(1) ni bora vita ya uganda alishinda kuliko vita ya ufisadi, mgao wa umeme iliyotushinda sasa na maandamano yasiyo na tija kila kukicha,(2) azimio la arusha lilishindwa kwa sababu nyerere hakutaka kudictate, alitaka watanzania waione nia thabiti katika maneno na matendo ya azimio hilo,ila tamaa za watanzania wachache na hasa wana ccm kipindi hicho hawakutaka usawa aliouwaza nyerere!(3) hakuna mzalendo kama nyerere, aliyeweza kufanya maamuzi magumu na kuyasimamia hata kama mabeberu wakiweka vikwazo.ndio maana aliona ni bora kuzalisha malighafi za kitanzania na zitumike tanzania kuliko kuruhusu soko holela!(4) ni km ilivyo tbc leo,haiwezi kuzungumzia mabaya ya rais,hata voice of amerika haiwezi kufanya hivyo!ni mtanzania gani wakati huo aliomba kuanzisha chombo cha habari akakataliwa hatuna ushahidi,hata hivyo nia ya ndani ya mwl na utashina utu wake vinamfanya watanzania tulio wengi tuendelee kumuona alikuwa kiongozi asiemithilika katika ulimwengu wa sasa!hauwezi ukaongea upuuzi kuhusu mwl mbele ya kadamnasi usipigwe mawe je bado leo hakuna uhuru wa kuongea,mbona bado watu tunamheshimu na kumuona kielelezo!hili sio kwa watu wa hali ya chini tu hata wasomi wa vyuo vikuu pindi wanapodai haki zao huimba ule wimbo maarufu wa " kama sio juhudi zako nyerere.....kama sio juhudi zako nyerere ....."hauwezi kupata urais wa nhi hii kutokana na kura za watanzania km utamponda mwl jukwaani!je bado hakuna uhuru mpaka leo?kubali ukweli mwl nyerere hafananishiki katika kizazi cha sasa!jaribu kufikiri km wewe ungekuwa rais leo ungekubali kufa maskini?kuishi kijumba km cha mwl?kusomesha wanao hapahapa bongo?kutenganisha famailia na uongozi?kujali nchi na wananchi kwa dhati km mwl?unaweza......??.....