Hii ni simulizi ya dereva wa boda boda aliyenusurika kifo cha kuteketea na moto kwenye ajali ya Moro
Anasumulia kwamba asubuhi ile alipata abiria wa kumpeleka Nane nane... Walipofika eneo la ajali ndio kwanza ajali ilkuwa imetokea na hakuna aliyeshunghulika na majeruhi kwenye cabin ya gari... Hivyo yule abiria alimuomba dereva wa boda boda watoe msaada... Wakapanda kwenye cabin na kukuta abiria mmoja mwanamke na dereva ambao wote walikuwa wamevunjika miguu ila walikuwa hai bado
Walipojaribu kuwanasua wakakuta wamebanwa na mikanda (safety belts) hivyo yule abiria wa boda boda akamuomba bodaboda wakatafute kisu ili waje wakate ile mikanda wawatoe majeruhi... Boda boda akataka kugoma lakini yule abiria wake akamsihi wakatafute kisu wawasaidie wale majeruhi kwakuwa hata yeye boda boda hajui atakuja kusaidiwa na nani maishani...
Maneno yale yalimuingia bodaboda na kukubali huku wengine wakiendelea na harakati za kuchota mafuta yanayomwagika.... Basi ni wakati wanaiendea boda boda yao, ndipo moto ulipolipuka
Dereva wa bodaboda alinusurika ila bodaboda yake iliteketea palepale pamoja na yule abiria wake aliyetaka kutoa msaada
Maisha ni kitu gani? Maisha yamebeba siri gani? Kusudi la Mungu ninini?
Abiria mpita njia aliyekuta ajali na kutaka kutoa msaada anapoteza maisha kwenye harakati za kusaidia... Boda boda ambaye hakuwa tayari kutoa msaada pengine akuwaza muda atakaopoteza pale.. Ananusurika...!!!
Abiria yule angepita na zake pengine yasingemkuta yaliyomkuta... Utu wema wake ndio umekuwa kiama chake
Dereva wa Lori na abiria wake nao waliteketea ndani ya ile cabin... Pengine moto usingewaka wangenusurika..... Lakini anayeacha simanzi ni yule aliyejitoa kuwasaidia hawa majeruhi naye anaishia kuungua mpaka kufa.... Maisha ni kitu gani?