Usililolijua Tabia za Watu Mkoa wa Arusha Soma Hapa

Wakuu huu naweza kusema ni mtazamo wangu kwakua nimetembea mikoa tofauti hapa Tanzania. katika mkoa huu wa Arusha nimekaa kwa muda mrefu na kuishi na watu wa jiji hili haswa niseme nimebobea katikati ya jiji! Sasa basi hebu fuatilia mtiririko huu hapa chini na wewe utoe experince yako:
  1. Ni mkoa ghali kulingana na maisha tuliyonayo hivi sasa.
  2. Asilimia kubwa ya vijana hawana kazi. (Utakuta vijana wengi wakowako tu).
  3. Kila mtu anajifanya ni dalali (chunga sana unaweza ukauziwa kiwanja hata cha kanisa).
  4. Wanaume ni wambea sana kuliko wanawake.
  5. Mtu akishakua na hela basi hatakosa wapambe wa kumpamba mpaka saa unakwenda kulala.
  6. Mtu akishakua na hela basi majina kama FOGO/KIFARU/MELI ndio majina utakayopewa.
  7. Mtu ukishakua na hela ya kunywa bia zaidi ya tano kaunta basi wewe ni FOGO/KIFARU/MELI. hata kama unakopa.
  8. Kutokana na ukosefu wa ajira vijana wengi wameingiwa na tabia ya kuamka asubuhi na mapema baa au Grosery na kuzimua maarufu kama KUTOA LOCK!
  9. Sio rahisi ukaamka asubuhi mapema katika ya jiji ukakuta maduka yako wazi sana sana ni kuanzia saa 3 asubuhi nakuendelea.
  10. Watu wa hapa hawana haraka sana yaani kwenda na muda, sana sana ukijifanya unaharaka utaambiwa si ungekuja jana au utaambiwa una kiherehere.
  11. Ukisikia mtu alikua Mirerani akaja na kijiwe chake akauza hata 100'000 moja halafu akaiingia baa na akasokota raundi mbili basi wewe sema lile jiwe uliuza shilingi 1000'000'000 wapambe watakupamba sana na hata wanawake hawatakaa mbali na wewe pamoja na madalali wa viwanja na magari.
Jamani kama kuna nililosahau naomba muongeze kwakua naamini hapa JF kuna wakazi wengi wa Arusha. Nawasilisha.

Mkuu, hayo mambo mbona hayapo Arusha?. Ebu jaribu kurudia tena utafiti wako. Nafikiri baada ya Dsm, mikoa iliyo busy kwa wakazi wake kujitafutia vipato ni pamoja na Mwanza, Arusha, na Mbeya.
Ukisema kuwa wakazi wa Arusha ni wavivu, wambea n.k., hii si kweli mkuu!
 
Labda Ndallo anatembelea sehemu zile kama Unga ltd....Lakini kwakweli Arusha watu wanapambana sio utani. Mji kuwa ghali sio tatizo, ni kwamba hela ipo yakutosha..Soko Kuu, pako busy sana jioni na weekends wakina mama wanafanya biashara na watu shopping kama kawa...Arusha bana we acha 2..wewe sema huna hela, watu wanazo zakutosha..
 
Black Woman nakubaliana na wewe
Hizi ni story ambazo watu wanasimuliana huko vijiweni na hazina mshiko wowote
Watu wanapiga kazi usipime ! Ghorofa zinapanda mjini kati kama Kariakoo tena wajengaji ni wazawa!
 
Mtanibishia sana mkitaka kuhakikisha kuwa wazuraraji hawapo basi subiri maandamano ya Chadema yatokee muone wenye kazi ni wangapi!
 
Kuna mtu hapa ameona ile number 4 kaishupalia sana sijui inamgusa?
 
Inawezekana kuwa ni kweli Arusha maisha yako juu mpaka inasemekana na baadhi ya watu kwamba ukiweza kuishi Arusha basi hautashindwa kuishi mji wowote Tanzania.
Baadhi ya mambo aliyoyasema Ndallo hapo juu ni ukweli mtupu ila kuna mengine yamepitwa na wakati baada ya watu kujifunza kutokana na makosa yaliyokwisha tokea.

Hilo la watu kupenda pombe na wapambe linategemea na uelewa wa mtu na kiwango cha elimu hasa elimu ya maisha na ndiyo sababu inashangaza sana kwa Arusha utakuta mtu ana kajumba ka kawaida kabisha hakazidi ml. 50 na gari ya kutembelea isiyozidi 30ml. Na bastola ya halali au ya haramu basi hasalimiani hata na jirani yake. Tofauti na miji mingine kama Dar. Mwanza nk. Utakuta mtu ana hela ya ajabu kwenye account zake na biashara endelevu kibao na magari ya zaidi ya 200ml. Lakini bado ana heshima na marafiki na majirani pia na anajichanganya na wengine bila kujali ana kipato gani.

Kwa maana hiyo inategemea na uelewa na aina ya mtu husika amekulia na kupata shekeli yake kwenye mazingira ya aina gani.
Kingine ambacho ni kigumu na kina kera sana ni tabia ya watu wengi wa Arusha kupenda vipato vya aibu ambavyo mtu yuko tayari kufanya lolote ili tu apate pesa aweze kuishi maisha ya kuabudiwa fulani vile na hapa ndipo utakutana na madalali feki washirikina wezi matapeli na zaidi sana wengi ukiwakopesha kulipa ni mpaka aitiwe ndugu zake viongozi wa dini na mwisho kabisa atishiwe kubambikiziwa kesi ya silaha au alipe pesa ambazo utaweka na za ziada za kuwapa polisi kutoka kwenye bili yake.

Kwa kifupi wengi ya watu wa Arusha kulingana na aina ya mji huu huwa wana roho mbaya na wanafiki pia na hata kama watahamia miji mingine kama Dar hasa wengi hupenda kuishi maeneo Mbezi kimara tegeta kwa uchache na kwenineko huwa bado utawakuta wana vitabia vya aina hiyo ki mtindo fulani zaidi ya yote mtu hutegemea amelelewaje na ana roho ya aia gani.
Blaki womani usinipige mawe ni aina ya uzoefu kidogo nilionao kwa muda niliowahi kukaa kanda hii ya kaskazini kama huamini nenda polisi kaangalie majalada ya kesi zilizoko mahakamani utakuta ni za kujipatia mali kwa udanganyifu wizi wa kutumia silaha kesi za ardhi kutishiana mashambulio ya aibu nk.
 
Mtanibishia sana mkitaka kuhakikisha kuwa wazuraraji hawapo basi subiri maandamano ya Chadema yatokee muone wenye kazi ni wangapi!

kama ni kuchemka umechmka labda hii reseach ulifanyia kwenye familia yenu ndiyo ukachukulia ndiyo tabia za watu wa arusha....
 
Mkuu Derimto,
Yani chali angu umepiga penyewe, A town wanasaka noti kwa nguvu sana wanaenda mpaka chini,
Baba kuna matajiri wanajulikana kwa urushi pesa za madawa ndo usiseme.

Umenikumbusha nilivyopoteza gari hivihivi kumbe ile ilikuwa system watu kibaooo wamepoteza mali zao mtu ana magari utafikiri yadi yote mtu kachukua pesa kashindwa kurudisha...hu mchezo siku nyingi upo na mambo ya kuzungukana kama unakumbuka wamasai wangapi wameuliwa sababu walikuwa na mawe au wakiwa wametokeamererani
 
Mtanibishia sana mkitaka kuhakikisha kuwa wazuraraji hawapo basi subiri maandamano ya Chadema yatokee muone wenye kazi ni wangapi!

Nadhani sasa umekuja kwenye point yako kwamba wanapenda umbea na wewe tayari ni mwathirika wa huo umbea maana umeshaanza tabia za kimbea.
Labda nikuulize wewe maandamano yameingiaje hapa kama siyo UMEANZA TABIA ZA KIMBEA WEWE MWENYEWE jenga hoja na utetee lile ambalo ni la haki penye mapungufu turekebishane.

Suala la maandamano ni la kudai haki na wengi wanaingia kwenye maandamano ni wale walionewa siyo watu kama wewe wanaopanda magorofani na kuanzisha thread na kupiga picha za maandamano wakati wanawake wanaandamana wewe mwanaume mzima uko kwenye keybord na kurusha thread ukiwa kwenye maghorofa ya wanaume wenzako kua Broda! Acha umbea na udaku.
 
Mtanibishia sana mkitaka kuhakikisha kuwa wazuraraji hawapo basi subiri maandamano ya Chadema yatokee muone wenye kazi ni wangapi!

mada yako ilikuwa haina element yeyote ile ya kisiasa lakini pia ungeweza ku defend hoja zako bila kutumia mambo ya kutaja vyama vya siasa, sasa thread yako itaharibika muda si mrefu kwa watu ku side kwa kutumia vyama vyao, hebu tuambie maandamano gani ya kisiasa yanafanyika mikoa mingine halafu wafanyakazi wa serikalini, wafanyakazi w makampuni makubwa na wafanyabiashara wakubwa wanashiriki? kwa hiyo wasio na kzi hawatakiwi kushiriki maandamano

kumbe ulikuwa una lako

anyways hakuna ukweli wowote kwenye mada yako zaidi ya inferiority complex and life defeat
 
Hapo sipo kabisa,naona mnatuonea hapa!mengi naona mabaya kuliko mazuri,mengi niya kufikirika kuliko uhalisia.
 
Mr. Rocky labda unaishi bwawa la Ma****i kule maeneo ya relini njoo huku maeneo ya Clock Tower uone wanaume wenye ndevu lakini hata ukishindia maji na pilipili wanajua!
Huko Bwawa la mavi siyo Arusha na Arusha pekee ni Clock Tower...
 
mie nshakoma, watu wa hii mikoa miwili hii, wana hasira sana utadhani wanakulaga manyigu. hawapendi kabisa kuambiwa ukweli, mweeeeeeee!
 
Mtanibishia sana mkitaka kuhakikisha kuwa wazuraraji hawapo basi subiri maandamano ya Chadema yatokee muone wenye kazi ni wangapi!

mkuu umeniacha hoi balaa kumbe ndio ulikuwa unataka kusema hilo mkuu :focus:
 
Back
Top Bottom