Usililolijua Tabia za Watu Mkoa wa Arusha Soma Hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usililolijua Tabia za Watu Mkoa wa Arusha Soma Hapa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ndallo, Dec 7, 2011.

 1. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Wakuu huu naweza kusema ni mtazamo wangu kwakua nimetembea mikoa tofauti hapa Tanzania. katika mkoa huu wa Arusha nimekaa kwa muda mrefu na kuishi na watu wa jiji hili haswa niseme nimebobea katikati ya jiji! Sasa basi hebu fuatilia mtiririko huu hapa chini na wewe utoe experince yako:
  1. Ni mkoa ghali kulingana na maisha tuliyonayo hivi sasa.
  2. Asilimia kubwa ya vijana hawana kazi. (Utakuta vijana wengi wakowako tu).
  3. Kila mtu anajifanya ni dalali (chunga sana unaweza ukauziwa kiwanja hata cha kanisa).
  4. Wanaume ni wambea sana kuliko wanawake.
  5. Mtu akishakua na hela basi hatakosa wapambe wa kumpamba mpaka saa unakwenda kulala.
  6. Mtu akishakua na hela basi majina kama FOGO/KIFARU/MELI ndio majina utakayopewa.
  7. Mtu ukishakua na hela ya kunywa bia zaidi ya tano kaunta basi wewe ni FOGO/KIFARU/MELI. hata kama unakopa.
  8. Kutokana na ukosefu wa ajira vijana wengi wameingiwa na tabia ya kuamka asubuhi na mapema baa au Grosery na kuzimua maarufu kama KUTOA LOCK!
  9. Sio rahisi ukaamka asubuhi mapema katika ya jiji ukakuta maduka yako wazi sana sana ni kuanzia saa 3 asubuhi nakuendelea.
  10. Watu wa hapa hawana haraka sana yaani kwenda na muda, sana sana ukijifanya unaharaka utaambiwa si ungekuja jana au utaambiwa una kiherehere.
  11. Ukisikia mtu alikua Mirerani akaja na kijiwe chake akauza hata 100'000 moja halafu akaiingia baa na akasokota raundi mbili basi wewe sema lile jiwe uliuza shilingi 1000'000'000 wapambe watakupamba sana na hata wanawake hawatakaa mbali na wewe pamoja na madalali wa viwanja na magari.
  Jamani kama kuna nililosahau naomba muongeze kwakua naamini hapa JF kuna wakazi wengi wa Arusha. Nawasilisha.
   
 2. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,506
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Demu ukikutana nae baa hata hapo hapo anakwambia mdogo wangu anaumwa na sina hela
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,177
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama utafiti wako umeufanya kwa makini
  Issue ya mtu kuuza mawe na kujifanya ana pesa na kuzungusha round ilikuwa miaka hiyo ya 1990 kwa sasa hakuna limbukeni wa mambo hayo
  Vijana wa arusha ni wapambanaji na wanatafuta maisha na wala sio watu wa kuringia kuzungusha round bar wala kuringia bia
  Vijana wengi labda ulikutana nao ni wauza madini ambao kazi zao zinahitaji kukaa sehem ambako ni mitaa yao ya biashara na sio kwamba hawana kazi za kufanya
  Siwatetei ila ukweli vijana wa arusha ni wahangaikaji mno na wanapambana sana kuyaweka maisha yao kwenye mstari
  Ughali wa maisha wa mji wowote unategemea na upatikanaji wa pesa na sidhani kama utafiti huo umeulinganisha na miji mingine ya wapi
  Na hapa jua kwamba kuna watu wa UN wako wengi sana hapa mjini na kulingana na hali kama hiyo ni lazima mzunguko wa pesa ni mkubwa na kuwepo kwao ambapo watu kama wale wanapokea mishahara na marupurupu makubwa ni lazima yafanye mji kuwa ghali

  Ni mawazo yangu hayo mkuu maana na mimi ni mkaazi wa arusha sana na ni muda mrefu sana
   
 4. m

  mr analysis Member

  #4
  Dec 7, 2011
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  wanapenda kuvaa jeans, hawana adabu na pesa ,na ukibeba bahasha unaonekana msomi.
   
 5. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,457
  Likes Received: 3,707
  Trophy Points: 280
  asante Mr.rocky
  hiyo Na 4 labda unaokuwa nao wewe
   
 6. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,177
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Asante sana Black Woman
  Anachoongea sijui ni cha kusikia kijiweni
  Maana wanaume wa Arusha wanapambana na maisha yao licha ya mji kuwa ghali bado wanamudu kuishi na familia zao
  Wanamudu hata kupata za kunywa na kuzimua asubuhi
  Maana kama wangekuwa wanakaa vijiweni tuu ni muda upi wangepata hata hizo za kuzimua asubuhi
  Na sidhani kama kuna wanaume wa aina ya no 4 uliyoandika hapo may be sample zako zilikuwa kwa marafiki zako wawili watatu ulio nao
  Na kama mtu ana pesa zake mwache aitwe majina anayotaka na hata akiitwa meli kama ana pesa zake kuna shida gani
  Na ya nini kufuatilia life za watu na kufanya uchunguzi kuwa wanakunywa asubuhi na mapema au wanapongezana bar au kuna mtu ameuza jiwe lake la mererani na anazungusha round bar
  huo muda uliupata wapi
   
 7. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #7
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,177
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Mambo mengine hata sio ya kusema
  Kwani kuvaa jeans nako kuna mkoa
  maana mtu anavaa kulingana na nature ya kazi yake
  Kama anauza duka la spare au la vifaa vya umeme ulitegemea avae suti
  Au anafanya kazi godown ulitegemea aulambe mkanda nje
  Duh sasa hii ni ushabiki wa ajabu
   
 8. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #8
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,457
  Likes Received: 3,707
  Trophy Points: 280
  alikuwa anatafuta kupata idadi ya wambeya

  nipo huu mkoa miaka mia nane
  hayo mambo ya mererani ilikuwa zamani enzi za titus
  leo wakipata jiwe wala huwezi jua ki vile kimya kimya
  kwa mambo yao kama ni pombe ni za kawaida
  kama wanywaji wengine
  kuhusu ugumu wa maisha mie naona kawaida
  ishi kuendana na kipato chako
   
 9. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Mr. Rocky labda unaishi bwawa la Ma****i kule maeneo ya relini njoo huku maeneo ya Clock Tower uone wanaume wenye ndevu lakini hata ukishindia maji na pilipili wanajua!
   
 10. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Mr.Rocky wanazimua na viroba vya shilingi 500! Tembea uone wewe!
   
 11. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,177
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  haijalishi ninanokaa wala nini ila utafiti wako kaurudie tena
  Hao unaokutana nao ni wale wale wa kila siku ambao hawana deal la maisha
  Niko huu mkoa mwaka wa Kumi na moja huu haya mambo sijawahi yaona
  Enzi za kuringia na kuzungusha round bar eti umepata jiwe la mererani likuwa miaka ya 90 huko sio sasa
  Watu wameelimika na wanajua maisha ni nini
   
 12. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #12
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,177
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Kama huna kazi hiyo mia tano ya kuzimua kila siku unaipata wapi
  Na kodi ya nyumba unayokaa nani anakulipia
  na maisha yako unaendeshaji kama hujiwezi
   
 13. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #13
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,177
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280

  Black Woman nakubaliana na wewe
  Hizi ni story ambazo watu wanasimuliana huko vijiweni na hazina mshiko wowote
   
 14. m

  massai JF-Expert Member

  #14
  Dec 7, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Unaweza kutujuza umekaa wapi tena zidi ya Arachuga??mimi nipo mwanza maisha ni rahisi ukilinganisha na Arachuga,watu kiuchumi huku wapo hohehahe kwaukweli hata ukimkuta mwenye afadhali pia anafanana tu na ambae hana kwani kujiweka smart inaonekana ni mzozo,ukiwaza maisha Arachuga basi hakuna utakaposhindwa kuishi kwani hata mnaisha ya dar hayalingani na Arusha ,nimeishi mikoa ambayo ukienda kula hotelini unaonekana kama mgeni sehemu hizo,kimavazi ukichomekea unaonekana kama unaenda kanisani jumapili au hospitali au unasafiri.arusha chumba chakupanga ni alfu hamsini bei ya chini,na hakuna chai ya mia tatu ni mia tano kwenda juu,tofauti na huku zoo mpaka sasahivi buku jero kifungua kinywa umemalizi kilakitu supu mpaka chai.jipange kuishi Arusha ndugu.
   
 15. s

  shreak Member

  #15
  Dec 7, 2011
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Mkuu kumbuka UN asilimia kubwa wameondoka mbona bado maisha ni ghali? Kinachofanya mji kuwa ghali ni madalali, huu mji ni wa kitalii si kama Dar, Dar ni mji wa kibiashara sasa mji wa Arusha unapokea wageni wengi kutoka sehemu mbalmbali wageni wanakutana na madalali ili kurahisisha mambo yao...mfano kuna wenye nyumba ukitaka nyumba kwake lazima upelekwe na dalali ndo hapo unakuta mzawa una compite na mgeni halafu ndo unambiwa mambo ya kulipa kwa dola, sasa mzawa utapata wapi dola labda uwe unafanya tourcompany sasa ukipiga hesabu kila kitu kimedhaminishwa kwa dola na si shilingi hata nguo madukani utasikia hii nilinunua dola ....kwa tsh ni... siunaona rate mwenyewe.

  Kwa kifupi Utaliii ,United nations, EAC, Madini na Madalali ndo vimefanya mji umekuwa juu kama dola.
   
 16. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #16
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,033
  Likes Received: 378
  Trophy Points: 180
  Ama kweli Adui wa Mwanamke ni Mwanamke. Yaani hapa wataka kurusha ngumi kuwa wanawake ndiyo zaidi kwa hii tabia mbaya?
   
 17. Sordo

  Sordo JF-Expert Member

  #17
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huyu jamaa analysis yake ni narrow maana watu wa arusha ni watafutaji sana na ukitaka kujua hilo amuka saa kumi na moja asubuhi uone wamama wanavyocharika yaani watu hawasalimiani hiyo asubuhi utazani china! kwa ujumla watu wa arusha ni watafutaji na mchana wanatafuta jioni/weekend ndio wanazitumia!
   
 18. L

  LAT JF-Expert Member

  #18
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  duh .... hii thread ngumi zitarushwa, ngoja tumsubiri PJ atoe verdict
   
 19. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #19
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,177
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  nakubaliana na wewe mkuu na ndo maana nilimpa mfano mmoja tuu wa UN maana bado kuna EAC bado huu ni mji wa kitalii ambao kila kukicha kuna wageni kibao wanaingia na kutoka bado kuna mashirika kibao ya kimataifa yapo hapa
  Sasa madai yake kuwa mji huu wanaume ni wambeya au wanaamkia bar kupata za kuzimua sidhani kama ni kweli
   
 20. s

  shreak Member

  #20
  Dec 7, 2011
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Mkuu nenda stendi ndogo vijana wangapi wanapiga debe ili tu wapate mia wakusanye siku nzima atakuwa na shilingi ngapi bado hajala ndom mana wanatoa lock kwa mia tano mana kwa hali ilivyo ngumu mtu anaona bora atoe wenge apate nguvu na ujasiri wa kupambana bila hivyo siku haiendi.
  Huwezi linganisha maisha ya Arusha na Mbeya au kwingineko, vyakula bei juu, nyumba ndo usiseme Viwanja hatuongei.
   
Loading...