Usinunue iphone 13

Umaskini ni kitu kibaya sana..yaani mtu anaetumia Gadget ya $900 anaonekana tajiri na mpenda anasa

there you said it, Jaman haya ni maisha ya watu kuna wengine wanapenda gadgets kuna mtu ana electronics devices za kila ainaa...kutumia simu nzuri sio dhambi wala sio anasa come on..ni kifaa cha mawasiliano tunaishi mara moja, sasa wewe unaesema huwez kununua simu kubwa sabab hasara unatunza pesa, vipi hizo investment ulizozifanya kutokana na ela ya simu zinaendaje ume invest bitcoin au umenunua share JATU
 
Sijawahi fikiri wala kuwa na hamu ya kumiliki iphone Hata Kidogo Hizi simu hazinifai kabisi Too much Complicated Kitaa tunaziita gate kali

Simu yangu Pendwa Google pixel Goja nijichange nivute 3XL

Sema wewe hauna hela kama simu yako pendwa ni Google pixel kwanini usichukue Google pixel latest maana hiyo 3 ni ya zaman
 
4GB sijawahi kuzijaza

Japo natumia simu yenye 128GB

Simu yangu akikamata wife huwa atajipiga mipicha atajirekodi mi video, mi sina habari nayo
 
Mkuu 1TB unatunza nini kwenye simu?

Mimi kwenye simu hua sizidishi 50GB, hapa nina simu ina 256GB najiuliza nitazijaza lini hizi?

Mimi napenda simu kubwa hizi ila sio kwa sababu ya storage, ni kwa sababu ya functionalities zake.

Toka nimeanza kutumia simu nimefanya analysis naona simu za 64GB zinanitosha kabisa sema nyingi za hivyo hazina functionalities nazotaka kama good camera, higher refresh rate, high screen resolution na mambo kama hayo.
Huyo naona anataka weka movie ,, GTA na yale magame ya mission nk

Kwa kawaida hata 256Gb humalizi data hazili nafasi kubwa hivo labda anataka hifadhi movie
 
Kuna sababu imesababisha nikapenda simu za camera kubwa, huko nyuma nilikua natumia simu za camera ya kawaida, nikawa napiga piga picha za matukio. Sasa nilikua nimepiga picha na mama yangu, bahati mbaya mama akafariki, sasa zile good moments nilizokua na mama nilipojaribu kuziweka kwenye kumbukumbu kama picha kubwa za ukutani zikawa haziwezekani, zinaharibika, kwa ujumla sio nzuri. Hilo jambo limeniuma sana, nikaamua kuanza kununua simu kubwa tu zenye camera bora kabisa.

Hiyo ndio sababu kubwa nikaona haya maisha tunaishi mara moja, ukipata nafasi ya kuweka kumbukumbu na mtu unaempenda basi hiyo kumbukumbu iishi kwa muda mrefu angalau kwa wakati wa maisha yako.
Pole sana mkuu
 
Huyo naona anataka weka movie ,, GTA na yale magame ya mission nk

Kwa kawaida hata 256Gb humalizi data hazili nafasi kubwa hivo labda anataka hifadhi movie
dunia inakwenda kasi sana ndugu zangu.

miaka 5 tu iliyopita,ukiwa na memorycard ya 2gb unajiona mjanja sana,kwa sasa ili uwe na amani na flash yako,inatakiwa at least iwe 64gb.

256gb,ni nyingi kweli,ila jaribu kurekodi video moja ya tukio muhimu kwa 4k,uone itatoka video kubwa kiasi gani,video ya ya 5min inachukua mpaka 700mb.picha moja inasoma 8mb,unaweza usione umuhimu wake leo,ila miaka 5 mbele,ukaona ulijidhulumu.
 
Uko kama mimi.. nikienda kununua simu mtu akianza kusifia camera huwa namwangalia tu.. yan camera kwangu sio issue mana picha zenyewe sipigi. Mtu akiongelea charge atleast namuelewa

Camera natumia nikiwa wasap labda nakula napiga picha chakula natuma chapu tofaut na hapo ni ngumu sana ..au nikisuka amplifier zangu au chchte cha electronics ndo nachukua video
 
Unatumia simu kwa uogauoga ili isidondoke kisa itakapo kuja mpya ukabadilishe? Huo ni umasikini. Tumia simu inapokuja mpya huna haja ya kuibadilisha tafuta mtu umpe/muuzie igawe au iweke kama makumbusho kisha chana wallet ukanunue mpya udhihirishe umwamba wako unaousema hapo
😁😁😁😁😂😂😂😂😂😂😂
 
dunia inakwenda kasi sana ndugu zangu.

miaka 5 tu iliyopita,ukiwa na memorycard ya 2gb unajiona mjanja sana,kwa sasa ili uwe na amani na flash yako,inatakiwa at least iwe 64gb.

256gb,ni nyingi kweli,ila jaribu kurekodi video moja ya tukio muhimu kwa 4k,uone itatoka video kubwa kiasi gani,video ya ya 5min inachukua mpaka 700mb.picha moja inasoma 8mb,unaweza usione umuhimu wake leo,ila miaka 5 mbele,ukaona ulijidhulumu.
Mfano mm picha hata kwa mtu iwe ina 10mb me ninachoangalia kwenye hii simu yangu inaonekanaje nina picha za mb 2.5 ni nzuri za hii simu nikimtumia yoyote bado ni kali na camera ako na 8mp tu
 
Nitanunua kwasababu ya storage tu. Kazi zangu nahitaji storage kubwa na ndio iPhone ya kwanza kuwa na 1TB. Baada ya hapo sitanunua smartphone kwa miaka 10 ijayo labda niibiwe.
Mbona 1TB harddrive zipo tena Kwa Laki 1 mpk 2 tu yaani Uchome mil 4 kisa 1TB
 

ambae ana iman Give away hiyo ya YouTuber Mr whose the boss anatoa iphone 13 nahis 10 zile
 
Sielewi kwanini watumiaji wa iphone wanaonekana "wanajisikia" sana

Kama kigezo cha kuonekana malimbukeni sababu iphone ni GHALI......basi iphone sio simu ghali pekee, wapo akina Samsung Huwawei nk na wana bei ghali sana kwenye flag ship zao

Kwenye maisha kila mtu anavipaumbele vyake........hakuna raha kwenye maisha kama kufanya jambo unalolipenda na kuliamini wewe binafsi, ni raha zaidi kuliko kufanya mambo kwa mujibu wa "fomula"

Sio kila apendacho mwenzako lazima kilete maana kwako au ukitafsiri kwa mujibu wa ulivyo karirishwa maisha yanatakiwa kuwaje

Utakuta mtumiaji wa tekno labda anamtukana kweli mtumiaji wa iphone kwamba anachezea hela wakati amepnga kwa mtogole wakati yeye mwenye na tecno yake kapanga pia kwa mtogole, unabaki ujiuliza kwanini yeye asijenge masaki kwasababu anatumia tekno ya laki?

Jamani tutafuteni hela tushibishe matakwa ya nafsi zetu
Kama wewe unadhani kumiliki iphone ndio kukwamisha maendeleo yako hiyo ni wewe tu ujuaji wako, wenzako wanamiliki na wanapanda daladala kama wewe mwenye itel

Katika maisha yako hata siku moja usitumie umasikini wako kuharamisha matumizi ya vitu vizuri kwa wenzio
Kama wewe huwezi wenzio wana weza
 
Back
Top Bottom