Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 692
Kutojali hiyo siyo kwamba ndio uwe mkatili kwa mwanamke. Kutojali hiyo siyo kwamba ndio usimtimizie mahitaji ya muhimu. Kutojali hiyo siyo kwamba ndio umfanye mwanamke hana thamani kwako.
Hapana. Sio hivyo. Ila unakua haujali kuhusu mihemko yake tofauti tofauti kila muda.
Hautojali sana kuhusu anachokisema, anachokifanya, au anachohisi, wakati unajua kabisa hamaanishi anachokisema, anachokifanya au anavyohisi.
Hautojali anasemaje pale anapojaribu kukubadili mawazo
Kuna mwanamke nilikua naye, tulipotoka mara ya kwanza, akawa ananisifia na anaonesha kunikubali. Lakini tulipofika nyumbani akabadili sura kabisa na kuniambia yani we sikupendi kabisa na sina hisia na wewe.
Nikamwangalia nikamjibu wote tunajua hilo siyo kweli. Akajaribu kunifanya nibadili mawazo lakini sikuonesha kujali kuhusu asemacho, na tukapata muda mzuri.
Hautojali mabadiliko ya kila saa ya mwanamke
Siyo nawe upande na kushuka kihisia kama mwanamke. Kama vile mwamba baharini, haijalishi mawimbi yatafanyaje, mwamba uko pale pale. Nawe uwe hivyo, mwamba usioyumbishwa na mawimbi ya hisia za mwanamke.
Hautojali anafanyaje pale anapojaribu kuonesha havutiwi nawe, japo unajua kabisa anakupenda
Wanawake hutumia mbinu ya kupotezea pale ambapo mambo yanaenda vizuri na kirahisi. Unajikuta umebaki na butwaa. Unabaki kujiuliza, huyu si jana tu tulikua tunaongea vizuri leo hii ameninua, lakini wewe baki na msimamo wako kuwa huyumbishwi na vitendo vyake vya hapa na pale.
Mfano rahisi ni mwanamke asiyekujibu sms, japo mlikua vizuri. Hilo lisikuyumbishe, usianze kumlazimisha akujibu sms. Akiwa tayari atakujibu kwa furaha tu. Akiuchuna we upo akirudi pia wewe upo vile vile.
Hata wanawake na wenyewe wanapenda mtu ambaye hawatoweza kuwaendesha sababu ya maneno, vitendo au hisia zake.
Wanataka mwanaume imara ambaye watamuegemea, wanataka mwanaume imara ambaye hatobadilika kama wao, wanataka mwanaume imara ambaye hatojali mawimbi yao ili wamjali.