Usijaribu kutoa mimba dhambi yake ni zaidi ya Jairo!

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,144
[h=2]Sunday, August 21, 2011[/h][h=3]Usijaribu![/h]

SWALI:
Hello mimi ni dada ninayeishi Iringa nina umri wa miaka 18 kwa bahati mbaya mpenzi wangu amenipa mimba na kutokana namna alivyo baba yangu Naamini akifahamu kwamba nina mimba ataniua Kwani mimi ni mwanafunzi.
Nimeongea na boyfriend wangu tumekubaliana tukaitoe.
Hata hivyo bado najiuliza kama kutoa mimba (abortion) ni kitu sahihi?
Na je, nifanyeje Kwani nipo kwenye njia panda.
MAJIBU:
Mdogo wangu pole sana kwa yaliyokukuta hasa kitendo cha kujiingiza kwenye masuala ya mapenzi badala ya kukomaa na shule kwanza.
Sikufichi umeshachanganya mambo na kuna gharama utalipa kwa maamuzi yako uliyoyafanya.
Jambo la msingi ni kwamba sidhani kama kuna anayehusika na utoaji mimba anayeweza kukwambia ukweli kuhusiana na kutoa mimba (abortion)
Kutoa mimba ni uuaji (murder) na kutoa hiyo mimba kutakufanya uishi kama muuaji sawa na wauaji wengine wanaoua watu na hiyo hatia itakaa moyoni mwako miaka yako yote hapa duniani.
Ukweli ni kwamba kovu la hisia za kutoa mimba zitakuwinda maisha yako yote na hatia (guilt) hutisha.
Utajisikia huzuni, hasira pale ikitokea mtu anaanza kuzungumzia suala la utoaji mimba (abortion) pia unaweza kujikuta una hisia mbaya unapowaona watoto wadogo hasa wale watakaokuwa umri sawa na yule mtoto uliyemuua kwa kutoa mimba yake pia unaweza kujikuta hapendi kabisa kushika watoto au kuwagusa watoto wenye umri sawa na yule ambaye angekuwa mtoto wako.
Ulipokuwa unafanya mapenzi na huyo boyfriend wako uliamua, na hamkutumia njia yoyote ya kuzuia mimba na ulijua wewe na boyfriend wako kwamba hicho kitendo kinaweza kusababisha mimba, hivyo basi wewe na boyfriend wako mnawajibika kwa ajili ya kuhakikisha huyo mtoto (kiumbe kisicho na hatia) anatunzwa tumboni na kuzaliwa salama na mnamtunza kama wazazi.
Pia ufahamu kwamba madhara ya kutoa mimba ni zaidi ya unavyofikiria, kuna wanawake hupoteza maisha wakati wa kutoa mimba na wengine huugua kiasi cha kufa.
Inawezekana ni kweli baba yako atakasirika sana kusikia una mimba, pia Naamini mzazi mwenye busara hawezi kumuua binti yake kwa kuwa ana mimba ya mjukuu wake. Naamini baba yako atakasirika na mwisho atakusamehe.
Kama ulikuwa unawaza kwamba siku moja utakuwa na mtoto baada ya ndoa au harusi kubwa, ni muhimu na busara kuanza kufuta hayo mawazo na badala yake tunza hiyo mimba na mtoto atazaliwa na maisha yataendelea kama kawaida.
Hakuna Tatizo linalotokea hapa duniani ambalo ni jipya yote yalikuwepo na maisha yanaendelea.
Inawezekana katika kutoa mimba ukapoteza kizazi au uzazi na siku moja ukaolewa na kushindwa kupata watoto na utajisikiaje utakapomwambia mume wako mpenzi kwamba huweza kupata mimba kwa kuwa ulimuua mtoto ambaye alikuwa tumboni mwako?
Inawezekana kwako kupata hiyo mimba ni bahati mbaya, hata hivyo mbele za Mungu huyo mtoto si bahati mbaya (accident) bali ni mpango wa Mungu kwamba azaliwe duniani na mtoto kama mtoto hana kosa ila wewe na boyfriend wako.
Je, ingekuwaje kama wazazi wako nao wangekuua ungali tumboni mwa mama yako?
Jiulize ni namna gani wangekosa unavyocheka, unavyo smile, unavyotoa machozi, unavyowapenda na vitu vyote vinavyowapa furaha ya maisha.
Achana kabisa na wazo la kutoa mimba.
Kumbuka kutoa mimba ni dhambi ya uuaji na hapa Tanzania pia ni kosa

Wewe kdnapper umetokea wapi tena?simply mwenye mada kaongelea abortion ya mtoto aliye tumboni,wewe unaongelea shahawa,kwa nini usijibu mada ilivyo alafu ukatafuta mda ukaleta ya kwako ya shahawa kama unapenda?mnaboa sana because of your irrational thinking,think positively great thinker!

Peleka uchangudoa wako maaluni mkubwa weye.

Jamani mbona mmekuwa wakali namna hiyo? Mwelewesheni taratibu sio wote wenye uelewa sawa!

Mimi nadhani alijaribu kuunganisha dhambi ya kutoa mimba na dhambi ya kutumia condom (kuna dini nyingine wanaconderm kabisa kuwa hii bi dhambi) so kama zote ni dhambi tufanyeje - tuache kufanya mapenzi kabla ya ndoa na ndani ya ndoa tuzae tu tukaijaze dunia hata kama hatuna uwezo wa kuwalea hao watoto - hakuna kutumia kinga. Ni thread nzuri hii kuidiscuss but nadhani zipo pia threads ambazo zilishalizungumzia hili jambo kwa kina.

sentensi ya huyo mwana jf haieleweki, uhusiano wa kidnapping na condom, which is which?

ushauri wangu. hata kama babu i mkali vipi, kuna mtu fulani ataweza kukusaidia tu, kimbilia huko. ni hulka ya binadamu kwa kuwa sasa una mimba kila mtu ( na hasa babu) atakuona wewe ni muhuni na mtu usiyefaa. lakini mtoto atakapozaliwa hapo ndo utaona faida ya wewe kutokutoa mimba, hata hao walokuwa wanakukataa watajirudi tu.. mpe mtoto wako maisha, huwezi jua pengine ukishazaa huyo, ndo basi hutafanikiwa kuzaa tena.. give life to your child... MUNGU AKUPE NGUVU NA KUKUVUSHA WAKATI HUU MGUMU

kumbuka mwanao anajulikana kwa Mungu na wanadamu

Yeremia 1:5 - MWANAO ANA KAZI MAALUMU MWACHE AJE KUIFANYA
"Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la
mama yako nilikujua,
kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi
maalumu,

nilikuweka uwe nabii kwa mataifa.''

Mithali 24:12-13 -OKOA MAISHA YA MWANAO
Okoa wale wanaoongozwa kwenye kifo,
wazuie wote wanaojikokota kuelekea
machinjoni.
Kama mkisema, "Lakini hatukujua lo lote
kuhusu hili,''
Je, yule apimaye moyo halitambui hili?
Je, yule awalindaye maisha yenu halijui hili?
Je, hatamlipa kila mtu kulingana na
aliyotenda?

ukweli mtu anaetoa mimba ni mnyama! Sio siri ni muuaji! Bora uuawe kuliko kuua. Wazo na makubaliano mliyoweka we na bf wako ni ya kiibilisi kabisa.

Jamani mbona mmekuwa wakali namna hiyo? Mwelewesheni taratibu sio wote wenye uelewa sawa!

Mimi nadhani alijaribu kuunganisha dhambi ya kutoa mimba na dhambi ya kutumia condom (kuna dini nyingine wanaconderm kabisa kuwa hii bi dhambi) so kama zote ni dhambi tufanyeje - tuache kufanya mapenzi kabla ya ndoa na ndani ya ndoa tuzae tu tukaijaze dunia hata kama hatuna uwezo wa kuwalea hao watoto - hakuna kutumia kinga. Ni thread nzuri hii kuidiscuss but nadhani zipo pia threads ambazo zilishalizungumzia hili jambo kwa kina.

Siyo hivyo babe! Unajua kila mahali kuna makosa kwa yule anayempa mimba na yule anayetoa pia na hapa tujaribu kujenga hoja na siyo kutetea upuuzi wa huyu dada kaniudhi kama nini! Mimi nadhani angetoa hoja yake tufanyaje kuzuia au kupunguza hali hiyo lakini yeye anakuja na kuhalalisha upuuzi wake humu!

ushauri wangu condom is a better option ikitokea bahati mbaya toa usiwe na wasi wasi.

Siyo hivyo babe! Unajua kila mahali kuna makosa kwa yule anayempa mimba na yule anayetoa pia na hapa tujaribu kujenga hoja na siyo kutetea upuuzi wa huyu dada kaniudhi kama nini! Mimi nadhani angetoa hoja yake tufanyaje kuzuia au kupunguza hali hiyo lakini yeye anakuja na kuhalalisha upuuzi wake humu!

so ndio umepata faraja kwa hayo maneno makali uliyoyatoa?

Back
Top Bottom