KWELI Ushuzi na Kinyesi cha Ng'ombe huzalisha Methane inayosababisha ongezeko la joto duniani

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
a583e612-47c6-47f8-a9fb-5e08db3bfe55_shutterstock_180495239_9f5e45fa_750x400.jpg

Ingawa ni kama utani na inachekesha ila huwezi amini kuwa ng'ombe akijamba/kutoa ushuzi basi kile kitokacho huambatana na gesi ya methane ambayo huzalisha joto na moto/mwanga.

Wanaharakati mbalimbali wa mazingira wamekuwa wakidiscourage ufugaji/uzalishaji wa ng'ombe kwa wingi na kusema wazi kuwa ushuzi wa ng'ombe huleta mabadiliko ya hali ya hewa, kwa sababu ng'ombe hutoa methane, gesi chafu inayohusishwa na ongezeko la joto duniani.

Ng'ombe akiwa anajamba, ukiwasha njiti ya kiberiti moto unawaka kutokana na gesi ya methane.

Ningependa kujua ukweli wa hili jambo.
 
Tunachokijua
Methane ni gesi isiyo na rangi wala harufu. Hupatikana kwenye jamii ya mafuta ya taa na kisayansi huandikwa kama CH4. Pamoja na kupatikana kwa njia za asili chini ya ardhi, methane inaweza pia kutengenezwa kutokana na shughuli za kibinadamu.

Sekta ya ng'ombe wa nyama na maziwa huzalisha takriban 14.5% ya gesi chafu duniani, na zaidi ya nusu ya gesi hii ni methane. Gesi hii chafu yenye nguvu hunasa joto katika angahewa mara 25 kwa ufanisi zaidi kuliko gesi ya carbon dioxide.

Uzalishai wa gesi ya Methane
Ng'ombe hutoa methane kupitia usagaji chakula na kinyesi, tokeo la asili la jinsi wanyama hawa wanavyotumia na kusaga chakula.

Ng'ombe ni kundi la wanyama wanaojulikana kama wanyama wa kucheua (ruminants) kama vile twiga, kondoo au mbuzi. Tumbo la wanyama wanaocheua huundwa kwa vyumba vinne, cha kwanza kinaitwa rumen.

Hapa, bakteria na fungasi huvunja sukari na wanga kutoka kwa mimea. Mchakato huo huitwa uchachushaji wa ndani na hutoa asidi tete ya mafuta na gesi kama vile carbondioxide na methane. Kwa ufupi, kiasi kidogo cha methane huingia angani kila ng'ombe anapotoa choo au ushuzi.

1-Figure1-1.png

Uzalishaji wa gesi ya Methane unavyofanyika kwenye mwili wa Ng'ombe
Sekta tano kuu zinazohusika na 98% ya jumla ya uzalishaji wa methane kutoka kwa shughuli za binadamu ni:
  1. Kilimo
  2. Mafuta na gesi
  3. Uchimbaji wa makaa ya mawe
  4. Udhibiti wa taka ngumu
  5. Usimamizi wa maji machafu
Methane inaweza kusababisha ongezeko la Joto duniani?
Methane ina uwezo mara 80 wa kuongeza joto wa muda mfupi kuliko gesi ya carbon dixoide, na kuifanya kuwa mojawapo ya gesi chafu zenye nguvu zaidi.

Wanasayansi wanakadiria kwamba nusu ya ongezeko la joto litakalotokea katika miongo miwili ifuatayo litasababishwa na kuongezeka kwa viwango vya methane katika anga hewa.

Uwezo wake wa kunasa joto hufanya hata ongezeko dogo la viwango vya methane kuwa muhimu kwa mabadiliko ya hali ya hewa. Kadiri tunavyozalisha methane nyingi, ndivyo dunia huongezeka joto haraka. Kwa hivyo, kupunguza kiasi cha methane ni muhimu ikiwa tunataka kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kwa muda mfupi.

Madhara mengine ye gesi la Methane
Viwango vya juu vya methane hupunguza kiwango cha hewa ya oksijeni inayopumuliwa kwenye mapafu. Hii inaweza kusababisha mabadiliko ya kihisia (mihemko), kizunguzungu, uchovu mkubwa, changamoto za kuona, kupoteza kumbukumbu, kichefuchefu, kutapika, kuwasha usoni na maumivu ya kichwa.

Katika hali mbaya, kunaweza kuwa na ongezeko la idadi ya mapigo ya moyo, kupatwa na ganzi, na kupoteza fahamu.

Benki ya dunia inashauri serikali na wadau wote wa mazingira kuweka vifaa vinavyoweza kubaini sehemu zote zinazotoa au kuzalisha gesi hii pamoja na matumizi ya mbinu mbadala zitakazopunguza uzalishwaji wa gesi hii tishio kwa ustawi wa dunia.

Kwenye mazingira yaliyo na hewa ya kutosha ya oxygen, Methane inaweza kuungua na kuzalisha moto ambao husababisha uzalishwaji wa maji na hewa ya carbon dioxide. Aidha, inaweza pia kutumia kama chanzo cha nishati.
Tunawezaje kuikusanya hio methane Kutoka kwenye ushuzi??

Kwann kisiwepo kifaa kiwekwe kwenye puru Ili kuikusanya hio gas.
 
Ingawa ni kama utani na inachekesha ila huwezi amini kuwa ng'ombe akijamba/kutoa ushuzi basi kile kitokacho huambatana na gesi ya methane ambayo huzalisha joto na moto/mwanga.

Wanaharakati mbalimbali wa mazingira wamekuwa wakidiscourage ufugaji/uzalishaji wa ng'ombe kwa wingi na kusema wazi kuwa ushuzi wa ng'ombe huleta mabadiliko ya hali ya hewa, kwa sababu ng'ombe hutoa methane, gesi chafu inayohusishwa na ongezeko la joto duniani.

Ng'ombe akiwa anajamba, ukiwasha njiti ya kiberiti moto unawaka kutokana na gesi ya methane.

Ningependa kujua ukweli wa hili jambo.
wanaharakati wanaharakati zao nao

Hiyo kitu ni asilia ko kwa mtazamo wangu naliona ni sawa sawia::=

CH4(g)+2O2(g)→2H2O(l)+CO2(g)

Methane + Oxygen → Water + Carbon dioxide
2.

Afu kitu ina obey the law of conservation of mass ani mass::=80g kote kote

Wasitake kushindana na asili maana methane iki_burn in presenceof air(oxygen) mambo yanakuwa murua tena kwa carbondioxide na water molecules
 
Kwa hili tuna amini-au tuna fahamu-ni Bora kufanya utafiti tena na tena kujilidhisha-
 
wanaharakati wanaharakati zao nao

Hiyo kitu ni asilia ko kwa mtazamo wangu naliona ni sawa sawia::=

CH4(g)+2O2(g)→2H2O(l)+CO2(g)

Methane + Oxygen → Water + Carbon dioxide
2.

Afu kitu ina obey the law of conservation of mass ani mass::=80g kote kote

Wasitake kushindana na asili maana methane iki_burn in presenceof air(oxygen) mambo yanakuwa murua tena kwa carbondioxide na water molecules
Mkuu fomula zako zimenikumbusha mbali sana, enzi naipiga chemistry kikamilifu😂😂
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom