Usiuchukulie poa mchepuko wa mwenza wako

Usiuchukulie poa mchepuko wa mwenza wako

Huu ushauri nadhani unawafaa wanawake wenzio, sidhani kama kuna mwanaume atajua mke wake anachepuka na akawa na ushahidi kisha akaendelea kuishi na huyo mwanamke.
Kweli kabisa mkuu labda awe poyoyo
 
Habari za weekend?
Leo nimeona nizungumze kidogo! Unakuta mke au mume wako ana mchepuko wanaendelea na mapenzi kwa muda tu.
Kuna katabia watu kujipa moyo ooohhh ' mi ndo mume/mke wa ndoa nna cheti mie'!!!!
Waweza baki na cheti ndani kisicho na faida kama graduate wa miaka hii 'first class ila maisha magumu hana ajira' huku mwenzio anakula raha na kuwekeza kwa mwingine miaka na miaka.

Kama zipo changamoto zinazomfanya mwenzio achepuke rekebisha kama ziko ndani ya uwezo wako. Vinginevyo atakula ujana huko,raha zote kwa mchepuko, atajenga huko,
Akizeeka, akipata matatizo hasa ya kufirisika magonjwa sugu anarudi kwako na usipomhudumia dunia itakunyooshea vidole kwa roho mbaya[emoji2] [emoji2] [emoji2]
Wahanga wengi wa hili ni wanawake,kuna ndoa nyingi zimevunjika kabisa kisa mchepuko anapendwa sanana anachukua nafasi yako. Sio kila uliyenaye kwenye ndoa anakupenda wengine walikuoa kimakosa alikuwa hajapata anachokipenda.

My take 'Never under rate mchepuko of your wife/husband'


Wahanga wa haya matukio ni wote sema tu wanawake wamezidi, maana anaweza kuwa na mchepuko akajisahau kabisa kuwa ni mke wa mtu na huyo aliyenaye ni mchepuko tu. Hapa ndipo inapowacost wanawake zaidi.
 
Wahanga wa haya matukio ni wote sema tu wanawake wamezidi, maana anaweza kuwa na mchepuko akajisahau kabisa kuwa ni mke wa mtu na huyo aliyenaye ni mchepuko tu. Hapa ndipo inapowacost wanawake zaidi.
Cost kwa nani?
 
Cost kwa nani?


Cost kwa wanawake....nimesema inawa-cost wanapokuwa katika relationship na michepuko yao maana wanajisahau kuwa wameolewa tayari. Yaani unakuta mwanamke anajisahau kuwa kaolewa na kulowea ama kuzimikia kwa mchepuko mpaka dunia nzima inajuwa. Mwanamme gani yuko radhi kuwa na mke wa namna hii, ndiyo maana tukigundua tunawaacha.
 
mi mkewangu akija kuchepuka sijui nita mfanyaje nita hakikisha atanikumbuka milele
 
Nadhani ingefika wakati wanawake wote tuolewe tu hizi ligi za side chick na main chick zingeishaga,,ila raha ya ngoma ingia kati ucheze,,mleta mada kama ungekua umeolewa nadhani ungeelewa kuwa wanaume kuchepuka kwao ni damuni hata umfanyeje,,sio kila mwanaume anaechepuka kuna kitu amekosa
 
Back
Top Bottom