Naomba nikupe shule kidogo kwenye hili la utabiri!
Unapofanya utabiri unatumia vifaa maalum vyenye uwezo wa ku-detect hali ya anga kwa muda na wakati uutakao.
Utabiri huu unapatikana kwa teknolojia za aina mbali mbali,ambazo gharama zake pia zinatofautiana!(kuna GCM na RCM)
Kutokana na umasikini wa nchi zetu,kushindwa kuhimili gharama za vifaa vingi na kuviweka maeneo mengi,(RCM) tunatumia zaidi GCM ambayo inakusanya taarifa kwa coverage kuuubwa sana,hivyo kupunguza "accuracy" ya utabiri!
Kwa mfano,kituo cha utabiri kilichopo Ilonga,Kilosa mkoani Morogoro,kikitegewa na wilaya 2 au 3,kitatoa taarifa ya jumla sana,kwa sababu hawatakuwa na uwezo wa ku-specify exactly ni eneo lipi mvua zitanyesha,matokeo yake taarifa inakuwa "......mvua baadhi ya maeneo,mawingu kiasi,ngurumo na vipindi vya jua….."
Lakini kama tungekuwa na uwezo na kuamua kununua vifaa na kuwa na vituo vingi vya ukusanyaji taarifa,basi tungeweza kupata taarifa sahihi kabisa za utabiri kwa maeneo husika pasipo kuwa na hata chembe ya mashaka!
Gharama za uendeshaji wa tecknolojia ya utabiri wa hali ya hewa ni kubwa sana,ndiyo maana nchi nyingi za kiafrika hazina "accuracy" kwenye ubashiri wa hali ya hewa!
Inagharimu kiasi cha dola za kimarekani si chini ya 5000 kwa kituo kimoja kwa siku,sasa kama tukitaka kupata utabiri sahihi itabidi tuwe kituo kwa kila kata,tuna kata ngapi Tanzania? Kwa gharama ya dola 5000 kwa kila kata kwa siku,tutatumia dola ngapi kwa ajili ya utabiri wa hali ya hewa?
Tuendelee kuvumilia tu,kwa sababu hali zetu ndiyo hizi hizi!¡
Sent using
Jamii Forums mobile app