Nicas Mtei
JF-Expert Member
- Dec 21, 2010
- 11,556
- 7,113
Yawezekana unapita katika magumu na unaona hakuna njia tena na unakata tamaa. Umefika mahali na unasema siwezi kupata kazi tena, hii kazi siwezi tena, haya mahusiano yamenishinda, hii NDOA imenishinda, hawa watoto wamenishinda, hii shule imenishinda, siwezi kujenga, hii biashara imekufa, siwezi kuwa na biashara tena, n.k.. Nakusihi sana usikate tamaa
Usikate tamaa wala kujiona huwezi. Kitu cha muhimu hapa ni kujitambua kwanza na kufahamu nia hasa ya Mwenyezi Mungu kukuleta hapa duniani. Binadamu ulipoumbwa na Mwenyezi Mungu na ukaletwa hapa duniani hukuletwa kuja kuteseka au kuja kuwa msindikizaji wa wengine ambao waliumbwa kama wewe ulivyoumbwa.Uliletwa kwa makusudi maalum na kila dakika unayoishi hapa duniani kumbuka hairudi tena na ikishaenda imeenda.
Badala ya kukumbatia magumu, inatubidi kuelekeza mawazo yetu kwa Mungu na tujue ya kwamba yeye yupo kwa ajili yetu na nguvu yake ipo kazini kwa ajili yetu. Tufike mahali tuone ya kwamba iwepo njia au isiwepo Mungu ndiye njia, Amini kuwa ipo siku nawe utafanikiwa kama wengine.
Kwa hiyo unapokuwa unataka kukata tamaa kwa kushindwa kutimiza lengo Fulani kwenye maisha au kwa kufeli shule,kufeli biashara, kufeli kwenye mahusiano/mapenzi, kufeli maisha, kufeli kupata kazi, kufeli kwenye kilimo au hata kufeli kiimani, unapaswa kwanza kutambua lengo la Mungu kukuleta hapa duniani.Hakuna sehemu yoyote iliyoandikwa kuwa umeletwa duniani kuja kufeli.hakuna sehemu yoyote iliyoandikwa kuwa umeletwa duniani kuja kuangalia wengine wakisonga mbele na wewe ukirudi nyuma.
Mungu Ni Mwema Siku Zote, Humpa Kila Mtu Sawasawa Na Mapenzi Yake, Ukishindwa Sehemu Moja Ya Maisha Jaribu Sehemu Nyingine Utaweza Tu, Hakuna Aliyeumbwa Kukosa, Unaweza Tena Sana, cha kufanya ni kujiamini tu.Ukijiamini kama unaweza basi hakuna kitakachokuwa kigumu kwako, usijipe moyo wa kushindwa hata siku moja. Ukikata tamaa tu kila siku utakuwa mtu wa kulia na kujuta na mafanikio kwako yatakuwa magumu sana kupatikana.
Kufanikiwa kumewekwa kwa kila mtu hapa duniani bila kujali umri au dini. Usiangalie una umri gani sasa na usiangalie umetokea familia gani wala mazingira ya sehemu ulipo wala elimu uliyonayo, unaweza kufanikiwa kama utaambatana na waliofanikiwa na kuachana na maneno ya waliokata tamaa za maisha. Usiwape Watu nafasi wakucheke, Wape Nafasi Watu wajifunze Kutoka Kwako.