Dr leader
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 1,077
- 1,444
Healing
Juzi nilikuwa Nyamagana, ndani ya ukumbi wa Tanzanite, tukizungumza kuhusu healing.
Nikasisitiza jambo moja muhimu sana:
Mtu inaweza kupita miaka 10… na bado hajapona.
Kwa sababu healing si tukio la siku moja, ni process.
Na zaidi ya yote, ni suala la utayari wa ndani.
Ndipo jamaa mmoja akasimama akasema:
“Mi nishaheal kabisa, niliachana na mke wangu miaka 6 iliyopita.”
Nikamuuliza
“Mkeo anaitwa nani?”
Akasema: Annastazia Johnson.
Nikamtazama, nikamwambia kwa upole lakini kwa uhakika:
“Mkeo sasa yuko kwenye ndoa mpya, ana mapacha wawili, ana furaha sana…
Na ukweli ni kwamba hata hakumbuki kama aliwahi kuolewa kabla.
Mtoto wako pia sasa anatumia ubini wa mume wake wa sasa.
Na wiki ijayo wanaenda vacation Uturuki.”
Ukimya ukatawala sekunde chache.
Nikamalizia:
“Kabla hawajaoana, nilikuwa mshauri wao wa ndoa… ndiyo maana nilipolisikia hilo jina, nikamfahamu.”
Ghafla… yule jamaa akalipuka:
“Yule ana mambo mengi hawezi kuolewa! Hakuna mtu angeoa ile takataka!”
Matusi yakaanza kumwagika… hasira, chuki, maumivu—vyote vikaanikwa wazi.
Nikamtazama tu nikamwambia:
“Unaona sasa… bado hujaheal.”
Ukikimbia healing, haimaanishi umepona.
Ina maana umeahirisha maumivu.
Na siku moja… yatakurudia kwa nguvu mara mbili.
Healing si kujisahaulisha.
Healing ni kukubali.
Kukubali kuwa umeumizwa.
Kukubali kuwa imekwisha.
Kukubali kuwa huwezi kubadilisha kilichopita.
Kwa sababu:
👉 Maumivu ukikubali, yanakufundisha.
👉 Maumivu ukiyakubali, yanapungua.
👉 Maumivu ukiyakataa… yanakutawala.
Ukishaumia na ukakubali, utaumia mara moja au mbili tu.
Lakini ukiyakataa maumivu… utaendelea kuumia tena na tena.
Usijidanganye umeheal kwa sababu umepita muda mrefu.
👉 Bado unachukia?
👉 Bado una hasira?
👉 Bado unalipuka ukikumbushwa?
Kama jibu ni ndiyo…
Bado una safari ya kufanya.
Abuuabdillah ✍️
0744 883 353
Mwanza