Usije ukasema hukuambiwa

Usije ukasema hukuambiwa

Muuza simu used

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2017
Posts
4,393
Reaction score
7,108
Ni hivi kama unataka kuowa mwanamke na kwao yeye ni mzaliwa wa kwanza na kwao wamezaliwa zaidi ya watoto watano na wewe muoaji pia ni mzaliwa wa kwanza na kwenu mpo zaidi ya watatu usioe huyo mwanamke hasa kama kwao wanatoka kwenye familia maskini.

Unajua kwanini?,kumbuka kama wewe una uhafadhali kidogo wa maisha mashemeji zako wote watataka msaada kwako kwa mgongo wa dada yao ambaye ndio tegemeo lao,na hapo usisahau na wadogo zako pia watataka msaada kwako kwa vile wewe ndie kaka yao!

Huo mzigo utaokuandama hutakaa ufanye maendeleo yeyote katika maisha yako na sana sana utajikuta unaingia kwenye mtafaruku isiyoisha na ndoa itageuka kuwa shubiri kweli kweli!

Nakushauri tu kama una pesa za kuunga unga hadi uuze simu used hakikisha kama wewe ni firstborn basi owa last born au last born.

Usije ukasema hukuambiwa
 
Nataka kuuza simu yangu used niunge unge haya maisha..
 
Usiwe na Imani ya hivyo aisee kuna muda mafanikio huja tu, yani kila unalo gusa linaenda.
 
Msaada kutoa si lazima. Unaoa mke si familia.

halafu acha uchoyo mkuu.
 
Mnazidi ongeza ma conditions hii kitu inakua more complex kinoma... unaweza amua usioe maisha yako yote uwe father timoti....
 
Unaonekana mbinafsi sana, itakuwa Kaka yako ndiye kaoa hivyo basi roho inakuuma sana kusaidia ndugu wa mkeo, kusaidia haimaanishi mpaka uwe first born, unaweza first born na ukawa kiazi vilevile
 
Mkuu, hawa walioshika nafasi ya pili na ya tatu hawawezi kukuelewa.
Tena uwe first born uliyetoboa, dah hatari
 
Hizo ni ngekewa..uwezi kukesha macho ukisubiri.
Bado hujajua utafutaji mkuu, unaweza ukawa unapambana lakini hufanikiwi ila kuna muda ukifika mambo yananyooka simple,

Usiku wewe umepewa kimtaji au kiduka cha urithi na kinyumba una maisha umwyapatia

Walio anza zero to hero ndio watanielewa.
 
Bado hujajua utafutaji mkuu, unaweza ukawa unapambana lakini hufanikiwi ila kuna muda ukifika mambo yananyooka simple,

Usiku wewe umepewa kimtaji au kiduka cha urithi na kinyumba una maisha umwyapatia

Walio anza zero to hero ndio watanielewa.
Hizo ni iman mkuu...jitume
 
Back
Top Bottom