Ushuhuda wangu kuhusu pombe

Ushuhuda wangu kuhusu pombe

New york City

Senior Member
Joined
Jul 24, 2020
Posts
176
Reaction score
567
Habari zenyu wana JF naamini mko salama na moja kwa moja ntakwenda kwenye Mada.

Kinyume na madhara ambayo watu wameyapata na ambayo watu wanahubiri kila siku juu ya pombe, kwangu imekuwa tofauti kwani kila ninapokunywa pombe (light beers) huwa nafanya mambo ya Msingi kuliko ninapokuwa sijanywa.

Sinywi pombe kulewa sana huwa nakunywa bia mbili tatu hapo nikiingia kazini ntakuwa na LUGHA nzuri sana kwa wateja, attention to details, na pia nakuwa naweza ku-avoid minor errors.

Sio hayo tu lakini pia najikuta mtu mwenye huruma ya kusaidia watu na kuwasaidia wafanyakazi wenzangu pale wanapokwama na mambo mengine kama hayo.

Mwisho napenda kusema kuwa sina mpango wa kuacha pombe kwa sababu inanifanya kuwa productive, kufurahia familia, kuwa mstaarabu n.k

ONYO: Unywaji wa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako.
 
Eti light beer! we jamaa wewee,nshakusoma unaipenda sana hiyo kitu.Vipi lakini unafanya ibada au imeshakutawala mpaka umemsahau muumba wako...?
 
Kunywa kupita kiasi ndio kunywa namna gani? Hicho kiasi kinapimwa vipi? Hivi pombe zilitengenezwa ili nini?

Natamani kunywa pombe siku moja.. nashawishika sana kuonja pombe....
 
Kila kitu huanza polepole, kidogo kidogo ... subiri kikue/kukomaa ndipo utajua madhara yake/faida yake
 
Pombe imewaangamiza wengi, pombe imewafanya vilema watu wengi, pombe imeletea umaskini watu wengi, pombe imevunja ndoa za watu wengi, pombe imegombanisha marafiki wengi, pombe imesababisha wazazi wengi kushidwa kusomesha watoto wao, pombe imeua biashara za watu wengi, pombe imeletea magonjwa watu wengi,pombe imesababisha watu wengi kufukuzwa kazi, pombe imepoteza dira (mwelekeo) za watu wengi-wape maskini pombe wanywe wasahau shida zao.

Ushauri kama hujawahi kunywa pombe nakusihii usijaribu kuja kuacha ni ngumu sana sana,kama umekwisha anza kunywa pombe kunywa kwa kiasi (kistaarabu) Drink responsibly [emoji56]
 
S bnñhhb u
nina ndg yangu nae aliaanza hv hvi ikafika kpndi uchumi ukabana sana akipata pesa yoyote ni pombe ,hataki kuona pesa akipata chochotee anaenda kunywea pombee mpaka famili inayumba sana kiuchumi kisa bia
Sasa kama nikhbkvinywa ndio nakuwa productive hela itaongezeka au itapungua?
 
Back
Top Bottom