Usimkopeshe hela mtu

Rafiki yangu nilimkopesha pesa mwaka jana, siku zimeenda kafilisika kibiashara na sioni dalili ya. Kupata hiyo pesa yangu, roho yaniuma sana
Huyu msamehe tunaongelea wasio na woga wa madeni, kama kafirisika muonee huruma.
 
Kunz dada mmoja alikuwa na shida mzigo wake wa kuuza umefika hana hela ya mzigo. Kaniomba nimkopeshe 150k atanipa baada ya week 2. Nikamuomba rafiki yangu anipe hiyo hela nimtumie. Mpaka leo hajanirudishia mpaka kani bloch simu zangu. Imebidi nilipe deni mimi. Ila nimemuambia unajizibia baraka hapa duniani, shida haziishi na hujui nani atakufaa kwa wakati gani.
 
Na wewe usikope kwa mtu..
 
tunaokopesha kibiashara huwa tuna.mikakati ya kuokoa hela zetu zisifie kwa manyang'au...

mimi mpaka sasa nina laki 8 iko nje kwa watu lakini inaniletea riba karibu 100,000 kila wiki.

wachache sana wameshindwa kuleta pesa na ndio nimewakamatia vitu vyao kama Tv, majiko ya gesi n.k.

kukopesha ni fursa ya kukupa hela usiifanye kisamaria.

Twanga watu riba sio unatoa hela kif.ala!

achukue laki alete 120,000 baada ya wiki 2.

Hii Tv mpaa leo iko kwangu na sina presha. Elfu 50,000 sijaiona hadi leo na mwenyewe kakusha tu. Kila Juma3 anatakiwa alete 10,000 kama riba, wiki ya 3 kakausha.
sundar 17" led Tv

huyu hapa alichukua mkopo wa Tsh 20,000 akaweka bondi jiko la gesi.

Akaahidi kuleta na riba ya Tsh 2,000 jioni yake.

nilimuwahi nikachukua elfu 10 akabakiza elfu 10.

Hii ni wiki ya 5 sijaona hata mia yake na jiko liko kwangu na wala sina presha.



Mikopo kwangu ni biashara Tosha.

nazibeba shida za watu nazigeuza faida.
 
Bora mpe Msaada sio Mkopo kama kakuomba Mil na unazo mpe elf 30 mwambie nakuchangia ...sina kitu kabisa...Utaokoa laki 970 na urafiki wenu pia utaendelea.
Hii technique ni nzuri sana, mtu akikuomba 50k unampa 5k na kumwambia sina kitu kwa sasa, hiyo nimekupa tu wala usirudishe
 
Siku sio nyingi nitamfunga kaka yangu kwa sababu ya kushindwa kulipa 2m. sasa hivi hapokei simu. Nimemtumia sms nitamnyoosha na undugu ufe tu. Usikopeshe ndugu mdau
Baada ya vitisho alilipa. Bahati nzuri akawa mstaarabu tukaombana msamaha. Tumeendelea kujaliana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…