Usiri wa wakaguzi & wapima mizigo na wamiliki wa mizigo hiyo katika viwanja vya ndege nchini tz... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usiri wa wakaguzi & wapima mizigo na wamiliki wa mizigo hiyo katika viwanja vya ndege nchini tz...

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by TUJITEGEMEE, Nov 13, 2011.

 1. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,776
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Katika siku za karibuni nilibahatika kutembelea baadhi ya viwanja vya ndege. niliweza kushuhudia jinsi utaratibu wa ukaguzi na upimaji wa mizigo unavyofanyika. Kuna jambo moja lilinishtua katika eneo hili ambalo nimehisi nanyi wa JF kuwashirikisha kulifahamu(kama ulikuwa hulifahamu). Jambo lenyewe ni usiri unao kuwepo kati ya baadhi ya wamiliki wa mizigo na wapimaji/wakaguzi wa mizigo hiyo katika viwanja hivyo vya ndege. Usiri huo unatokea baada ya wakaguzi/wapimaji wa mizigo kumaliza kazi ya kukagua/kupima mizigo hiyo. Utawaona wahusika wanaitana pembeni na kupeana "vikaratasi" kwa uficho.

  Wasiwasi wangu juu ya USIRI huo ni kuwa kuna uwezekano wa ulaghai wa uzito halisi na uhalali wa mzigo unaosafirishwa, jambo ambalo linaweza kusababisha:

  1.0 upungufu wa mapato kwa shirika la ndege husika na serikali (kama uzito utakaosafirishwa utakuwa mkubwa kuliko ulio unaoonyeshwa kwenye nyaraka)
  2.0 Kusababisha ajari kama ndege hiyo itabeba mzigo kupita kiasi( kama mwendesha ndege hatakuwa makini kugundua hilo)

  3.0 Kurahisisha shughuli za uharamia wa ama kuteka au kulipua ndege unaoweza kufanywa na watu wasio na "utu" na kusababisha maafa makubwa(endapo mizigo hiyo itakuwa ni ya kudhuru usalama wa abiria).

  USHAURI WANGU: Mamlaka zinazohusika(Usalama,TRA n.k) zifuatilie jambo hilo.

  Nawasilisha.
   
 2. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,776
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Mod delete one thread, due to duplication of threads
   
 3. 1

  19don JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  ninavyo jua mimi kuhusu taratibu za kusafilisha mizigo
  mwenye mzigo; ataandaa mzigo wake na kuuleta eneo la mzigo katika kiwanja cha ndege
  -
  wakala wa ndege; atapima mzigo ili kujua uzito na aina ya mzigo kwa ajili ya kuaandaa karatasi ya mzigo (awb)
  = ; atatengeneza draft ya malipo na kumpa mteja(mwenye Mzigo) ili aandae malipo ya huduma hiyo ya kusafilishiwa mzigo wake
  eg; MYC ,ADC,AWB CHA, SC ,TC na nyingine kutokana na shilika la ndege lililovyo weka taratibu zake
  ; baada ya mteja kukamilisha malipo husika wakala ataandaaa AWB na kuanza taratibu za customs
  tra ; afisa wa tra atakagua documenty zote kama ziko sawa
  eg; release order, cdf(tansad) awb invoice na attachement nyingine zinazo husika (vibali) kutokana na aina ya mzigo
  ; akisha hakiki docs ataenda kukagua mzigo physical eneo la ukaguzi kuna maofisa wengine wa selikali
  eg; kilimo, nyara za selikali , chakula ,afya etc hawa na wanakagua mzigo huo kama unahusika na kitengo cha na wagonga
  muhuli wao baada ya nao kuhakikik docs na ukaguzi waliofanya
  swissport ; watakagua uzito wa mzigo uliopo kwenye mzani na ule ulioandikwa kwenye awb kama upo sawa mteja atalipia terminal charges
  za swissport
  taa ; wanakitengo cha scanner watascan mizigo yote iliyopo kwenye awb kama ipo sawa na akilidhika kuwa ipo sawa atabandika stiker
  ya usalama (security check) na mzigo utaingizwa bond kwa kusubili taratibu nyingine za kusafilishwa

  sasa kwa utalatibu huu sielewe hicho kificho kiko sehemu gani tufafanulie zaidi
   
 4. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,776
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  SAMAHANI SANA KWA KUCHELEWA KUTOA UFAFANUZI.

  Mlolongo watu wanaopaswa(shwa) kuwepo eneo hili kama ulivyoeleza sikuuona. Kulikuwa na Wafanyakazi wawili wanakagua mizigo na kusaidia abiria kupitisha mizigo hiyo kwenye "scanner". Mfanyakazi wa tatu alikuwa kwenye control unit ya scanner. Mfanyakazi wa nne alikuwa kwenye sehemu ya kupima mzigo ambaye huyu baadaye alikuja kusaidiwa na mmoja ya wafanyakazi waliokuwa wanapitisha mizigo kwenye scanner. Mfanyakazi watano alikuwa anakagua tiketi(alivaa kitambulisho cha 'agent' wa shirika la ndege). Mfanyakazi wa sita alikuwa dreva wa gari liliobeba mizigo kutoka eneo la upimaji mizigo kuelekea kwenye ndege. dereva huyu alisaidiana na wale wafanyakazi waliohusika kupima mizigo kupeleka mizigo hiyo kwenye ndege. mfanyakazi wa saba alikuwa anakagua tiketi za abiria kabla ya kuingia kwenye ndege. Wafanyakazi sita walikuwa na vitambulisho vya Tanzania Aviation Authority. Huko kwenye ndege kulikuwa na wahudumu wa ndege na (ma)rubani wawili.

  Kificho kilikuwa kati ya wale wafanyakazi waliohusika kupitisha mizigo kwenye scanner na kupima pamoja na abiria aliyekuwa anahusika na mizigo hiyo.
   
 5. 1

  19don JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  nimekupata mkuu eneo unaloongelea ni terminal 2 ,hapo nimekupata
   
Loading...