Huu uzi na mleta uzi ni watu wanaotumika kuleta fitna.
Nawaomba
Moderator mziangalie vizuri sana hizi nyuzi.
Hawa USA wanataka kuanzisha au wameshaanzisha chokochoko za kutuchafua Tanzania?
Ukiitazama hii habari, ukiitazama habari ya aliyechana Qur'an, ukija kusoma nyuzi kama hii za.huyu anayejiita
Mcqueenen hapa JF.
Ukifikiri ya Makonda kunyimwa visa, ukifikiri ya Watanzania kuondolewa kwenye bahati nasibu ya green card, ukifikiri ya World Bank, ukifikiri ya msaada wa silaha kutoka USA, ukifikiri ya Tanzania kutangazwa siyo salama sana kwa utalii.
Kwa yote hayo unaweza kuunganisha dots na kukuta tayari jungu limeshapikwa na linangoja kupakuliwa tu.
Allah tulinde na wenye kutia wasiwasi kwenye nyoyo za watu. Allah tuepushe na shari na hassad zote, tunazoziona na tusizoziona.
Haya si madogo kwa kiwango chochote kile, inabidi serikali, wasio na dini na wenye dini, tuwe macho na kuwa na subira na tusifanye pupa kwa hizi fitna zinazoendelea.
Tusikubali kuchonganishwa.