Usije sema sikusema, nasema haya kabla sijafa

Mtumaini Mungu

JF-Expert Member
Aug 3, 2021
879
1,061
MUNGU ANAKUPENDA SANA.

Ndio, sijakosea.. Mungu ANATUPENDA SANA na ndio maana Ameuleta ujumbe huu mbele yako leo hii.

Ni uamuzi wako, Kuchagua Mema na Uzima AU mabaya na mauti.

Mimi ni mdhambi kama wewe, ndio wewe ni mdhambi kama mimi, lakini Mungu hapendi tuishi katika dhambi na ndio maana Ametupa muda wa kuwa hai mpaka wakati huu unaposoma ujumbe huu.

Fikiria wangapi wanakufa sekunde hii kabla hawajapata nafasi ya kuusoma ujumbe huu?

Mimi sitaki kukuambia kuwa kwa kufanya hivi au vile hauta pata nafasi ya kwenda peponi, Hapana... Mimi nataka nikuambie, KAMA HAUTA TUBU MADHAMBI YAKO SASA UNGALI UNA NGUVU NA UWEZO WA KUFANYA HIVYO, Basi itakuwa ngumu kuingia peponi.

Iogope Zinaa, dhambi zote hufanyika nje ya mwili.. ila Zinaa ni ndani yako, ndio ndani ya huo mwili ambao Mungu amekupa umtumikie Yeye.

TUBU, narudia tena TUBU.. Nakuomba TUBU NA UREJEE KWAKE MUNGU AMBAE NDIYE MUUMBA WETU, ACHA KIBURI, USIJIONE MSAFI... WEWE NA MIMI SOTE WACHAFU MBELE ZA MUNGU.

"Sote tumetenda dhambi Tutubu na Kurejea Kwa Mungu"

Ninamuomba Mungu, akutoe kwenye huo uraibu na hivyo vifungo vya nafsi na roho.. TUBU HUJACHELEWA NDUGU YANGU.

SAMAHANI KAMA NIMEKUKWAZA, TUBU UNIOMBEE NA MIMI.

20.08.21 (TUBU Ewe Mwanadamu)
 
Watu Mungu wanampenda ila kwenda kwake ni kigumu
Mbona ni rahisi sana kwenda kwake.

Yeye katoa muongozo wa wazi kabisa.

Amesema... "Tubuni, Mziache njia zenu za zamani, na Mrejee Kwangu."

Mfano, ulikua mwizi, Tubu (Omba msamaha kwa Mungu kwa matendo yote ya wizi uliyowahi kushiriki, kwa mawazo, maneno au matendo..) kisha Acha kuiba mara tu baada ya kuomba toba, na Ule muda amabao ulikuwa unauutumia kupanga kuiba sasa utumie kumtumikia Mungu.

Tubu.
 
Hivi wale wa sodoma na gomora na kwampalange wanasameheka wakitubu
Tubu, narudia tena TUBU... Dhambi zetu zi wazi mbele ya Mungu, anachotaka ni Kukiri kuwa ulifanya, na umuombe msamaha. ATAKUSAMEHE

Ukitubu BADILIKA..

TUBU leo ndugu yangu, Mungu Muumba akufanyie wepesi kaka angu.
 
Naomba Mungu akufanyie wepesi, Tubu leo na urejee kwa Mungu wako kwa moyo wako wote.

Amina.
Amen Amen mtumishi

Tutubu wapendwa jumbe kama hizi isije fika kipindi tukazitafuta kwa tochi. Mungu atusaidie tutembee katika neema yake...INGALIPO. Jesus Christ alivyokuja HE said Tubuni na kuiamini injili.

HE also said ufalme wa MUNGU umekaribia...tutubu. Tushike sana tulicho nacho asije mtu akatwaa taji zetu. Tuishi humo yani, tutembee humo...upendi baina yetu uongezeke tusije tendeana mabaya.

Tulijue neno lake, tumuombe sana.....naye atatusikia na kutujibu. Tuifanye kama agenda moja kuu ya maombi.
 
Amen Amen mtumishi

Tutubu wapendwa jumbe kama hizi isije fika kipindi tukazitafuta kwa tochi. Mungu atusaidie tutembee katika neema yake...INGALIPO. Jesus Christ alivyokuja HE said Tubuni na kuiamini injili.

HE also said ufalme wa MUNGU umekaribia...tutubu. Tushike sana tulicho nacho asije mtu akatwaa taji zetu. Tuishi humo yani, tutembee humo...upendi baina yetu uongezeke tusije tendeana mabaya.

Tulijue neno lake, tumuombe sana.....naye atatusikia na kutujibu. Tuifanye kama agenda moja kuu ya maombi.
Mungu amekupa maarifa na majaliwa na neema zake naona zipo nawe.

Usimuache mkimbilie daima kwa kutubu na kutenda yenye kumpendeza hakuna mkamilifu, ila toba itatuunganisha na muumba wetu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom