Usipoacha tabia hizi hautakuwa huru kifedha

Doctor Ngariba

JF-Expert Member
Jan 28, 2020
480
765
Habari wakuu,

Uzi huu unatokana na maisha anayoishi shemeji na mdogo wangu lakini pia naamini wapo wengine wanaoishi maisha kama ya hawa madogo. Ikumbukwe nimeleta uzi huu siyo kwa lengo la kuwabeza, kuwabagaza, kuwatweza au kuwadhihaki kwa namna yoyote ile bali kwaajili ya kuwapa wengine tahadhari ili wasiwe kwenye kundi lenye kufanana na hawa Jrs.

1. Kupenda sana wanawake kuliko kipato chako
Vijana wengi siku hizi wanapenda wanawake kuliko uwezo wa kumudu mahitaji ya wanawake wanaotoka nao. Kashemeji kangu siku moja kalinambia, "Bwashemeji naomba unipe elfu 20,000 nimtumie Khadija", nilimjibu dogo tafuta hela kwanza ndipo uingie kwenye mapenzi. Hajawahi kuniomba tena pesa kwa jambo lenye mfano huo. Dogo ukitaka kuruka agana nyonga.

2. Uvivu na kupenda sana vya dada na kaka zao
Utasikia "Oya brother shemeji yupo home, nataka kuja kula chakula leo mchana". Hebu mujiongeze kidogo, wewe kijana ushafika 25+ bado unafikiria kuja kula kwangu eti kwa kuwa mimi ni kaka au shemeji yako?

Kuna mmoja ananambia "Ukihamia kwako, chumba kimoja nitaishi mimi!" Jinga sana huyu dogo. Unakaa 12 hours kazi kubadilisha channels kwenye TV tu. Amka pambana umiliki TV na kisabufa cha kwako.

3. Hawajifunzi kuweka akiba
Unabet unaliwa, unahonga hovyohovyo. Huweki akiba hata kidogo kwamba ukipata dharura ikusaidie.Tafuta pesa weka akiba kuza mtaji baadae uzitumie vizuri alaah.Wewe kila siku unapiga mzinga tu hata buku ya daladala unampigia simu dada yako.

"Sister naomba buku nije huko ya kurudi atanipa bwashem"Bwamdogo mimi shemeji yako siku hizi buku zangu nawapa wajomba zako wapate kununua ice cream wakiwa shuleni.Hujui kwamba utawanyima haki zao. NB: Sijadharau betting hapa msije nipopoa tafadhali.

4. Wengi hawana adabu na heshima
"Oya brother, hakuna koneksheni unipe mdogo wako nifanye?" Hebu mujifunze lugha mzuri basi walau "Kaka naomba unitafutie koneksheni mdogo wako", Unampa koneksheni bila kujali lugha yake halafu bado anaharibu kwa mabosi kwa lugha za vijiweni "Xaxa boxi nitumie buku 20,000 poti kaninasa hapa Vigwaza". Ukiuliza kosa hakuzingatia alama za barabarani. Nani kakwambia umuandikie lugha ya hovyo bosi wako? Nini maana ya xaxa?

5. Acheni kujipa makuu wakati hamna hadhi hiyo
"Bwashemeji kwa kazi hiyo mimi hapana niko tayari nikae ndani". Dogo hivi unajua mimi shemeji yako nilihitimu degree yangu na niliwahi kubeba viroba vya saruji vya kgs 50 pale bandarini kama kuri? Unadhani utapata mchekea kwenye maisha?

Nahisi povu litanitoka sana, hebu tuwasanue hawa madogo kwa kuziangalia tabia zao za hovyo ili wajifunze na waondoke kwenye Ujunior.

Nafasi ya update ipo.
 
Mwanamke hata Kama haumpi hela fahamu tu kuna uwezekano mkubwa akawa tatizo la wewe kutoboa maana mafanikio huwa yanahitaji utulivu mkubwa Wa akili na hisia sasa ukiwa na mwanamke anakucheat basi tayari umeshaua kiungo muhimu katika safari yako ya maisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom