Usimdhamini 'foreigner' police... Nilinusurika kuingia lupango!

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,796
Wamarekani wana kitu wanaita classified information... Yaani habari fulani kwa kundi fulani la watu... Na muda ukipita haiwi classified tena bali hutolewa kwa umma.. Lakini ni baada ya kujiridhisha haina madhara tena....

Kiswahili tunasema mavi ya kale hayanuki... Kisa hiki ni cha muda mrefu sana... Sitataja wahusika kwa majina na baadhi kwa vyeo

Nilikuwa nafanya kazi na raia 6 wa kigeni, ofisi kuu ikiwa Dar na ndogo ikiwa Lugoba... Tiktak za maisha na kutaka kutoboa kwa haraka hawa ndugu wakafanya makaratee yao na mamlaka ya mapato.. Dili ikavia na mzigo ukakamatwa.... Klichofuata ilikuwa ni kuwatafuta wahusika...
Bila kujua kinachoendelea Dar siku moja tukiwa tunarudi Dar kupitia Chalinze tukadakwa Kibaha... Lakini kwenye maelezo ikaonekana waliodakwa ni waajiriwa tu... Mabosi walikuwa dar 3 na walishakimbia kusikojulikana... Hawa 3 niliokuwa nao walikuwa waajiriwa tu kama mimi, hivyo nikaombwa niwadhamini... Kwa Makubaliano kuwa jumatatu yake (siku iyo ilikuwa ijumaa) niwarudishe Kibaha Polisi

Baada ya kukamilisha mchakato wa dhamana ilikuwa saa tatu usiku... Tulikamatwa saa tano asubuhi... Wale wageni hawakutaka tena kwenda Dar hivyo wakalala kibaha mimi nikarudi Dar nikijua hii ni ishu ndogo hivyo jumatatu yake nikafanya mambo mengine nikisahau kabisa ishu ya polisi na wale wageni jumamosi yake walirudi Lugoba
Jumanne asubuhi ndio nikaondoka Dar kurudi Lugoba nikiwa na gari ya ofisi.... Saa tano asubuhi hivi nikiwa napita kibaha nikapata simu ya polisi kuniuliza niko wapi..... Nikadanganya kuwa niko mbezi akanikumbusha kuwa jana yake nilipaswa kuwapeleka police na sikufanya hivyo.... Hivyo nimeanza kutafutwa
Wakati nazidi kuumiza kichwa msiri wangu akaniambia nasubiriwa kibaha nikamatwe.... Duu wakati niko kwa Mathias.... Nakaribia miembe saba nikapigiwa tena simu kuwa police wametoka Chalinze wanaenda Lugoba kuwakamata wale wageni tuunganishwe kwenye kesi moja.. Pona yangu ni mimi kuwawahi polisi na kuwakabidhi polisi wale wageni...

Nitafanyaje sasa!!! Siwezi kupaa niko Kwa mfipa wakati huo na polisi wa Chalinze tayari wako njiani kwenda Lugoba na muda si mrefu itajulikana nimeshapita Kibaha hivyo zitawekwa barriers mpaka Chalinze... Kwa vyovyote inabidi nisikamatwe na wale wageni wasikamatwe... Mpaka niwapate mimi kwanza

Gari yetu ya ofisi ilikuwa maarufu sana kwa askari wote wa patrol na trafiki kuanzia Lugoba mpaka Dar... Namba zake, rangi zake na shepu yake iliifanya itambulike kirahisi.... Mahesabu yangu ilikuwa ni kufika Mlandizi bila kukamatwa lakini pia kuhakikisha wageni hawakamatwi
Nafika checkpoint msiri wangu akanitonya kuwa gari imeonekana ikipita Kibaha muda si mrefu hivyo taarifa zishafika kwenye barriers zote.. Nisipite nizuiliwe popote nitakapopatikana..... Ilibidi akili ichemke haraka sana.... Kutoka checkpoint pale TRA kuna barrier 4 mpaka kufika Mlandizi na barrier kubwa iko madafu... Kwahiyo ili nisikamatwe inabidi kutembea off road lakini kwa tahadhari... Hatua iliyofuata ni kuwapigia wageni simu wafunge geti kwa na waruke ukuta watoke kwa nyuma... Nikawalekeza pa kusubiria wakati nawatumia gari toka Chalinze
Nilifanikiwa kufika Mlandizi bila kunaswa kwa kupitia njia za vichochoroni.... Nilifanikiwa kuwatoa wageni Lugoba mpaka Chalinze nikawabadilishia gari.... Jumla zilitumika tax 4 mpaka kuwafikisha mlandizi... Hapo nikawa na amani sasa

.... Mwisho wa sehemu ya kwanza.....
 
Sehemu ya pili
Kule Lugoba polisi walikuwa tayari wamewasili kwenye nyumba husika na kuweka guard wakisubiri amri ya kuingia kwa nguvu kama mpaka usiku itakuwa hakuna aliyefungua geti... Huku njiani kumbe walikuwa wameshajua kuwa nilipita kibaha ila sijakatiza Mlandizi niko wapi? Muda wote huo nilikuwa nawasha simu na kuzima mpaka nilipohakikisha nimewatia mkononi watu wangu... Msiri wangu akanitext kuwa niage kabisa familia... Madereva tax wa Chalinze walifyatuka ila kwakuwa wa pili aliishia kuwapeleka mpaka mizani sheli hakujua walipoelekea... Nikazima simu zote zao na zangu
Tukatafuta gesti ya vichochoroni nje ya mji ttukalala kwa kukesha mpaka asubuhi.... Wao wakiniomba msaada niwafikishe dar salama, mimi nikipanga nikawakabidhi central police mwenyewe
Alfajiri tukanyanyua, kuelekea Kisarawe then Dar.. Morogoro road isingepitika wala Bagamoyo road kote huko tulikuwa tunasubiriwa kama mpira wa kona
Nyuma ya Sterling, nina mnyama V8 four wheel drive, shockup za umeme saa mbili asubuhi tulikuwa Kisarawe kupitia barabara ya Vumbi iliyotubidi tuende mpaka maneromango
Safari ya dar ilikuwa ngumu hasa kutoka gongolamboto mpaka External... Ilikuwa kesho yake ni IDD hivyo mji ulikuwa na foleni ya kufa mtu.... Baada ya tabu nyingi saa sita ndio tunafika external
Nilikuwa nimezima simu tangu jana ile jjioni kuwasha tu ni ujumbe wa msiri wangu kuwa nifanye niwezavyo niwafikishe watuhumiwa central mimi mwenyewe na si sehemu nyingine yoyote
It was the race against time

Mwisho wa sehemu ya pili
 
Sehemu ya tatu
Tukiwa external sio mbali na ofisi nikiwa sasa najua wazi natafutwa nikapata simu iliyonifanya nusu nizirai... Nikapigiwa simu na mtu mkubwa akinitaka by saa tisa niwe nimewakabidhi watuhumiwa wangu kituo chochote cha polisi la sivyo nitaunganishwa kwenye kesi... Ni wakati nimeenda kujisaidia narudi sioni mtu wala gari funguo niliacha mezani... Nikauliza uelekeo na kuonyeshwa wameelekea njia ya buguruni.... Niliwakuta mwananchi wamegonga daladala iliyoingia barabarani bila hadhari.... Nikawakabidhi palepale kituoni
Haikuwa kesi rahisi lakini hatimaye sikuingia lock up... Kumbe wale wajinga wakati nadrive walikuwa kwenye mawasiliano ya siri na jamaa zao waliokuwa Ilala
 
Mshana una madini adimu kama mgodi wa Buzwagi. Ila chonde chonde tusije kohoa kwa utamu wa story kisha tukabaki kuishia mikononi mwa mwera.
 
Back
Top Bottom