Usije sema sikusema, nasema haya kabla sijafa

Usije sema sikusema, nasema haya kabla sijafa

Mungu afanyii mtu wepesi, uchaguzi wa mtu ndo matokeo ya maisha ya Mtu, Mungu yupo kutimiza neno lake!

Aliposema mshahara wa Dhambi ni mauti, alimanisha, ukifanya dhambi utakufa, usipofanya utaishi na kufurahia, wepesi jifanyie mwenyewe!
Mwanzo 20:6
[6]Mungu akamwambia katika ndoto, Nami nimejua ya kwamba kwa ukamilifu wa moyo wako umefanya hivi, ndipo nami nikakuzuia usinitendee dhambi, kwa hiyo sikukuacha umguse.

Umeelewa mtu wa Mungu? Ukifungwa(Ukitiwa uzito) ni rahisi kutenda dhambi, ukitiwa wepesi/majaaliwa/neema/kudra za Mungu zikiwa nawe.. ni rahisi kuiepuka dhambi.
 
Hii vita inaitaji ujasiri sana
Mungu ndiye Bwana wa majeshi, Jemedari wa vita.. Akiwa upande wako, Je ni nani atakayeinuka dhidi yako na kukushinda? HAKUNA.

Ili ukae upande wa Mungu.. TUBU, nakusihii sana TUBU Kwa moyo wako wote.
 
Mungu anatupenda, yes.
Tutubu ,yes
Tuache dhambi , yes.

Ila mambo ya wewe kufa ,mi hayanihusu Mkuu.
Utajifia zako huko, watakuzika.
Watamalizana na wewe, mi hata sitajua.
Kama ambayo we hutajua.

Tusifanye maisha ya kumpendeza Mungu ni vitisho.
We utakufa kivyako,watahusika ndugu zako huko.
 
Mi sijatubu bado ila kwanza nimeanza kupunguza (kujitenga ) na kimoja kimoja kinachonifanya ni angukie dhambini, naamin nitaweza japo najua siku nikirudi kwa Mungu lasmi nitapoteza wengi na vingi
Wakati ndio sasa, yumkini bado kuna mizigo inakushinda kuipunguza lakini kwa kutubu itaondoka yenyewe.

NIKUIBIE SIRI...

Shetani anatutumikisha kiuhalali kwakua tumempa nafasi ndani yetu, ILA kwa kutubu maana yake tunamwambia MUNGU nisaidie, Ingilia kati na uniondoe kwenye huu utumwa.. Mungu MWAMINIFU lazima atakuondoa kwenye mafungo na utumwa wote.. (Hutohitajika kuanza kupunguza kimoja kimoja, utumwa utafika mwisho/utakoma kwa wakati)

Toba ni Kuomba msamaha na msaada kwa pamoja, Mungu ni Mwaminifu ndio maana uko hai mpaka sasa.
 
Mwanzo 20:6
[6]Mungu akamwambia katika ndoto, Nami nimejua ya kwamba kwa ukamilifu wa moyo wako umefanya hivi, ndipo nami nikakuzuia usinitendee dhambi, kwa hiyo sikukuacha umguse.

Umeelewa mtu wa Mungu? Ukifungwa(Ukitiwa uzito) ni rahisi kutenda dhambi, ukitiwa wepesi/majaaliwa/neema/kudra za Mungu zikiwa nawe.. ni rahisi kuiepuka dhambi.

Mungu cannot do anything nje ya neno lake, Hakuna maana pameandikwa Mungu atamfanyia mtu wepesi!

Mungu anaweza kufanya kila kitu mpaka atakaposema vinginenevyo, utajifanyia wepesi kwa kumtii Mungu tu!
 
Mungu cannot do anything nje ya neno lake, Hakuna maana pameandikwa Mungu atamfanyia mtu wepesi!

Mungu anaweza kufanya kila kitu mpaka atakaposema vinginenevyo, utajifanyia wepesi kwa kumtii Mungu tu!
SAWA, Ila Mungu anao uwezo wa kuzuia mtu asimtendee dhambi.. si ndio?
 
Kibinadamu itaonekana umepoteza mengi, lakini utakua umefanya maamuzi ya busara sana kuiponya nafsi yako. Kati ya hivyo unavisumbukia na kusema utavipoteza, utaviacha vyote hapahapa duniani. Utaondoka kama ulivyozaliwa, bila kitu.

Hakuna aliyemkamilifu, ile hali ya kunyenyekea na kuonyesha moyo wa kubadilika ndio ya muhimu.
Mungu akubariki zaidi.
 
Mungu anatupenda, yes.
Tutubu ,yes
Tuache dhambi , yes.

Ila mambo ya wewe kufa ,mi hayanihusu Mkuu.
Utajifia zako huko, watakuzika.
Watamalizana na wewe, mi hata sitajua.
Kama ambayo we hutajua.

Tusifanye maisha ya kumpendeza Mungu ni vitisho.
We utakufa kivyako,watahusika ndugu zako huko.
Nimekutisha kwa lipi? Unaogopa kifo?

Ukweli utabaki palepale... Sote tutakufa, Lakini kabla ya umauti haujakukuta ni lazima uitimize kazi ambayo Mungu alikuleta uifanye... (NASEMA HAYA KABLA SIJAFA... Namaanisha nisiposema na nikafa nitakuwa sijaitimiza kazi iliyonileta, na hapo utakapoulizwa wewe, Au mbingu au ardhi kama shahidi Je, Huyu ndugu aliwakumbusha watu WATUBU?... Kama sikukumbusha huoni utakuwa na haki ya kusema Huyo bwana hakusema alijikita kwenye kuzini na kugida mipombe kisha akatunakana watu... Lakini nikiyasema kabla SIJAFA.. nimetimiza lengo la mimi kuwepo hapa ulimwenguni.)

Tubu, ishi kwa kumpendeza Mungu..m kadiri unavyotubu ndio unazidi kuusogelea uwepo wa Mungu... Na hapo HOFU (Huko kusema kuwa NAKUTISHA) Kutaondoka.

Tubu kakaangu, tena utubu ldo hii na uache kuitumikia hiyo miungu ambayo inakuzuia kumtumikia Mungu kwa moyo wako, akili yako, na nguvu zako.

"Sote tumetenda dhambi Tutubu na Kurejea Kwa Mungu"
 
SAWA, Ila Mungu anao uwezo wa kuzuia mtu asimtendee dhambi.. si ndio?

Hana hata Kidogo! Amempa mwanadamu uchaguzi, angeweza angemzuia Adam, dhambi ya Adam ilimgharimu Yesu, why? God is principled and cannot change any of his word.
 
Hana hata Kidogo! Amempa mwanadamu uchaguzi, angeweza angemzuia Adam, dhambi ya Adam ilimgharimu Yesu, why? God is principled and cannot change any of his word.
Huo mfano wa Mungu kumzuia abimeleki asimtendee dhambi umeuelewaje?

Naweza/Tunaweza kusaidiana kama uko tayari maana naona unayo neema lakini pengine hutambui...
 
MUNGU ANAKUPENDA SANA.

Ndio, sijakosea.. Mungu ANATUPENDA SANA na ndio maana Ameuleta ujumbe huu mbele yako leo hii.

Ni uamuzi wako, Kuchagua Mema na Uzima AU mabaya na mauti.

Mimi ni mdhambi kama wewe, ndio wewe ni mdhambi kama mimi, lakini Mungu hapendi tuishi katika dhambi na ndio maana Ametupa muda wa kuwa hai mpaka wakati huu unaposoma ujumbe huu.

Fikiria wangapi wanakufa sekunde hii kabla hawajapata nafasi ya kuusoma ujumbe huu?

Mimi sitaki kukuambia kuwa kwa kufanya hivi au vile hauta pata nafasi ya kwenda peponi, Hapana... Mimi nataka nikuambie, KAMA HAUTA TUBU MADHAMBI YAKO SASA UNGALI UNA NGUVU NA UWEZO WA KUFANYA HIVYO, Basi itakuwa ngumu kuingia peponi.

Iogope Zinaa, dhambi zote hufanyika nje ya mwili.. ila Zinaa ni ndani yako, ndio ndani ya huo mwili ambao Mungu amekupa umtumikie Yeye.

TUBU, narudia tena TUBU.. Nakuomba TUBU NA UREJEE KWAKE MUNGU AMBAE NDIYE MUUMBA WETU, ACHA KIBURI, USIJIONE MSAFI... WEWE NA MIMI SOTE WACHAFU MBELE ZA MUNGU.

"Sote tumetenda dhambi Tutubu na Kurejea Kwa Mungu"

Ninamuomba Mungu, akutoe kwenye huo uraibu na hivyo vifungo vya nafsi na roho.. TUBU HUJACHELEWA NDUGU YANGU.

SAMAHANI KAMA NIMEKUKWAZA, TUBU UNIOMBEE NA MIMI.

20.08.21 (TUBU Ewe Mwanadamu)
Asante mtumishi
 
Back
Top Bottom