Usiombee kutendwa

Usiombee kutendwa

Pole. Ilishanitokeaga had chakula hakipand. Ila JF ilinisaidia kusoma mikasa ya wengne..bada ya muda mchache tu maisha yakarud normal...ni ngumu ila inaishaga..
 
Haya maandiko yako yamenifunza sanaa,kila kitu fanya kwa kiasi,nikitendwa mm ambaye nishasoma mchezo maumivu n tofaut na ww uliye deep down.hawa viumbe c wa kwenda mzma mzmw,wakishajua unawapenda bac ndo huanza visa wakidhan utaomba msamaha tu.
Noma sana
 
Wanaume tumeumbwa na ujasiri sana, na siyo rahisi kuonyesha udhaifu wake ata pale anapoona ameumizwa sana na mahusiano

Wengi wao huwa tunazuga kama hali hiyo haituumizi kumbe moyoni mwetu kunafukuta maumivu ambayo yanauma na ata umeze Lori la panadol sio rahisi kupata nafuu,binafsi hali hiyo imenikuta na kuna wakati natamani ata nisitoke nje kuona kinacho endelea ila ndio hivyo lazima maisha yaendelee.

Natamani nibadili namba ya simu pengine nahisi naweza kupata utulivu na kumkwepa ila nahisi nitapoteza watu wengi sana ambao tunasaidiana kimaisha,nipo kwenye msongo mzito sana wa mawazo

Hapa JF ndio sehemu pekee naweza kueleza hizi hisia ambazo siwezi Ku share na mtu yeyote physical ila nina uhakika na hili litapita.
Fanya maisha yako kwani huyo sio mzazi wako useme huwezi muacha
 
Wengi wenu mnapata tabu kwa vile mlikuwa na expectations kuubwa,hii hutokea hasa kwa vijana kwa vile awali hukuwahi kujua saikolojia hasa ya mwanamke
Binafsi nilichojifunza kwa miaka hii nimeishi duniani ni kwamba usiwe na matarajio chanya tuu kwa kitu chochote kwenye maisha wewe jua tu kwamba Jambo lolite unalolifanya kwa malengo chanya Basi jua Kuna hasi yake pia.Hii itakusaidia kujiandaa kisaikolojia kuhimili pindi hasi ikitokea ili usipotee kwenye reli yaani uwe na huzuni inayohimilika na kuganga yajayo,ukizaa watoto kwa mfano jua pia wanaweza wakafariki au wakaugua au ukabahatika wakawa vizuri
Ukioa wewe jua inaweza tokea ukawa cheated nk so jiandae kisaikolojia kwa Jambo lolote hasi kwenye maisha ,kuishi kwenye nadharia ya perfection,rightness na positive response mda wote ni mbaya lazima utatoka kwenye reli,utakata tamaa na inaweza pata stroke kwa heart attack
 
Samahani mkuu hivi mnaosema mapenzi yanauma mlishawahi jigonga kwenye ncha ya kitanda na ugoko au kidole cha mwisho..? Anyway tuachane na hilo vipi ulishawahi kabwa roba ile inaitwa "usiempenda kaja..?"
Ila Basi ktk maisha kila mtu anajua maumivu yapi yamewahi kuwa makali kwake ila in serious way kabisa mkuu kaa ukijua afya njema ndio msingi wa starehe zote,so fanya juu chini afya iwe imepatikana imara utakuja nishukuru one day na utaelewa namaanisha Nini.
Ni kweli mkuu kitu kikubwa cha kukilinda kwa sala,maarifa na juhudi zingine za kibinadamu ni afya ya mwili na akili,hayo mengine yanahimilika hata upoteze kila kitu kuanzia watoto,mali au kazi utapambana lakini pia omba hayo yasikufike uzeeni hasa la kupoteza Mali kwenye umri ambao mwili hauna tena nguvu na maarifa ya kutafuta ,utalia Zaid ya maombolezo ya Daudi wa kwenye Bible.
 
Nimeona hakuna aliyekushauri uchukue dose, hayo maumivu unayopata ni Moto na dawa yake ni moto. Ruhusu macho yakupe mwenza mwingine (hata kama awe rafiki wa muda, tumia bima ya afya ya mwili), kila ukimkumbuka aliyekutosa, waza kupata dose, omba dose, siku so nyingi, upo huru. Akiba ni muhimu, usiitupe hiyo dose.
 
Mkuu acha kabisa, maumivu yake ni makubwa sana , hapa naandika lakini mimi still nimepitia changamoto hiyo siku si nyingi , kweli niliumia sana hasa ukitegemea nilimpenda sana huyo mtoto lakini yeye akaniona BOYA .

Wenye pesa waka mchukua nikafuatilia ishu nzima , nikaja kumuuliza kwa kumtega amekataa kabisa kwamba sio kweli tena macho makavu kabisa.

Nikimuangalia nabaki kulia mwenyewe maana nawaza huyu nimfanyeje ila sina chakufanya namshangaa mpaka saa hii. Anawezaje kunidanganya kiasi hicho?

Kama anaweza kutembea na mtu mwingine akakataa mblele yangu atakuwa kanidanganya mangapi?

Acha tu man
Kiufupi nitalia kwa mengine sio mapenzi, niliwah umia na kutetemeka mwili kwa mapenzi back in 2010s huko kuanzia hapo nilijifunza kupenda kwa kutumia akili na sio moyo tena Hadi Leo nimeoa mwendo ni huo huo.
Angalizo na tahadhari,kupenda kwa kutumia akili kutakufanya uone makosa zaidi kwa mwenzio na unaweza kuwa mkatili so jitahidi ku balance na hakikisha mwanamke unaempata ni yule anaeweza vumilia Hali hiyo,usijesema sijakutambua Ila hii njia haitakuja kukumiiza maana umeshajenga saikolojia ya lolote laweza kutokea na uko tayari.Faida ya njia hii ni kufocus kwenye mambo ya msingi ya familia kuliko kuwaza kuridhishana kwa kusimamia kucha kwenye mapenzi
 
Ukiona Giza limeongezeka usiku,ujue ni karibu na mapambazuko.Mungu ni wa rehema na hajawahi kukuacha Wala kukusahau kamwe,hivo jiandae kupata kilicho bora zaidi kuliko ulichokipoteza, pole sana ndg.
 
Mkuu acha kabisa, maumivu yake ni makubwa sana , hapa naandika lakini mimi still nimepitia changamoto hiyo siku si nyingi , kweli niliumia sana hasa ukitegemea nilimpenda sana huyo mtoto lakini yeye akaniona BOYA .

Wenye pesa waka mchukua nikafuatilia ishu nzima , nikaja kumuuliza kwa kumtega amekataa kabisa kwamba sio kweli tena macho makavu kabisa.

Nikimuangalia nabaki kulia mwenyewe maana nawaza huyu nimfanyeje ila sina chakufanya namshangaa mpaka saa hii. Anawezaje kunidanganya kiasi hicho?

Kama anaweza kutembea na mtu mwingine akakataa mblele yangu atakuwa kanidanganya mangapi?

Acha tu man
Mkuu kwani ulimsomesha?Kama ulimsomesha imekula kwako maana mchumba hatugharamii siku hizi...labda awe mke tu
 
Nilishasema wanawake wapendeni kwa kiwango usijinyime kula kisa unawekeza pesa zako kwa mwanamke ukizani ndio utamfurahisha, usijiumize kitandani ukidhani ndio njia ya kumtuliza, hawa viumbe hata uwape nini huwa kuna mda wanabadilika tu, anaweza kutana na mtu ndani ya wiki moja na akamtunuku tunda kimasihara

Penda kwa kiasi mtakuja kulia
Point
 
Mkuu kwani ulimsomesha?Kama ulimsomesha imekula kwako maana mchumba hatugharamii siku hizi...labda awe mke tu
Sijamsomesha hata, nilikuwa nae katika mahusiano ila nilijifunza kumuamini , nikamuamini sana kwamba atakuwa wangu!! Daah kilichotokea kumbe akiwa na mimi kuna jamaa walikuwa wanafaidi kijanja bila mimi kujua . Ila kutokana na kumwamini sikufahamu hilo , badae nikaamua kufanya mambo ya (BLACK MAGIC )
Kwenye kasimu kake loooooh nilichoka sana.

Watu wanalipa mpaka kodi ya nyumba , na mambo mengine ukicheki nilikuwa na malengo nae sana ila kwasasa nimebakia mtazamaji tu , japo ukweli naujua ila sijamwambia nimeamua kunyamaza , nayeye ananichora tu anajua sifahamu kitu
 
Pole Sana mkuu...ilishanitokea....ila muda ni mwamuzi mkubwa Sana nilishamsahau
 
Wanaume tumeumbwa na ujasiri sana, na siyo rahisi kuonyesha udhaifu wake ata pale anapoona ameumizwa sana na mahusiano

Wengi wao huwa tunazuga kama hali hiyo haituumizi kumbe moyoni mwetu kunafukuta maumivu ambayo yanauma na ata umeze Lori la panadol sio rahisi kupata nafuu,binafsi hali hiyo imenikuta na kuna wakati natamani ata nisitoke nje kuona kinacho endelea ila ndio hivyo lazima maisha yaendelee.

Natamani nibadili namba ya simu pengine nahisi naweza kupata utulivu na kumkwepa ila nahisi nitapoteza watu wengi sana ambao tunasaidiana kimaisha,nipo kwenye msongo mzito sana wa mawazo

Hapa JF ndio sehemu pekee naweza kueleza hizi hisia ambazo siwezi Ku share na mtu yeyote physical ila nina uhakika na hili litapita.
Nothing sucks forever in life, be strong bro.

Nalo litapita tu.
 
Acha kulialia wewe mtoto wa kiume bwana!
 
Back
Top Bottom