Usikate tamaa, kuwa mkakamavu na mwenye bidii ya kutafuta

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
8,181
11,601
Ukiwa mvivu, mlegevu na asie na bidii, maarifa wala kujituma katika kufanya kazi, kila kitu kwako utaona kimekosewa, kina makosa, dosari au kasoro nyingi sana...

Utaishia kulala sana magetoni nyumbani na ukiamka utakunywa chai ya mama na kuanza kulalamika tu, kulaumu, kughadhabika na kuhemka mno, kutokana na hali duni ulonayo....
Mafanikio ya wengine utayaona kero kwako.
Utasumbuka na kupata tabu sana kisaikolijia. Muda waenda mbio na hakuna extra time, umri nao unasonga huna mke, mtoto wa kusingiziwa, wala ka-ploti, na nguvu za kijinsia zinakusumbua, halafu fainali uzeeni 🐒

Maisha ndio haya haya, biashara ndio hizi hizi, fusra ndio hizi hizi, ni utayari wako tu...
Toka mafichoni usizubae...

Kupanga ni kuchagua, kua maskini au tajiri ni uamuzi wako...

Zidisha juhudi katika kufanya kazi, kwani mtaji ulio nao ni nguvu zako mwenyewe, hususani nyakati hizi... Na kwa Neema na Baraka za Mungu yote yanawezekana, atakuonyesha njia, atakufanyia wepesi, utafanikiwa 🐒
 
Back
Top Bottom