Usithubutu hata kidogo kumnyima mwenzi wako tunda

b191

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
742
Reaction score
1,032
Habari!...

Kuna wanaume au wanawake wengi wakigombana tu na wake au waume zao huwa wanatabia ya kunyimana tunda.

Unapomnyima mwenzi wako tunda unasababisha madhara yafuatayo;
1. Kutafuta mchepuko

2. Kuyumba kiuchumi ndani ya familia. Kwasababu mara nyingi atatumia kiasi cha pesa kwa ajili ya mchepuko badala ya familia.

3. Madhara ya kisaikolojia kama msongo wa mawazo.

4. Ugomvi usioisha ndani ya familia. Hasa mmoja wenu anapokutana na mafundi wazuri wa nje ya ndoa.

Tafadhali wanajamvi unapogombana na mwenzi wako USISUSE KULA TUNDA.

"TUNDA NI TIBA MUHIMU SANA"
 
Wenye ndoa ebu nijibuni tafadhali, hivi kama mke hayupo period, wala hana discomfort yoyote, akitaka kukunyima unyumba huwa wanatumia maneno gani???
 
ana

kwambia mara amechoka mara tumbo linamuuma au anajisikia uchovu umuhurumie apumzike
 
Haya maelezo hayatoshi mkuu...yaani sina mchepuko, nina genye alafu unasema umechoka??? labda anene kwa lugha.
 
Hili lina wahusu zaidi kina dada mara nyingi ndio hufanya kama komoa kwa wanaume zao japo hawajui jipu wanalo tengeneza lita wagharimu pakubwa
 
ana

kwambia mara amechoka mara tumbo linamuuma au anajisikia uchovu umuhurumie apumzike
[emoji1] [emoji1] [emoji1]

Huyo mbona mstaarabu, wengine wanakupa makavu live.
 
kweli mkuu kuna jirani yangu hapa mdada anakitembeza sana wamegombana na mume miezi mitano sasa hawajaduu
 
Haya maelezo hayatoshi mkuu...yaani sina mchepuko, nina genye alafu unasema umechoka??? labda anene kwa lugha.
Aisee.. hiyo kitu ukiwa na hamu nayo halafu ukanyimwa akili huwa inahama kabisa na concentration kwenye mambo mengine huwa ni zero.
 
kweli mkuu kuna jirani yangu hapa mdada anakitembeza sana wamegombana na mume miezi mitano sasa hawajaduu
[emoji1] [emoji1] [emoji1]

Halafu siku hizi vijana mtaani wakigundua tu hilo wanawekeza fasta
 
Habari!...

Kuna wanaume au wanawake wengi wakigombana tu na wake au waume zao huwa wanatabia ya kunyimana tunda.

Unapomnyima mwenzi wako tunda unasababisha madhara yafuatayo;
1. Kutafuta mchepuko

2. Kuyumba kiuchumi ndani ya familia. Kwasababu mara nyingi atatumia kiasi cha pesa kwa ajili ya mchepuko badala ya familia.

3. Madhara ya kisaikolojia kama msongo wa mawazo.

4. Ugomvi usioisha ndani ya familia. Hasa mmoja wenu anapokutana na mafundi wazuri wa nje ya ndoa.

Tafadhali wanajamvi unapogombana na mwenzi wako USISUSE KULA TUNDA.

"TUNDA NI TIBA MUHIMU SANA"
Ukiona Umenyimwa Tunda Ujue Ugomvi Bado Haujaisha, Inabidi Utafute Namna Nyingine Ya Kusolve Huo Mgogoro Kabla Ya Kuomba Tunda Tena.
 
Back
Top Bottom