Usijaribu kununua gari ya mwanamke, utajuta

zipumbovu

Member
Nov 27, 2023
6
136
Habari wakuu, huu Uzi ni maalum kwa ndg zangu wote ambayo pengine mnatarajia kukunua gari kwa mtu (yaani gari iliyotumika bongo)

Madalali wamekuwa na tabia ya kuzisifia sana gari ambazo zimekuwa zikimilikiwa na wanawake, utaskia hii ni gari ya mdada iwai chap.

Wengi wanaamini gari ambayo imaendeshwa na mwanamke pengine inaweza kuwa ni nzuri yaani nzima, haijatumika vibaya.

Ukweli ni kwamba wanawake hawajui kutunza magari, wanajua kuendesha kwa tahadhari, lakini hawawezi kuitunza gari, yaani kuzingatia service.

Nimewahi kununua gari kwa mwanamke (nilijuta sana) kwa mwonekano ilikuwa nzuri lakini hakuwa akizingatia service (gari ilikuwa mbovu mbovu tuu).

Nina jamaa yangu ambae wiki iliyopita amenunua gari kwa mwanamke, kwasasa jamaa unaweza kusema ni mgonjwa (gari ipo inampasua kichwa mno )

Kama hutaki stress basi nakushauri ukiskia hii ni gari ya mdada basi nenda na jopo la mafundi kwenye ukaguzi..

NB: Wadada hawajui kutunza magari
 
Hii iende sambamba na Wanaume wenye Wake zao wanaotumia magari kuhakikisha wanasimamia magari hayo kikamilifu kuepusha hatari.

Alichosema mtoa mada ni sahihi kwa 100% wenzetu wanahitaji kusimamiwa sana kwenye hii sekta.

Waweza kuta Steering Fluid imekauka yeye anatwanga tu pedal... too risk.

Nimewahi ona pale parking ya UDSM mdada anaomba msaada kumbe rejeta imekauka ina wiki kadhaa hakuna maji yeye anaendesha tu.

So kuna point hapa
 
Mwenzio kuna siku gari ikanizimia ghafla njian nikampigia fund nikidhan ni ishu ndogo arekebishe nisepe. Fundi kuja anasema engine inabid ifanyiwe overhaul sijui cyllinder head sijui kitu gan kimepinda sijui kisa sikuwa nacheki maji wala oil.Mimi ni kutia funguo na kusepa😂 Hannah
 
Back
Top Bottom