Nakubali kwamba mwalimu alikuwa kiongozi mahiri; hilo siwezi kulipinga. Ninachokipinga ni justifications zako za kutetea mapungufu yake. He was HUMAN and NOT GOD NOR AN ANGEL.
Vita ya kagera na Umeme wa mgao ni two separate elements ambazo hazilinganishiki. Na sikumbuki hata mara moja kusema naunga mkono umeme wa mgao na kuzalisha umeme kwa utaratibu wa emergency; unless you just wanted to bring that as a justification of your lame argument.
Eti Mwalimu hakutaka ku diktate; unayajuwa yaliowakuta akina Bibi Titi Mohammed? Fukua upate uhalisia wa mambo. Kambona had to flee abroad, merely because he had a different view; sasa hapo utasema nini nini hicho? Mwalimu alisimamia 'fikra sahihi za mwenyekiti' wakati wote; ukileta valangati hata ya ku kunja uso - RUPANGO!
Ishu ya kutosikiza mabeberu ni sahihi; ila alipaswa kuleta maendeleo na sio tu kutowasikiza mabeberu. Kweli makao makuu ya ukombozi wa nchi za afrika yalikuwa DSM na kuna wakati yakiongozwa na Brigedia General Hashim Mbita. tumechangia sana katika kukomboa Afrika; ikiwemo Afrika ya Kusini ambao hadi hivi karibuni walikuwa wamesahau fadhila na kuwataka watanzania waingie kwa viza. Ila kuwakatalia mabeberu sio kuwanyima wananchi basics. mbona Cuba na China walifanikiwa na sisi ndio ilikuwa mifano yetu? Poor management and supervision. Yeye alikuwa akiona TV ya Satelite IKULU, sawa? Kama hakutaka kusomesha familia yake au sijui unasema kitu gani, hilo ni shauri lake; ila kusomesha familia yako sio ufisadi; tena una wajibu wa kufanya hivyo kama mzazi.
Kuhusu TV, si angeruhusu walau Watanzania Bara waangalie TV; kule Zanzibar Karume alifungua kituo cha kwanza cha Runinga coloured 1964. Yeye tangu 1961 - 1985; hata TV????? That was shameful. Kwani ilikuwa lazima afungue cha mtu binafsi, kwani ile ya Zanzibar ya mtu binafsi?
Kuhusu NYUMBA; Nyerere hakuwa na mpango wa kustaafu na alijua atafia IKULU. Mwinyi alimuenzi kwa kumpatia Nyumba ya Msasani na kuagiza jeshi wamjengee jumba la kipekee kule Butiama. Ushafika ukaliona hilo Jumba; kwako wewe lile Banda?
Mwisho, kama alitaka kuishi kama mtanzania, angefia Muhimbili au sana sana India. Yeye ni mbinafsi as any other leader. Ana mafanikio na ana mapungufu PERIOD.
Kuhusu hiyo nyimbo; ni kwa kuwa ndio slogan ya kufanya rioting; haina any significance what so ever.
(1) ni bora vita ya uganda alishinda kuliko vita ya ufisadi, mgao wa umeme iliyotushinda sasa na maandamano yasiyo na tija kila kukicha,(2) azimio la arusha lilishindwa kwa sababu nyerere hakutaka kudictate, alitaka watanzania waione nia thabiti katika maneno na matendo ya azimio hilo,ila tamaa za watanzania wachache na hasa wana ccm kipindi hicho hawakutaka usawa aliouwaza nyerere!(3) hakuna mzalendo kama nyerere, aliyeweza kufanya maamuzi magumu na kuyasimamia hata kama mabeberu wakiweka vikwazo.ndio maana aliona ni bora kuzalisha malighafi za kitanzania na zitumike tanzania kuliko kuruhusu soko holela!(4) ni km ilivyo tbc leo,haiwezi kuzungumzia mabaya ya rais,hata voice of amerika haiwezi kufanya hivyo!ni mtanzania gani wakati huo aliomba kuanzisha chombo cha habari akakataliwa hatuna ushahidi,hata hivyo nia ya ndani ya mwl na utashina utu wake vinamfanya watanzania tulio wengi tuendelee kumuona alikuwa kiongozi asiemithilika katika ulimwengu wa sasa!hauwezi ukaongea upuuzi kuhusu mwl mbele ya kadamnasi usipigwe mawe je bado leo hakuna uhuru wa kuongea,mbona bado watu tunamheshimu na kumuona kielelezo!hili sio kwa watu wa hali ya chini tu hata wasomi wa vyuo vikuu pindi wanapodai haki zao huimba ule wimbo maarufu wa " kama sio juhudi zako nyerere.....kama sio juhudi zako nyerere ....."hauwezi kupata urais wa nhi hii kutokana na kura za watanzania km utamponda mwl jukwaani!je bado hakuna uhuru mpaka leo?kubali ukweli mwl nyerere hafananishiki katika kizazi cha sasa!jaribu kufikiri km wewe ungekuwa rais leo ungekubali kufa maskini?kuishi kijumba km cha mwl?kusomesha wanao hapahapa bongo?kutenganisha famailia na uongozi?kujali nchi na wananchi kwa dhati km mwl?unaweza......??.....