Tarakilishi
JF-Expert Member
- May 19, 2013
- 2,180
- 2,454
I love this post very muchAchana nayo kama huna abc za psychology! ukiiendekeza unaweza jiua! Unaweza kujiathiri bure kisaikolojia kabla ya kuwa karibu na jamii basi ukawa una antisocial behaviour, pia ukajaa kutwaa zigo la ukichaa, au uzezeta, au umasikini, au faraka na bipolar na mengineyo
Ushauri wangu, jifunze kumshukuru muumba na kumsifia kwa ukuu, ujuzi na utaalamu wake juu ya viumbe vyake na utukufu wake...
Muombe akujalie elimu yenye manufaa, na umuombe akusutiri na auepushie maradhi ya kiakili.. Muombe aifanye akili na moyo wako kustahmili kila jambo kwa kuwa na subira na uvumilivu na pia uwe na good social skills katika interactions etc.
Neema ya akili, ni moja kati ya neema kubwa mno, hii neema haipaswi kufanyiwa majaribu ambayo side effects zake hazicha chambuliwa effective...
Wito; Kwa wale ma psycho programer wa akili kuanzia wazazi, waalimu na jamii na wahadhiri..kuna haja ya ku builts hizi ego kwa manufaa ya jamii, kwa mafaa ya mjengwa, kwa manufaa ya mazingira na kwa kuzingatia stratergy maalumu..ambayo mjengwa na mjengaji watasaidiana pindi litokeapo tatizo.
Alamsiki
Its bullshit you're just wasting your time, omba Mungu, ingia chumbani kwako piga magoti, mweleze Mwenyezi shida yako atakupa unachotaka... Meditation!?? Bullshit
Kweli hajitambu isikute hata jinsia yake haitambui pia.Una hakika gani kuwa hiyo unayofanya ni meditation labda unakosea je???
Una mwalimu aliekuongoza siku za mwanzoni au unafanya tu mwenyewe??
Ulitegemea kupata faida gani??? (Pesa au??) maana kulingana na swali lako ni kama ulitegemea kupata kitu flani mara tu ilipoanzia kufanya taamuli.
Pia faida kubwa ni kujitambua sasa we kulingana na huu uzi wako ni kwamba bado hujajitambua.... Unahitaji kujitambua zaidi mkuu ili niweze kupata faida za taamuli kimwili na kiroho pia.
Nimekupenda bure kwa maelezo sawia, big up!Lengo la Meditation ni simple. Lakini faida zake ni nyingi. Faida zake ni kutoka katika lengo moja. Na kila faida inaweza kuleta faida nyingine. Kuna faida kuu au lengo kuu ambalo matokeo mengine hutokea kama matawi. Ni kama mti na matawi. Lengo ni kuweza kutoa mshikilio uliopo akilini ambao kwa kawaida huonekani kwani tumezoea hali ya kushikilia akili zetu na hatuifahamu nature ya akili yetu.
Sio lengo ni kupata vipaji, sio kuwa na utajiri, sio kupata nguvu za ajabu, au jinsi wengi wanavyofikiri. Kuipata furaha ya kweli, kujitambua, kudhibiti hisia, mazoea, tamaa, hasira, chuki na ubinafsi, na kuweza kuiongoza akili yako. Hayo ni matokeo tu na faida za meditation zinazotoka katika faida kuu. Na faida hizo zinaweza kuzaa nyingine zaidi kama vile kuwa na tabia njema, kuacha mazoea mabaya, kujifahamu na kufahamu akili na ufahamu wa watu. Na faida hizo zinaweza kuleta faida zaidi kama kuwa na maisha mazuri kwani unaweza kujithibiti na unaishi vyema kwa akili na busara, unaweza kushirikiana na watu, unaweza kujidhibiti na kujitawala na kuwa mtu wa haki na msimamo. Pia unakuwa mwepesi kuisikia nafsi / intuition.
Kinachowarudisha nyuma wengi ni kuwa hawapitii kwanza maelezo ya mwanzo ya kuyafahamu kama vile akili ni nini, ina nini, ufahamu ni nini, una nini na nini. Akili ipoje na Ubongo? Ubongo na milango ya ufahamu vimeungana vipi na ufahamu? Chanzo cha mawazo ni nini? Ufahamu upoje na akili? Akili na mwili vimeunganika wapi? Wazo ni nini? Kulala ni nini? Nini kitatokea usipolala? Ndoto ni nini? Baada ya kupitia introduction kidogo ya kufahamu sayansi hiyo ndipo utatambua meditation ni nini na kwanini kuna meditation. Wengi huanza kusomea meditation bila kufahamu maelezo ya mwanzo katika kujifahamu na kufahamu ufahamu na akili ni nini.
Nenda YouTube ka search video za meditation for beginners zitakuja hapo kisha download.mimi nina mwezi sasa nimeshindwa kufanya meditation l, sina mwalinu na tatizo kuingiliana kwa mawazo wakati ninapotaka kufanya meditation
Its bullshit you're just wasting your time, omba Mungu, ingia chumbani kwako piga magoti, mweleze Mwenyezi shida yako atakupa unachotaka... Meditation!?? Bullshit