Narudia tena, usiulize kwanini na unywaji bia wangu wote sijawahi kutoka na wanawake naokutana nao bar. kama mtu mzima huna budi kujiongeza pale ndugu yako anapopatwa na majanga. wahenga walisema mwenzako akinyolewa zako tia maji.
nimejifunza kuachana na uhuni kupitia ndugu yangu. Ndugu yangu wa damu kabisa alifariki kwa ugonjwa wa UKIMWI wakati bado kijana mwenye nguvu za kutumikia taifa. nilisikitika ila sikuwa na uwezo wa kumfufua, ila uwezo niliokuwa nao ni kujifunza kupitia maisha yake aliyoishi.
ukikutana na mwanamke bar mpige bia, mchekeshe mpaka mbavu zivunjike, bambia ubambiavyo, ila mwisho wa siku usije ukaamua kulala nae, huwa tunakutana tu sehemu za starehe angali hatujui afya ya yule tunaeongea nae ipoje. piga bia lipa bili kisha rudi kwa mamsapu ukaburudishwe na steki zake, hizi steki za mtaani ambazo hatujui kama zimethibitishwa na tbs zinaweza zikawa ni vibudu.
nimemaliza, karibu bia