prince songoroka
Member
- Nov 11, 2019
- 59
- 73
Habar za leo wana JF,
Mwenzenu nimepata changamoto ambayo asilimia kubwa ya sisi vijana tunaipitia haswa kwenye ishu ya mahusiano.
Kuna mdada tulipendana nae mwaka 2020, tunapendana kama mbwa na mkia wake, na kipindi hiko alikuwa amehitimu kidato cha nne. Tuliweka malengo na akawa sehemu kubwa sana ya kila hatua nayoipiga kuyakimbilia mafanikio.
Matokeo yalipotoka alienda mbali na mimi na kwa kuwa mimi nilimpenda nikahamisha biashara na makazi yangu mahali karibu.
Tuliweka malengo ya kuoana ifikapo 2023 lakini kadri siku zilivyozidi kusogea kwenye ratiba alibadilika na kila anapoambiwa kuhusu suala la kuoa anakuwa mkali, mwisho wa siku kaishia kunidanganya ya kuwa wazazi wake wamekataaa.
Namshukuru Mungu na kumshukuru huyu binti kwa sababu nimejifunza maisha ambayo sikutegemea kama ningejifunza mahali pengine popote zaidi ya kupitia haya nilioyapitia.
Hawa madada tuwapende ila tusisahau.
Songoroka.