakuta mke au mume wako ana mchepuko wanaendelea na mapenzi kwa muda tu.
Kuna katabia watu kujipa moyo ooohhh ' mi ndo mume/mke wa ndoa nna cheti mie'!!!!
Waweza baki na cheti ndani kisicho na faida kama graduate wa miaka hii 'first class ila maisha magumu hana ajira' huku mwenzio anakula raha na kuwekeza kwa mwingine miaka na miaka.
Kama zipo changamoto zinazomfanya mwenzio achepuke rekebisha kama ziko ndani ya uwezo wako. Vinginevyo atakula ujana huko,raha zote kwa mchepuko, atajenga huko,
Akizeeka, akipata matatizo hasa ya kufirisika magonjwa sugu anarudi kwako na usipomhudumia dunia itakunyooshea vidole kwa roho mbaya[emoji2] [emoji2] [emoji2]
Wahanga wengi wa hili ni wanawake,kuna ndoa nyingi zimevunjika kabisa kisa mchepuko anapendwa sanana anachukua nafasi yako. Sio kila uliyenaye kwenye ndoa anakupenda wengine walikuoa kimakosa alikuwa hajapata anachokipenda.
My take 'Never under rate mchepuko of your wife/husband'