Habari zenyu wana JF naamini mko salama na moja kwa moja ntakwenda kwenye Mada.
Kinyume na madhara ambayo watu wameyapata na ambayo watu wanahubiri kila siku juu ya pombe, kwangu imekuwa tofauti kwani kila ninapokunywa pombe (light beers) huwa nafanya mambo ya Msingi kuliko ninapokuwa sijanywa.
Sinywi pombe kulewa sana huwa nakunywa bia mbili tatu hapo nikiingia kazini ntakuwa na LUGHA nzuri sana kwa wateja, attention to details, na pia nakuwa naweza ku-avoid minor errors.
Sio hayo tu lakini pia najikuta mtu mwenye huruma ya kusaidia watu na kuwasaidia wafanyakazi wenzangu pale wanapokwama na mambo mengine kama hayo.
Mwisho napenda kusema kuwa sina mpango wa kuacha pombe kwa sababu inanifanya kuwa productive, kufurahia familia, kuwa mstaarabu n.k
ONYO: Unywaji wa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako.