H r n
JF-Expert Member
- Oct 3, 2019
- 1,100
- 2,078
Wakuu mpo good
Leo asubuhi nimeamka nikiwa nimechelewa kwenda kazini. Nikatoka nje kwa haraka, nikakutana na boda mmoja nikamsimamisha.
Nikamuuliza, “Mwanangu, nataka kwenda sehemu fulani, mpaka huko ni shingapi?” Akaniambia bei yake, nikakubali. Tukapanda, safari ikaanza fresh kabisa. 😅
Tukaingia main road, ndipo nikagundua kwamba pikipiki haina side mirror kabisa!
Sasa huyu jamaa kila akitaka kujua kinachotokea nyuma, anageuza shingo mzima kuangalia. 😂
Na kwa kuwa nilikuwa nimekaa nyuma yake, kila mara alikuwa anafanya kama anataka kuhakikisha nyuma kuna nini.
Tatizo kubwa lilikuwa pale tulipoanza kuingia kwenye barabara za vichochoro na kupita-pita huku na kule.
Mara anageuka kuangalia nyuma, mbele kuna bodaboda mwingine; mara gari linakuja; mara tunatoka kwenye njia ndogo tunaingia main road.
Kuna muda tukawa tunakaribia kugongana na bodaboda, muda mwingine tunakaribia kukutana na gari. Mimi nilikuwa nimekaa nyuma nikajiuliza:
“Hivi leo nimechelewa kazini au nimeamua kwenda kujitoa muhanga?” 😂
Cha kushangaza ni kwamba dereva mwenyewe anaonekana kawaida kabisa, anaendesha kama hakuna tatizo. Mimi ndio nilikuwa naona kila sekunde kama safari inaweza kugeuka kuwa tukio la kusimuliwa.
Hapo nikagundua kitu kimoja: Side mirror kwenye pikipiki sio mapambo. Ni kitu muhimu sana kwa dereva kujua kinachoendelea nyuma bila kulazimika kugeuza shingo kila baada ya sekunde chache.
Mwisho wa safari nilifika salama, lakini niliposhuka nilijisikia kama nimetoka kwenye mtihani wa maisha. 😂
Swali kwa waendesha bodaboda: Pikipiki isiyo na side mirror, mnaweza kweli kuendesha kwa usalama kwenye main road? Au dereva anapaswa kuwa anageuka-geuka hivi kuangalia nyuma?