Usiniulize kwanini sichepuki

Usiniulize kwanini sichepuki

nanya

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2016
Posts
672
Reaction score
523
Narudia tena, usiulize kwanini na unywaji bia wangu wote sijawahi kutoka na wanawake naokutana nao bar. Kama mtu mzima huna budi kujiongeza pale ndugu yako anapopatwa na majanga. wahenga walisema mwenzako akinyolewa zako tia maji.

Nimejifunza kuachana na uhuni kupitia ndugu yangu. Ndugu yangu wa damu kabisa alifariki kwa ugonjwa wa UKIMWI wakati bado kijana mwenye nguvu za kutumikia taifa. nilisikitika ila sikuwa na uwezo wa kumfufua, ila uwezo niliokuwa nao ni kujifunza kupitia maisha yake aliyoishi.

Ukikutana na mwanamke bar mpige bia, mchekeshe mpaka mbavu zivunjike, bambia ubambiavyo, ila mwisho wa siku usije ukaamua kulala nae, huwa tunakutana tu sehemu za starehe angali hatujui afya ya yule tunaeongea nae ipoje.

Piga bia lipa bili kisha rudi kwa mamsapu ukaburudishwe na steki zake, hizi steki za mtaani ambazo hatujui kama zimethibitishwa na TBS zinaweza zikawa ni vibudu.

Nimemaliza, karibu bia
 
Wewe jamaa upo kitengo nini? Kila siku bia. Nimepata kiu ya fasta.. ngoja tuone siku itaishaje.


My take; naona umeoa karibuni. Una hamu na mkeo.... ipo siku utakuja kuleta ushuhuda wa kuchepuka.
huyu mamsapu nna miaka nae minne, hakuna uhuni ambao sijawahi kuufanya ila tangu blaza alivyopotea kwa ugonjwa wa kukondesha, nimeamua kuwa mpole na kutafuna steki za mamsapu exclusively.. karibu bia mkuu
 
labda kwa ufupi ni kwamba sina historia ya kuchunwa, nilikua nawatafuna watoto wa kishua tu tena nyumbani kwao.. usione watu wameamua kutulia mkuu, wana historia chafu. karibu bia
nadhani hujaelewa neno loweka lilivyotumika hapa,yani unapiga kavu kavu
 
Narudia tena, usiulize kwanini na unywaji bia wangu wote sijawahi kutoka na wanawake naokutana nao bar. kama mtu mzima huna budi kujiongeza pale ndugu yako anapopatwa na majanga. wahenga walisema mwenzako akinyolewa zako tia maji.

nimejifunza kuachana na uhuni kupitia ndugu yangu. Ndugu yangu wa damu kabisa alifariki kwa ugonjwa wa UKIMWI wakati bado kijana mwenye nguvu za kutumikia taifa. nilisikitika ila sikuwa na uwezo wa kumfufua, ila uwezo niliokuwa nao ni kujifunza kupitia maisha yake aliyoishi.

ukikutana na mwanamke bar mpige bia, mchekeshe mpaka mbavu zivunjike, bambia ubambiavyo, ila mwisho wa siku usije ukaamua kulala nae, huwa tunakutana tu sehemu za starehe angali hatujui afya ya yule tunaeongea nae ipoje. piga bia lipa bili kisha rudi kwa mamsapu ukaburudishwe na steki zake, hizi steki za mtaani ambazo hatujui kama zimethibitishwa na tbs zinaweza zikawa ni vibudu.

nimemaliza, karibu bia
Ina maana kwa muono wako kila mhudumu wa baa ana VVU?
Au kila demu unayekutana naye maeneo ya kinywaji anaweza kukuambukiza VVU?
 
Unavyosema ni ukwel ila control ya pombe duh
 
Usirogwee...one mistake one goal. Iheshimu njia kuu
 
Back
Top Bottom