Usimkopeshe hela mtu

Nyinyi mnaoendelea kukopesha ndo mna lea tatizo
 
Pesa, Fedha, Cash, Dollars, Pound, EUR, Dinnar, Shekeri, Ngawira Ni Shida Usimpe Mtu
 
Nakazia mkuu.Mwaka 2020 nimejifunza somo kubwa sana baada ya kuwakopesha watu wa karibu pesa tena kwa kujinyima.Nimeambulia kejeli.Usikopeshe kamwe akafie mbali na shida yake
 
Siku hizi nakopesha wanawake tu maana huwa hawana longo longo
Yap wanawake hawanaga mbwembwe , akikuzungusha Sana unajipimia kama mke , full stop ...Ila Wana daaah ....
 
Mimi hata iwe 20k Namuambia mtu kalete kitu chenye value ýa 20K iwe Vyombo au Radio weka apo afu sema unalipa lini hata awe ndugu nafanya ivo siku alizosema zikipita nampa wiki moja ya ziada ikisha hio bado hajalipa nauza kwa hasara kitu chake
 
Kopesha kwa maandishi

Usikopeshe Rafiki kizembe...urafiki utakufa na Pesa hakurudishii

Pesa ni kitu kingine man
Maandishi yapi mkuu mimi nadai laki moja na tuliandikishiana polisi huu ni mwezi wa 7 hamna kilichopatikana.
 
Bora mpe Msaada sio Mkopo kama kakuomba Mil na unazo mpe elf 30 mwambie nakuchangia ...sina kitu kabisa...Utaokoa laki 970 na urafiki wenu pia utaendelea.
 
Kopesha kwa maandishi

Usikopeshe Rafiki kizembe...urafiki utakufa na Pesa hakurudishii

Pesa ni kitu kingine man
Hata kwa maandishi haisaidii labda akifa ndg wamlipie kama ushahidi lakini ukienda kushitaki kosa linakurudia wewe unakopa bila leseni
 
Endelea kuomba MUNGU uwe ni mwenye hali nzuri kiuchumi

la hasha kuna siku utaomba pesa mtoto mdogo akukopeshe maana mnadhani wanaokujaga kukopa wanapenda

Mkuu hivi umeshawai kukopesha mtu pesa unayoitegemea ila akakuahidi anarudisha baada ya wiki moja

Ukaona isiwe tabu ukamkopa alafu ikapita miezi hata miwili yupo kimya amekausha hata taarifa ua kuomba radhi ameshindwa kulipa ndani ya muda hakupi?

Hii kitu ikikupata utajua kwanini hii biashara ya kukopesha hailipi.
 
Wewe kama unajijua ni rafiki yangu kindakindaki nikikukopa ujue sikulipi, marafiki hatukopeshani marafiki tunasaidiana.

Labda hizi ten ten Mkuu, pesa serious aisee nitakuja attach mali zako zipigwe mnada ukijiona. Mbwai mbwai tu!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…