Usilipize kisasi!!!!!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usilipize kisasi!!!!!!!!!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jpinduzi, Nov 24, 2011.

 1. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #1
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  Kuna hasara zinazoweza kukupata ukiamua kulipa kisasi kwa mambo uliyofanyiwa ambayo hayakupendezi. Ikiwa ni masuala ya kikabila, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya kidini, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya kifamilia, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya kikazi, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya uhusiano wako na majirani zako, usilipe kisasi.Ndiyo! Usilipe kisasi! Kwa nini? Kwa sababu"imeandikwa kisasi ni juu yangu Mimi; Mimi nitalipa, anena Bwana".
  Lakini ikiwa utaona ya kuwa Mungu hawezi kukusaidia na ukaamua kujichukulia madaraka ya kujilipiza kisasi hasara zifuatazo hakika zitakupata!

  Hasara ya Kwanza:
  UTASHINDWA!
  Katika jambo lolote lile lililokukasirisha - liwe la kidini, au kikabila, au kifamilia, au kikazi, na kadhalika ukiamua kulipa kisasi utashindwa wewe kwa sababu vita hivyo si vya mwili na wala silaha ambazo Mungu amekupa si za mwili! Tunasema hivi kwa sababu katika 2 Wakorintho 10:3- 5 imeandikwa hivi:"Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi yamwili; maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome, tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo".

  Tena katika kitabu cha Waefeso 6:12 imeandikwa hivi: "Kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho".
  Uwanja wa mapambano uliyonayo ni "katika ulimwengu wa roho" na mapambano uliyo nayo "si juu ya damu na nyama" - ingawa unaona ya kuwa ni watu na ni binadamu kama wewe wanaokusonga - lakini fahamu hili ya kuwa wanatumiwa tu na ibilisi!
  Mbinu mojawapo ya shetani anayotumia akitaka kukuangamiza ni kukufanyia kitu kitakachokukasirisha ili uamue kujibu au kushindana kimwili kwa sababu anajua ukishindana "kimwili" au katika mwili utashindwa hakika, maana vita hivyo si vya mwili wala silaha ambazo Mungu amekupa si za mwili!

  Hasara ya Pili:
  MATATIZO HAYATAKWISHA!
  Kumbuka imeandikwa hivi katika kitabu cha Wagalatia 6:7; "Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa chochote ampandacho mtu. Ndicho atakachovuna".
  Ikiwa umeamua kulipa kisasi kwa kumfanyia ubaya yule aliyekufanyia - ubaya hautakwisha, kwa sababu utavuna ulichopanda.Ndiyo maana imeandikwa hivi:"Yeye arudishaye mabaya badala ya mema, mabaya
  hayataondoka nyumbani mwake" (Mithali 17:13)
  Ukiamua kulipiza kisasi kwa kumfanyia ubaya yule wa nyumbani mwako - Biblia inasema "mabaya hayataondoka nyumbani mwako" Hii ndiyo maana matatizo mengi katika ndoa na katika jamii hayaishi - kwa sababu mtu akifanyiwa ubaya naye analipa kisasi.
  Ukiamua kulipa kisasi kwa kumfanyia ubaya yule wa nchini mwako ujue hakika mabaya hayataondoka nchini mwako. Hili ndilo lililowapata wenzetu wa nchi za Burundi na Rwanda - kulipizana kisasi - matokeo ni uhasama usiotaka kupotea - pamoja na juhudi zote za kimataifa kutafuta suluhisho.
  Ukiamua kulipa kisasi kwa kumfanyia ubaya yule wa kazini kwako - fahamu mabaya hayataondoka kazini kwako. Ikiwa ni shuleni - mabaya hayataondoka hapo shuleni.
  Tena hali ya mwisho inakuwa mbaya zaidi,kila wakati kisasi kinapoendelea kupandwa. Kwa sababu ukiwapa watu ubaya - nawe utapewa ubaya kwa; "kipimo cha kujaa na kushidiliwa, na kusukwa - sukwa - hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile upimacho ndicho mtakachopimiwa (Luka 6:38)
  Kumbuka ubaya haushindwi na ubaya mwingine, bali unashindwa na wema - kama vile dawa ya chuki si chuki bali upendo! Ndiyo maana Warumi 12:21 inasema; "Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema".

  Hasara ya Tatu:
  UNAMZUIA MUNGU KUKUPIGANIA
  Unaweza ukashangaa, lakini ndivyo ilivyo! Ukiamua kulipa kisasi juu ya tatizo ulilonalo - unamzuia Mungu asikusaidie kulitatua.Mungu hawezi kukusaidia kwa sababu imeandikwa "msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana, imeandikwa, kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana".
  Neno "ipisheni" limeandikwa kwa sababu kulipa kisasi "kunazuia" ghadhabu ya Mungu isipigane upande wako! Tena si hivyo tu lakini ukilipa kisasi unaingilia kazi ambayo si yako! Ni kazi ya Mungu maana anasema "Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana" Ikiwa kisasi ni juu ya Mungu kulipa, basi huhitaji wewe kulipa. Je, tunakwenda pamoja katika hili?
  Hatua yako ya kulipa kisasi inazuia mkono wa Mungu kukupigania - kwa hiyo ipishe ghadhabu ya Mungu kwa kutokujilipizia kisasi!

  Hasara na Nne:
  UNAJICHUMIA DHAMBI!
  Unapoamua kulipa kisasi, unajichumia dhambi! Hii ni kwa sababu kulipa kisasi huja kwa njia ya chuki iliyojengeka ndani yako kwa ajili ya mambo mabaya uliyofanyiwa. Huwezi kulipa kisasi bila ya kumchukia huyo unayejilipizia kisasi kwake. Na Biblia inasema hivi:
  "Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajuaya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake" (1 Yohana 3:15).
  Umeona hilo! Chuki huzaa kisasi, na huzaa dhambi ya kuua! Na
  Isaya 59:2b inasema; "dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia".
  Kwa hiyo kama umekwisha lipa kisasi au umekusudia moyoni mwako kulipa kisasi ni muhimuutubu ili Mungu akusamehe na mawasiliano yako na Yeye yawe mazuri.source -mwakasege.
   
 2. NTINGINYA

  NTINGINYA JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Jameni punguzeni kidogo mnatupa uvivu wakusoma
   
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kama mtu amekutendea kitu kibaya.
  Mimi huwa nafikilia kuwa huyo mtu hajui atendalo so
  Unamrudi kwa kumtendea lile lile ili iwe fundisho kwake kwani atagundua kuwa
  Oh kumbe halifai
  Mungu atakubariki sana kwa kuweza kumsaidia huyo jamaa asidhidi kukwaza watu na kuchuma dhambi.

  Usimtendee jirani yako kile wewe usingependa kutendewa.
  Amen!
   
 4. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 180
  Ukiwa mtu wa visasi kama Kikwete huwezi kufanikiwa. Si unaona nchi inavyoyumba hii.
  Ni ujinga kusign muswada wa katiba wakati wananchi hawana baraka nayo.
  :focus:
   
 5. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  umenena kweli.............niliwahi kutumbukia kwenye huo mtego wa kulipa kisasi; nikfanikiwa kuleta madhara zaidi ya nililotendewa lakini haikumaliza kabisa hasira niliyokuwa nayo!

  Ni upuuzi kufikiria kulipa kisasi! Ni kujiumiza na kujichumia dhambi kweli!
   
 6. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Yap_na hiyo ni sheria ya manabii(Musa)...jino kwa jino,.....ahahahaahaaaaaaaa and it works in the real world.
   
 7. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #7
  Nov 24, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  NTINGINYA...Kwasababu tu baadhi yenu hampendi kusoma haina maana ndo watu waandike makala zisizojitosheleza na kupoteza maana ya kile wanachoandika. Because then ujumbe wake hautafika vile anakavyotaka na hata nyie (msiopenda kusoma)mkisoma hamtapata alichokusudia hivyo ni kazi bure.....So stop complaining...Kama wewe unaesoma tu unalalamika je yeye alietumia muda wake kutafakari na kuandika hicho unachoona ni kazi sana kusoma???
   
 8. Mkono Mwekundu

  Mkono Mwekundu New Member

  #8
  Nov 24, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ooooo Yeah ....
   
 9. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #9
  Nov 24, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  mmh!! usiusemee moyo,sema unanipa uvivu na sio unatupa uvivu!!
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  Nov 24, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Na kuhusu kulipa kisasi mtoa mada... I prefer looking at it as teaching someone a lesson.Kuna watu ambao wanahitaji kuonyeshwa ubaya wa kile walichofanya ili wajifunze...wasiendelee kutendea wengine hivyo.Ila hii ni kama unajali atakayofanya huko mbeleni...otherwise unampotezea na kuendelea na maisha yako.Wakati mwingi hii ya pili inauma zaidi maana kama mtu alijaribu kukuangusha mahali ukampotezea na kuongeza kasi ya mafanikio yako ataishia kuumwa roho kichinichini.
   
 11. NTINGINYA

  NTINGINYA JF-Expert Member

  #11
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  NTINGINYA.Nikweli maneno yako samani kwate niliowakwaza. hatahivyo nimeirejea kusoma nimefaidika
  Kwasababu tu baadhi yenu hampendi kusoma haina maana ndo watu waandike makala zisizojitosheleza na kupoteza maana ya kile wanachoandika. Because then ujumbe wake hautafika vile anakavyotaka na hata nyie (msiopenda kusoma)mkisoma hamtapata alichokusudia hivyo ni kazi bure.....So stop complaining...Kama wewe unaesoma tu unalalamika je yeye alietumia muda wake kutafakari na kuandika hicho unachoona ni kazi sana kusoma???[/QUOTE]
   
 12. N

  Nsuri JF-Expert Member

  #12
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 996
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 60
  Nimesoma heading tuu!!!
   
 13. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #13
  Nov 24, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  [​IMG] Kwahiyo..........???
   
 14. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #14
  Nov 24, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  huuuuuuh na hvi metoka kwa office mechoka hbu nlale ntadeal nayo nkiamka
   
Loading...