Namna mifuko ya Sukari, Ngano na Sembe iliyotumika inavyoweza kubadilisha maisha yako

Jebel

JF-Expert Member
Jul 10, 2021
306
2,041
Waungwana natumaini mu wazima na kwa Neema na Baraka za Mungu majukumu yanaenda vema kwa kila mmoja wetu. Kama mambo hayaendi vema kwako usikate tamaa, kesho yaweza kuwa zamu yako ya kubarikiwa, endelea kufanya yote kwa bidii, maarifa bila kusahau kuomba na kushukuru.

Twende kwenye maada, rafiki na jamaa yangu amepiga hatua kubwa sana kimaisha kwani anamiliki nyumba nzuri sana, gari la kutembelea na mbili za biashara, anaishi vema na tayari anamiliki na Kitambi (mind you kumiliki kitambi siyo jambo jepesi hata kidogo, ukicheza kidogo kinasepa).

Biashara hii ni watu wachache sana ambao wanaifahamu na hivyo ushindani wake bado siyo mkubwa sana na hata kama kuna ushindani basi ukijifunza vizuri na kuwa mbunifu zaidi ya wenzako ni rahisi sana kutoka kimaisha.

UFAFANUZI

A. NAMNA NA SEHEMU YA KUPATA MIFUKO HII

Ili uweze kufanikiwa daima katika biashara yoyote ni lazima ujue sehemu ya kupata malighafi na sehemu ya kuuzia. Sasa mifuko hii ambayo ujazo wake ni wa 25Kg na 50Kg kwa ngano, sukari, chumvi, sembe au pembejeo za kilimo, hupatikana zaidi katika majiji makubwa Tanzania hasa D’Salaam, Mwanza na Arusha. Lakini pia sehemu nyingine kama Dodoma, Tanga na Mbeya naamini inaweza kupatikana kwa wepesi.

Kwa D’Salaam kuna madalali wanaikusanya kutoka kwa wafanyabiashara wa maduka na kisha kuiuza kwa wafanyabiashara wanaonunua bidhaa hii. Kwa Mwanza pia kuna madalali lakini ukiingia soko kuu kuna watu wanaiuza kwa hiyo unaweza kuipata bila hata kupitia madalali.

B. BEI YA KUNUNUA MIFUKO HII
Kwa jiji la D’Salaam na Mwanza mifuko hii hupatikana kwa Tsh300-400, kwa Mwanza Bei inaanzia Tsh400-500. Kwa Moshi na Arusha bei iko chini kidogo japo upatikanaji nasikia siyo mwepesi kama huna connection nzuri. Kabla ya kununua mifuko hii ni vema ujue utaenda kuuzia wapi ili upige gharama zote za ununuaji na usafirishaji na faida utakayopata.

C. SOKO LAKE
Kama nilivyosema hapo juu, biashara yoyote ili uweze kuifanya vema ni lazima ujue soko la bidhaa yako. Sasa biashara hii, soko lake ni MIGODINI hasa migodi ya dhahabu ambapo kuna wachimbaji wadodo wadogo wengi. Mifuko hii ndiyo hutumika kuwekea mawe ya dhahabu kwa hiyo kama sehemu kuna wachimbaji wengi unaweza kuona ni jinsi gani mifuko hii itahitajika sana. Soko lake limetofautiana kutoka sehemu moja hadi sehemu nyingine kutokana na utamaduni na mazoea ya watu, hapa Nina maanisha;
  • Maeneo yote ya Kahama, yaani migodi kama Mwime, Mavumbini, kwenda hadi Kakola kote wanatumia mifuko ya 25Kg zaidi kwa hiyo kama soko lako limelenga maeneo haya ya Kahama, Masumbwe, kwenda hadi Runzewe ni vema ukanunua mifuko ya 25Kg hasa mifuko ya ngano ya Azam.
  • Maeneo yote ya migodi Geita, Katoro hadi Nyarugusu wanatumia zaidi mifuko ya 50Kg na zaidi mifuko ya sukari ya TPC ndiyo yenye soko sana na inatoka kwa kasi ya 5G.
NB. Kuna maeneo mengi sana ambayo uchimbaji wa dhahabu unafanyika katika Mikoa ya Tabora, Mara na Shinyanga hivyo kama kijana ni vema ukatembea ili ufanye research na kuona namna unavyoweza kutoka kimaisha na kuacha kutoa lawama kila siku kwa serikali na kwa mtu ambaye hata hayupo anymore.

D. BEI YA KUUZA MIGODINI
Kwa migodi ya Geita mifuko hii ya 50Kg huuzwa na wafanyabiashara wadogowadogo wenye vijiduka migodini kwa bei ya Tsh 1000. Hivyo ukiweza kuipata kwa Tsh 400 plus gharama za usafiri unaweza kuwauzia hawa wenye maduka kwa bei ya JUMLA ya Tsh 700 na kwa kila mfuko unaweza kupata faida ya Tsh200.

Kwa kuwa bidhaa hizi gharama ya ununuaji ni ndogo, utagundua kuwa faidi hii ni nzuri sana kwani ukiwa na 1.5M kwa mfano unaweza kununua mifuko hadi 3750, idadi hii ya mifuko ukipata faida ya Tsh 200 kwa kila mfuko ni sawa na Tsh 750,000. Hii pesa kwa trip siyo mbaya kama ukiweza kupeleka mara mbili tu kwa mwezi basi utakuwa na uhakika wa kupata hadi 1.5M kwa mwezi, hapa huwezi kuendelea kutoa lawama kwa mtu asiyekuwepo anymore duniani.

Jamaa yangu huyu alianza na laki5 kwa sasa anajaza gari zima yaani anapeleka zaidi ya mifuko laki 2 sasa zidisha mara 200 tu kwa kila mfuko.

Kwa Kahama mifuko ya 25Kg bei ya rejareja ni Tsh700-800 kwa migodi mingi kwa hiyo unaweza kuangalia namna ya kununua mifuko hii kwa bei ya chini ili uuze kwa Tsh 600 JUMLA ili ubakie na faida.

USHAURI: Kama mtaji wako ni mdogo, unaweza kununua mifuko labda ya laki5 kisha ukaenda mwenyewe migodini na kuiuza kwa bei ya chini ya wauzaji wa kule, yaani kama wanauza 1000 wewe unauza 800, hapa utawahi kumaliza na kurudi kununua tena, ndani ya mda mfupi ni lazima mtaji wako utapanda ghafla kwani biashara hii faida yake imefichika ila ni nzuri sana.

E. CHANGAMOTO ZAKE
Kila biashara lazima inachangamoto zake, kwa biashara hii changamoto kubwa ni ukopaji. Wachimbaji wengi wanakopa mifuko hii kwa ahadi kulipia baada ya kuuza mawe ya dhahabu kwa hiyo kidogo ni changamoto lakini kama upo focused unaweza kutafuta namna ya kukabiliana na changamoto hii na biashara ikasonga vema.

USHAURI NA HITIMISHO
1. Hapa kuna watu wanafanya biashara hii kwa hiyo ukiona povu, vipondo, criticisms, isikukatishe tamaa kama umependa idea. Go ahead fanya research, pata data nzuri, ingia kwenye biashara sehemu yoyote ulipo kama kuna migodi; Iwe Singida, Mpanda, Mara, Arusha bahati nzuri Tanzania nzima Mungu ameibarikia madini.

2. Biashara yoyote ya migodini inahitaji focus ya hali ya juu sana, kuna wafanyabiashara ya maku kwa hiyo usipokuwa makini unaweza kujikuta faida yote wanakula wao na baadaye watakula mtaji na wewe utajikuta unageuka kuwa mchimbaji wa kuingia shimoni kwa malipo ya siku. I’ve seen some people harvesting this end.

3. Kabla ya kuanza, nasisitiza kufanya ka utafiti ili ujue namna rahisi na sahihi kwako kuifanya shughuli hii, unaweza kwenda kule na kujenga kibanda kisha ukamweka kijana halafu wewe ukawa unaingia town kukusanya mzigo na kumpelekea kijana, hapa jitahidi upate kijana mwaminifu ili usije kujilaumu. Utafiti huu pia utakusaidia kujua aina ya mifuko inayohitajika katika mgodi husika.

NAKUTAKIA MAFANIKIO MEMA NA MUNGU AKUTANGULIE

Aquila Non Capit Muscas!!
 
Ikija fursa ya kuuza lita tano, kumi na ishirini za madumu ya mafuta ya kula nishtue maana naona vimejaa sana hapa nilipo
 
Mbona sisi huku twainunua 600

1000 ni huko Buhemba

Inawezekana mkuu bei inatofautiana kutoka mgodi mmoja hadi mwingine, kulingana na idadi ya wachimbaji na thamani ya mawe. Kwa mfano kama mgodi ndo umehira na dhahabu ikawa ni ya sesa lazima mifuko ipande bei hadi 1500 niliwahi kushuhudia kipindi fulani pale Mavumbini.
 
Duuh!! Umetisha mkuu, ila naona ka competition fulani kitakachopelekea kushuka kwa faida ya muuzaji coz deal Kama hiyo ni wengi watakaokuwa wanapiga
 
Eee ndio ndio
FCEBF810-3E11-490E-840A-E7A6FE571768.jpeg
7543FF5A-4647-4886-8D0C-6F66C4D53079.jpeg
FCEBF810-3E11-490E-840A-E7A6FE571768.jpeg
7543FF5A-4647-4886-8D0C-6F66C4D53079.jpeg
76F49A11-530F-4F7E-A03B-5F1699C776EC.jpeg
 
Back
Top Bottom