Foxhound
JF-Expert Member
- Dec 15, 2013
- 28,739
- 76,374
Amini unavyoamini kama huamini ni juu yako kutokuamini.Chai na ugali..kwa pamoja, shibe YAKE hunyanyuki bila winch!!!
ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹ [emoji377]

SEHEMU YA KWANZA.
Mimi nafanya shughuli zangu city centre.. Natumia usafiri wa pikipiki kuendesha shughuli zangu mjini ili kufika sehemu kwa wakati.
Kuna order iliwahi kutolewa na mkuu wa Mkoa Mh Paul Makonda kutoingia mjini bila kibali. Ili kutii agizo hilo huwa nakata kibali kila baada ya miezi 6 ili niweze kuendelea na shughuli zangu bila bughudha.
Picha linaanza mwezi september kwa kukamatwa nikiwa nimesimama kwenye mataa ya mnazi mmoja nikisubiri taa ziruhusu magari ,mara paap nadandiwa na mtu aliyevalia kiraia na kuchomoa ufunguo ghfla. Namuuliza kulikoni? Najibiwa leta pikipiki pembeni. Baada ya kusogea pembeni naambia achia pikipiki nauliza kwa nini? Naulizwa una bei gani nikuachie?
Duuu nikajua tapeli huyu,nikamjibu nikupe pesa kwa kosa gani? Nikaambiwa sina Leseni, nikaonesha leseni. Baada ya dakika kadhaa za mabishano anaingia mwingine ananiamuru niachie pikipiki, tukaanza kuvutana wakanizidi nguvu. Pikipiki ikachukuliwa nikaambiwa nikae nyuma. Kweli, kumbe ni askari akanipeleka hadi central , kufika tu yule aliyenikamata akasema "afandeeee huyu kosa lake mwendo kasiiii" shabashiiiii nataka kuongea nikambiwa kaa kimya unajifanya jeuri, kaa chini nyosha miguuu, duuuu nikatii sheria bila shuruti. Walikuepowengine wengiwaliokaa chini wanachukuliwa maelezo.
Baada ya muda zamu yangu ikafika nikaanza kuhojiwa. Nikaulizwa kosa nikasema sina kosa. Askari akaniambia usinipotezee muda mimi sijakukamata. Akaniambia chagua kosa niandike Mwendokasi au wrong parking, duuuh nimebisha pale mwisho a picha nikaandikiwa Wrong parking.
Baadae tukapekuliwatuakawekwa ndani wote. Tulikuwa kama 20. Tukiwa ndani tukawa tunabadilishana mawazo na madereva wenzangu. Wengi ni Bodaboda. Nikaambiwa hapa kesho asubuhi unatakiwa uandae wadhamini 2waje na barua za serikali za mitaa. Kweli kesho yake akaanza kutoka mmoja baada ya mwingine. Zamu yangu ilipofika nilidhaminiwa na mtu mmoja. Nikaachiwa kama saa 6 mchana. Nikaambiwa kesho saa 4(siku iliyofuata) nije na LESENI, KADI YA PIKIPIKI, BIMA, SUMATRANA RISITI.
Kesho nikaenda navyo vyote. Tumekaa pale asubuhi hadi mchana hakuna kinachoendelea ila naona wenzangu(wazoefu wa kukamatwa mjini) wanachukua pikipiki wanaondoka. Ikabidi na mimi nijiongeze nikamuuliza aliyetoka na pikipiki,utaratibu wa pikipiki ukoje?mbona nimeshakaguliwa lakini sioni nikiachiwa? Akaniambia Bro hapa huwa hawataki maneno wanataka pesa au uende mahakamani ukajitetee? Duuhh kusikia mahakamani nikapagawa.
Nikamuuliza wanataka kiasi gani? Nikaambiwa laki na nusu (150,000/=). Baada ya kukaa muda ikabidi na mimi niende ofisini pale kwa Afande Beka kwenye ofisi ya karibu na mwembe ili nilipe 150,000/=. sikkufanikiwa kumuona afande Beka. Nikapewa namba nimpigie askari anisaidie kuitoa pikipiki. Akaniambia bila laki na nusu pikipiki huitoi, nikamwambia laki na nusu ninayo. Akaniambia nisubiri baada ya nusu saa kwa sababu yupo mbali.
Baada ya nusu saa akanipigia simu nipeleke pesa. Nikaenda nikampa keshi 150000. Nikapelekwa kwa Afande Beka nikaaandikiwa kimemo, pikipiki nikapewa. SIUKUPEWA RISITI. NILIPOULIZA RISITI NIKAULIZWA KWANI PIKIPIKI YAKO HUJAPATA? NIKAISHIWA POZI IKABIDI NIWE MPOLE.
SEHEMU YA PILI.
Mwezi November. Picha linaanzia mataa ya kamata. Nikiwa nimesimama ktk mataa mara paap funguo zimechomlewa. Kama kawaida. Tukaenda kuwekwa kwenye karandinga karibu na roundabaout ya kuelekea sentro na mbagala. Ilipofika jioni aliletwa jamaa mmoja anashushiwa kipigo cha hatari. Alishushia sitiki za kufamtu. Kumbe yule jamaaalikua mwanajeshi ila yeye alikuwa abiria alivyoona wamerukia ufungua wa bodaboda aliyekuwa amemubeba alihisi kutaka kusababishiwa ajari, ikabidi awape adabu kidogo asikari duuh baada ya hapo walikusanyika kama wote walimshushia kipigo cha mbwa mwizi pamoja na kuwaonesha kitambulisho kama afisa wa jeshi hawakumuelewa, walimpa kipigo hadi akawa anatoa chozi kwa uchungu. Siku hiyo kama kawaida tukapelekwa central, usiku huo zilipigwa simu nyingi sana zikilenga kusaidia huyo mjeshi bila mafanikio. Siku hiyo tulikaa pale tukachuliwa maelezo hadi usiku wa saa 6. Baadae tulipelekwa mahabusu wote ,tukapekuliwa tukaingizwa chini lakini yule mjeshi alibaki kaunta tulikuja ambiwa kesho yake kuwa aliachiwa.
Kama kawaida utaratibu wa kutoka ulikuwa uleule. Nililipa 150,000/=BILA RISITI, BILA KUANDIKIWA MAKOSA MATANO ILI IENDANE NA PESA ILIYOLIPWA YA MAKOSA 5, ILA SIKU HIYO NILIANDIKIWA KOSA LA KUPITA MWENDO KASI WAKATI NIMEKAMATIWA MATAA YA KAMATA NIKIWA NATOKA POSTA.
SEHEMU YA TATU.
Baada ya pale baadhi ya madereva bodaboda walivyoona nakamatwa kizembe walinishauri nisiwe nasimama kwenye mataa. Wao huwa hawasimami kwe mataa kwa kuogopa kudandiwa na askari bila sababu za msingi. Nikaona hii imekaa poa sana. Na mimi sasa nikawa siheshimu mataa, nikiona upenyo tu napenya. Laikini hili halijanisaidia kwa sababu sasa hivi hawa askari wamejaa kila mtaa. Naambiwa wanatumia shirikishi na baadhi ya madereva bodaboda kukamata wenzao. Unaweza ukawa unatembea mara ghafla inabinywa clutch. Kwa style hii ya hovyo nimekamatwa mara 2 na mara zote hizi nilianguka chini kwa sababu ya kung'ang'aniwa clutch.
Kuna mbinu nyingine wanakublock na bajaji au na pikipiki kiasi kwamba wanaweza kukusababishia ajari. Hii mbinu nadhani imeanza baada ya kuona hatusimami tena kwenye mataa.
Picha linaanzia february. Nimekamatwa mara 5 toka february hadi jana. Kama kawaida mkamataji anaweza kukuliza kwanza una bei gani, mkimalizana anakuachia. Mara nyingi ukiwa na elfu 50, 30, 20 ya papo kwa papo unaachiwa. Kama huna pesa ya papo kwa papo ndo unafikishwa kwa pilato. Kwa afande Beka.
Angalau sasa hivi wamepunguza bei. Pale sasa hivi unaambiwa lipia makosa mawili yaani 60,000/=. Bila hiyo pesa huachiwi na chombo kinabaki polisi. NAWAONEA HURUMA BODABODA WANAOCHUKULIWA PESA ZAO BILA HURUMA KUWA WENGINE WANAENDESHA FAMILIA ZAO KWA KAZI YA BODABODA. Bodaboda na waendesha pikipiki wengine hapo mjini huo ndo mtindo wa kisasa. HII ADHA MADEREVA PIKIPIKI TUNAIPATA KWA SABABU YA TAMKO LA MH MKUU WA MKOA PAUL MAKONDA.Unaweza kuwa na Kila kitu lakini ukifika pale unapigwa biti na maasikari pale utadhani umeua. Hupewi pikipiki ukaendelee na shughuli bila kulipia faini. Husikilizwi hata kidogo. Hii ni tofauti na gari unaandikiwa bill hata kama huna pesa kwa wakati huo unalipia baadae. HII HALI YA VITISHO, KUWEKWA NDANI , NA KULAZIMISHWA KULIPIA FAINI YA PAPO KWA PAPO NDO INAONGEZA RUSHWA NA HATUPEWI RISITI. PESA ZOTE ZINAISHIA PALE KWA AFANDE BAKARI BADALA YA KULIPA KWA CONTROL NAMBA AU KWA MHASIBU.
BODABODA NA MADEREVA WENGINE WA PIKIPIKI HASA WA DAR-ES-SALAAM NAO WANA FAMILIA. HUU UONEVU WA KUPIGWA FAINI KUBWAKUBWA UNAWAONGEZEA STRESS ZA MAISHA. MUDA UTAONGEA.
Safi Sana bro umemsaidia Sana bodaAmini unavyoamini kama huamini ni juu yako kutokuamini.
ᴮᵉʷᵃʳᵉ ᵒᶠ ᵗʰᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ⁻ ¹⁹ [emoji377]
Beka sio peke yake inaonekana huo ni mtandaoHuyo afande Beka dawa yake inachemka hawezi kula pesa za watu kirahisi hivyo!!
Kama anapenda pesa za bure aje huku Mombasa..!!
Nakumbuka alivyonifikisha alitaka kunirudishia 5000 yangu ila nilimwambia asijali maana maisha ndivyo yalivyo. [emoji120][emoji120][emoji120]Safi Sana bro umemsaidia Sana boda
Halafu bodaboda mnaunga juhudi wanasiasa wkt wa uchaguzi kwa mafuta ya buku 5!!
Makonda huyo huyo akiwaita mnajaza mibendela ya chama kama vibaka!
Sent using Jamii Forums mobile app
Huu ni mtandao. mkuu wa mkoa kama mwanzilishi anaujua. wanapiga pesa sana. kuna pikipiki zaidi ya 200 za watu walioshindwa kulipa hizo pesa. Nimeambiwa kuna askari hadi wanaenda kuroga ili wapangwe kitengo cha pikipiki mpunga njenje za papo kwa papo field na za mgao ofisini.Huyo afande Beka dawa yake inachemka hawezi kula pesa za watu kirahisi hivyo!!
Kama anapenda pesa za bure aje huku Mombasa..!!
kazinja..
Una bahati sana kupewa onyo tu wenzio ni pesa kwenda mbele. Hakika jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kinanukaMimi nililala central hapo mwaka jana, nilikamatwa mataa ya kamata na askari kavaa kiraia akanivuta pembeni, akaniuliza una kila kibali nikamwambia ndio akaichukua akanipeleka kwa inspetor. Inspector akaniuliza pikipiki yako ina tatizo gani? Nkamwambi ina kila kibali fanya ukague, hilo ndo likawa kosa langu. Asbh nikapewa kosa la wrong parking, kutotii amri ya askari na jingine siukumbuki IL nilipewa barua ya onyo kwa makosa yangu nliyopewa. Ila nililala had kesho yake mchana. Kule selo ni pasafi sana ila nyampala alinipiga banzi moja matatu la mgongo siwez lisahau
Sent using Jamii Forums mobile app
Mambosasa ana mgao?Enzi za Kangi kila mwendesha pikipiki alipumua. Angalau hata ukikamatwa uliandikiwa kosa moja japokuwa napo risiti hatukupewa. kuna jamaa kanieleza huu ni mradi wa wakubwa wa kupiga pesa.
Mafuta mliyokua mnawekewa ndio mnayalipa kwa mishindo sasa. Msiuze tena haki zenu kwa kuwekewa mafutaUkweli hii inauma sana mi nilikamatwa kama siku 10 zilizo pita kwenye mataa ya kamata nikatoa30000 nikaachiwa yan nashindwa kuelewa huu utapeli hawa viongozi hawauwoni au wote wanagawana haya mapato nchii hii huu uonevu utaisha lini mi nafikir hata aIGP anahusika na kama hausiki hasikiii kilio cha sisi waendesha Pkpk
Tushasikia wanatoa matamko ambayo hayatekelezeki tunaelekea uchaguzi sasa cjui mtakuja na jambo gani jipya mtaanza kujipendekeza tena na kuwawekea mafuta madereva wa boda boda
Mnakera sana yani waendesha Pkpk wanakua kama sio RAIA wa Tanzania yan imekua kabla ya kuondoka nyumban unawaza cjui kama nitafika salama
Serekali ya jamhuri mko wapi rais magufuli husikii kilio cha waendesha Pkpk inauma.
Sent using Jamii Forums mobile app
Yupo bingwa wa kubambika kesi anakusikia. Nashauri hawa polisi tuwataje kwa namba zao ili watambulike kabisaPolisi Tanzania ni kati ya Jeshi ambalo sina Imani nalo hata kidogo, mwezi wa 11 walikula 150,000 yangu kwa kosa la kubambika.
Ila najua hao waliogawana hiyo pesa yangu hawatakaa wapate amani ya moyo na matendo hayo.
Kama kuna polisi yumo humu na amesoma hizi comments mjue mnafanya dhuruma ambayo laana yake haitakaa iishie kwenu, itakula hadi watoto na wajukuu wenu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo hiyo ambayo maafisa wao wamekamatwa juzi huko tanga kwa kudai rushwa kwa mtu aliyekua na tuhuma za rushwaTAKUKURU IPI?
Askari wengi wa majeshi yetu hawana nidhamu kwenye utendaji wao. Kuna mahali inatakiwa ushawishi na elimu wao ni nguvu tu hadi nashindwa kuelewa kulinda raiya na mali zao maana yake ni nini.[emoji28][emoji28][emoji28], kuna siku nimekwenda Segerea magereza kumsalimia mahabusu, kuna askari magereza mmoja akawa hatumii ustaarabu anasukuma watu watoke mle ndani kwa madai muda umekwisha waingie wengine, akawa kama ananisukuma nitoke, nilimuuliza kwa ukali huku nimemkazia macho kwanini ananisukuma, kunambia tu hakutoshi?....Nikamsindikiza na msonyo juu...Alinicheck kwa mihasira yake, nafikiri alikuwa anajiuliza nimepata wapi ujasiri ule.Mie huyo nikaondoka zangu.
Nawe kafanye hilo jaribio lako utupatie mrejesho.
Duuh! hakunaga askari wa hivi, wewe ni raia tu.Dua la kuku halimpati mwewe!
Tunakula hela zenu na laana haitupati.
Tumemuua Mwangosi, muuza magazeti huko Morog. Akwilina na wengi wengineo ndiyo kwanza tunanenepa, we subiri kama tutalaanika.
Sent using Jamii Forums mobile app
Bodaboda wanaendesha maisha yao na familia zao kwa pikipiki polisi wanapozing'ang'ania badala ya kuwaandikia faini inakuwa mtihani kwaoNdugu sasa wewe unawahurumia tu boda boda badala na wewe ujihurumie maana kila siku unasema unakamatwa
Sent using Jamii Forums mobile app
Dar kuna vituko,yani kutoa pikipiki 150,000 kweli watu wanaonewa sanaSEHEMU YA KWANZA.