Ushuhuda wangu kuhusu pombe

Ushuhuda wangu kuhusu pombe

Habari zenyu wana JF naamini mko salama na moja kwa moja ntakwenda kwenye Mada.

Kinyume na madhara ambayo watu wameyapata na ambayo watu wanahubiri kila siku juu ya pombe, kwangu imekuwa tofauti kwani kila ninapokunywa pombe (light beers) huwa nafanya mambo ya Msingi kuliko ninapokuwa sijanywa.

Sinywi pombe kulewa sana huwa nakunywa bia mbili tatu hapo nikiingia kazini ntakuwa na LUGHA nzuri sana kwa wateja, Attention to details, na pia nakuwa naweza ku-avoid Minor errors.

Sio hayo tu lakini pia najikuta mtu mwenye huruma ya kusaidia watu na kuwasaidia wafanyakazi wenzangu pale wanapokwama na mambo mengine kama hayo.

Mwisho napenda kusema kuwa sina mpango wa kuacha pombe kwa sababu inanifanya kuwa productive, kufurahia familia, kuwa mstaarabu n.k

ONYO: Unywaji wa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako.
Subiri usikie wakisema bila "pombe hawezi kufanya kazi".

Na kweli huwezi kufanya kazi vizuri kwa sababu umeshazoea.

Katika vitu duniani sio vya kujaribu ni pombe, adhari zake ni kubwa mno kuliko maelezo.
 
Subiri usikie wakisema bila "pombe hawezi kufanya kazi".

Na kweli huwezi kufanya kazi vizuri kwa sababu umeshazoea.

Katika vitu duniani sio vya kujaribu ni pombe, adhari zake ni kubwa mno kuliko maelezo.
Ahsante Mtumishi hata soda zina madhara dawa ni kuheshimu kiasi, nimesema nakunywa kiasi.
 
Kama kipato kinaruhusu, bia mbili au tatu ni sehemu ya chakula, bia ni ngano.
 
..sema unakunya kidogo kukuongezea ujasiri/confidence ya kukutana na wateja wako
 
29 Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu?

30 Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.

31 Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu; Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu;

32 Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira.

33 Macho yako yataona mambo mageni; Na moyo wako utatoa yaliyopotoka.

34 Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.

35 Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.

Achana na pombe mkuu haya unayoyasema sasa kuwa ni faida baada hutayaona ila ubatili tu huku ukiwa umeshalewa
 
Kunywa kupita kiasi ndio kunywa namna gani? Hicho kiasi kinapimwa vipi? Hivi pombe zilitengenezwa ili nini?

Natamani kunywa pombe siku moja.. nashawishika sana kuonja pombe....
kuna aliyekuzuia kunywa?maana kwenye katiba au biblia hujazuiwa..
 
Hata mimi kipindi naanza kuvuta bangi nilikua naenda kanisani nafanya usafi nje na ndani nilikua mwema hivyohivyo subiri iko siku utaona madhara yake
 
"33 Macho yako yataona mambo mageni; Na moyo wako utatoa yaliyopotoka.

34 Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.

35 Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena"


Hii mistari yote inazungumzia Ulevi mimi sio mlevi mkuu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mimi kipindi naanza kuvuta bangi nilikua naenda kanisani nafanya usafi nje na ndani nilikua mwema hivyohivyo subiri iko siku utaona madhara yake

Enhe ikakufanya nini baadae bange mzee? 😅 ebu tuambie....




Let's meet at the top, cheers 🥂
 
Nizidi kukumotiveti
255653429097_status_0f792709959645ff98577c2494a0c40c.jpg
 
Back
Top Bottom