shamu,
nimekwambia safari yangu ya kwanza uganda ilikuwa 1962. Kwa hiyo hayo unayoyasema mimi nimeyashuhudia. Lakini kusema kuwa uganda ilikuwa na uhuru zaidi ya tz hapo sitakukubali kabisa. Kwanza huwezi kuwa na uhuru kama mnabaguana kwa makabila. Waganda hawakutaka hata kusikia mambo ya lugha ya kiswahili. Wanatuita sisi walagh'ai, wezi, waswahili. Siku ya kwanza nazungumza kiswahili sokoni mjini kampala nilizungukkwa na kundi la mama wa kiganda wakisema "mtanganyika, mtanganyika. Nikamuuliza mwenyeji wangu aliyekuwa makerere wakati huo ndio akanisimulia ubaguzi wa waganda dhidi ya abanyamaanga ( ndio sisi hao, non ugandans) wale waliokubaliana na idi amin na sera zake ndio hao aliokuwa anawapa marupurupu ya friji na tv. Lakini, overall, lini friji na tv vikawa vipimo eti watu wanaishi maisha huru na bora? Waulize walibya.