USHUHUDA: Namna ambavyo Mungu amekuwa akijibu maombi yangu

Sawa mkuu hata mimi naomba Mungu siku zote sijapata majibu kwa matatizo lukuki niliyokuwa nayo.
Huoni itakuwa vizuri akifunguka zaidi, mbona hamtaki na sisi tufanikiwe8 kama yeye inakuwaje hapo

Halafu badala ya kujibu hoja yangu amepiga "like". Yaani amejificha nyuma ya Like. Mungu huyo huyo anamwona anavyotupiga chenga hapa.
Mkuu ondoa shaka kabisa. Nimejifunza kwa muda mrefu kuwa Neema ya Mungu haitegemei unaabudu kanisa gani. Kitu kikubwa ni kuwa na IMANI na kuwa mtiifu kwake. Kuwa mtiifu kwa Mungu siyo kitu kinachotokea kama hisani, ila huja automatic kulingana na matendo yako na bidii unayoweka kuwa karibu na Mungu. Kuwa mtiifu kwa Mungu ni hali ya mtu kuanza kuchukia au kuwa mzito wa kutenda mabaya, na kuwa mwepesi au kuwa na hamu ya kutenda mambo mema. Ukifikia hatua hiyo basi ni dalili moja wapo ya kuanza kumpenda Mungu.

Mimi siyo mkamilifu sana na wala siyo mcha Mungu kama ambavyo nadhani inatakiwa kuwa kama ilivyoandikwa kwenye vitabu vya Mungu. Na wala sina mali, utoshelevu wa vitu au niliye na kila kitu kizuri kama ambavyo binadamu angetamani kuwa navyo. Ila itoshe kusema nimeona NEEMA na NGUVU za Mungu zikitenda kazi.

Kingine ni kuwa, haya madhehebu yasikutishe sana. Naona ni njia tu ya mtu kumtafuta Mungu. Je, unafahamu historia ya Makanisa mengi Duniani? Mengi yalianza kutokana na sababu moja ama nyingine. Sifahamu kama ndivyo Mungu alipanga iwe, ila nadhani Mungu ama YESU angependa watu wawe wamoja katika kanisa moja.

Ukitaka kufahamu historia ya makanisa Ulimwenguni soma historia kwa kurejea kisa cha Papa Bonafasi III na kanisa Katoliki mwaka wa B.K. 606, rejea kisa cha mfalme wa Rumi Konstatino mwaka wa B.K 313 na kanisa la Orthodox la Mashariki, rejea pia kisa kati ya Martn Luther na Papa Leo X mwaka 1521 na kuanzishwa kwa dhehebu la Kilutheri, vilevile rejea kisa cha Mfalme Henry wa VIII wa Uingereza na Anglikana. Kisa cha John Huss na dhehebu la Moraviani, historia ya madhehebu ya Assemblies of God kuanzia mwaka 1914 huko Marekani. Kisa kuanzia kwa Mhubiri aitwaye William Miller, Samuel Sheffield Snow, George Storrs, F.H Berick, Jonathan Cummings, kisha akina Ellen G White na mmewe James White, kisha Joseph Bates,Hiram Edson, Fredrick Wheeler na S.W Rhodes na dhehebu la Wasabato (Seventh- Day Adventists) na madhehebu mengine mengi siwezi kuandika historia yake yote hapa.

Hivyo point yangu ya msingi siyo kudhihaki madhehebu ya watu wala kusema dhehebu lipi ni bora, bali ni kuendelea kusisitiza kuwa mwaminifu kwa Mungu. Sisi Wakristo ni kumwamini YESU kuwa ndiye njia ya ukombozi wetu WANADAMU, kisha Mungu atatenda kadri ya Mapenzi yake. Wapi unasali na namna ipi, kwa maoni yangu si suala la mkazo sana, wewe endelea kujinyenyekesha kwake siku zote.

Binafsi huyafananisha maisha na safari ya mtu atembeaye kwa miguu mwendo mrefu. Ambapo kuna wakati hufika anatakiwa kupanda kilima nakuchoka sana, anapotaka kutaka tamaa kisha anaona mwisho wa kilima umefika na kuanza mteremko kisha tambarare. Lakini pia kwakuwa ni safarai ya mwendo mrefu, hurejea tena kukutana na kilima mbele yake na kisha mteremko na tambarare tena. Hivyohivyo mpaka anafika mwisho wa safari yake. Muhimu ni kuwa hakuishia njiani bali alifika mwisho ambako alipata pumziko la mwisho kabisa (baada ya kifo).Wakati wa mteremko na tambarare ni pale unapokuwa na maisha ya raha na furaha sana, wakati wa kupanda kilima ni ule wakati unapokutana na majaribu ya hapa na pale katika maisha. Hakuna awezaye kuishi maisha ya furaha siku zote za uhai wake bila kukutana na changamoto. Bali kuna nyakati zote za furaha na changamoto katika hii Dunia.
 
Mkuu ondoa shaka kabisa. Nimejifunza kwa muda mrefu kuwa Neema ya Mungu haitegemei unaabudu kanisa gani. Kitu kikubwa ni kuwa na IMANI na kuwa mtiifu kwake. Kuwa mtiifu kwa Mungu siyo kitu kinachotokea kama hisani, ila huja automatic kulingana na matendo yako na bidii unayoweka kuwa karibu na Mungu. Kuwa mtiifu kwa Mungu ni hali ya mtu kuanza kuchukia au kuwa mzito wa kutenda mabaya, na kuwa mwepesi au kuwa na hamu ya kutenda mambo mema. Ukifikia hatua hiyo basi ni dalili moja wapo ya kuanza kumpenda Mungu.

Mimi siyo mkamilifu sana na wala siyo mcha Mungu kama ambavyo nadhani inatakiwa kuwa kama ilivyoandikwa kwenye vitabu vya Mungu. Na wala sina mali, utoshelevu wa vitu au niliye na kila kitu kizuri kama ambavyo binadamu angetamani kuwa navyo. Ila itoshe kusema nimeona NEEMA na NGUVU za Mungu zikitenda kazi.

Kingine ni kuwa, haya madhehebu yasikutishe sana. Naona ni njia tu ya mtu kumtafuta Mungu. Je, unafahamu historia ya Makanisa mengi Duniani? Mengi yalianza kutokana na sababu moja ama nyingine. Sifahamu kama ndivyo Mungu alipanga iwe, ila nadhani Mungu ama YESU angependa watu wawe wamoja katika kanisa moja.

Ukitaka kufahamu historia ya makanisa Ulimwenguni soma historia kwa kurejea kisa cha Papa Bonafasi III na Ukatoliki mwaka wa B.K. 606, rejea kisa cha mfalme wa Rumi Konstatino mwaka wa B.K 313 na kanisa la Orthodox la Mashariki, rejea pia kisa kati ya Martn Luther na Papa Leo X mwaka 1521 na kuanzishwa kwa dhehebu la Kilutheri, vilevile rejea kisa cha Mfalme Henry wa VIII wa Uingereza na Anglikana, na madhehebu mengine mengi siwezi kuandika historia yake yote hapa.

Hivyo point yangu ya msingi ni kuendelea kuwa mwaminifu kwa Mungu. Kisha yeye atatenda kadri ya Mapenzi yake. Wapi unasali na namna ipi, kwa maoni yangu si suala la mkazo sana, wewe endelea kujinyenyekesha kwake siku zote. Wakati wa mteremko na wakati wa kupanda kilima.
Asante sana Mkuu kwa kuliweka hilo sawa nadhani watu wengi wamenufaika na majibu haya.

Cha msingi kila mtu aache roho mbaya na dhambi kwa ujumla tumche Mungu.
 
Wewe mtoa mada nadhani u were just lucky, kuomba Mungu na kupata majibu si rahisi kihivyo, ingekuwa Mungu anajibu maombi kirahis hivyo, basi kusingekua na maskini duniani, na duniani kusingekuepo na wanaokufa njaa, watu wasingeenda Kwa waganga wa kienyeji, kama Mungu anajibu maombi kirahisi, wale waliomuomba Mungu na hawajajibiwa, waje kutoa ushuhuda wao hapa Heaven Seeker
 
Update maombi yako .naona ya mwaka juzi uko...leta ya ivi karbuni

Time is a drug. Too much of it kills you
 
Ushuhuda mzuri sana lakini kila mtu anaomba kwa Mungu labda ungejaribu kueleza maombi yako unayafanya kwa namna gani ili wale waombao lakini hawafanikiwi wajue wanakosea wapi??
 
Aisee inashangaza sana unakosa hofu ya Mungu kabisa hadi una comment hivi??,
Kusema kweli sijaona kitu cha ajabu hapo!,normal life kabisa you hustle you get! Mbona ni mtiririko usionashaka.. kuwapita wanaojua kiingereza huo nao ni muujiza.. angalia pia personality yako huenda ikawa inavutia kwa wengi wala sijaona muujiza, kwenye interview huenda una jiamini shinda wengine n.k

Mungu wako siku akiinua wagonjwa waliolala mahospitalini kwa dk moja ndo nitajua yeye ni Mungu nje na hapo hizi stori ni kitu cha kawaida sana ila wewe tu vile unazichukulia as muujiza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe mtoa mada nadhani u were just lucky, kuomba Mungu na kupata majibu si rahisi kihivyo, ingekuwa Mungu anajibu maombi kirahis hivyo, basi kusingekua na maskini duniani, na duniani kusingekuepo na wanaokufa njaa, watu wasingeenda Kwa waganga wa kienyeji, kama Mungu anajibu maombi kirahisi, wale waliomuomba Mungu na hawajajibiwa, waje kutoa ushuhuda wao hapa Heaven Seeker
Yakobo sura ya kwanza

5 Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
6 Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku.
7 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana.
8 Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.

Naye Yesu alisema hivi katika Marko 11
23 Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.
24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.


Hivyo, mhimu wakati unaomba, usiwe na shaka.
 
Aisee inashangaza sana unakosa hofu ya Mungu kabisa hadi una comment hivi??,

Sent using Jamii Forums mobile app
He he! Wacha uoga wewe kipi hakiwezi semeleka..?
Maisha ni uhalisia,wengi wanaoumwa wapo hospitalini lkn kwanini hao watu wenu wa Mungu huangaika na waliopo nyumbani!! Kama Mungu anaponya,anatibu na anahuruma kwanini watu hawamkimbilii wanakimbilia hospitalini wakatibiwe..??

Mungu haiminiwi Kama first class! Bali last chance!! Na kwavile maisha ni halisi nani ataamini kuwa nikivunjika mfupa Mungu atauunga kwa sekunde ama dk hiyohiyo!! Si bora kwenda hospitali kutibiwa mfupa ujiunge kwa wiki kadhaa kuliko kusubiri muujiza ambao sifahamu kama upo au haupo!!

Vitu vya Mungu vimekaa kinadharia zaidi kuliko kihalisia ndio maana wengine hatumuamini!!
Nitakuelewa vipi Mungu anahuruma wakati nikienda mahospitalini watu wanahangaika bora kufa!!
Nitakuelewa vipi Mungu anajali wakati kuna viumbe vyake mwenyewe vinateseka bora kufa!!
Hivi wewe kama mzazi umemzaa mwanao lkn anakuambia heri afe unafikiri nini..?

Ulichomezeshwa ndicho umekishika
Una hofu ya Mungu ila hauna hofu ya uhalisia wa maisha!
Jitahidi kurefusha fikra zako kwamwe hautamuona Mungu kama mtegemezi bali sheria zilizopo za nature zitaamua nini kifanyike juu yako!! Na si yeye Kama ulivyoaminishwa.
 
Shuhuda huwapa watu sababu za kumkubali,kumuamini na kumfuata MUNGU. Hii ni injili tosha.
 
Uwanja wa walokole huu...... Mbarikiwe Sana watumishi wa Bwana.
 
Kipindi hiki ambacho kumeibuka taharuki Ulimwenguni kote kutokana na COVID 19, ambapo imefikia hatua hata wale ambao siku zote husema tunamtegemea Mungu kwa kila jambo, nasi tunaanza kukosa matumaini na kujawa na hofu, na kudhani huenda Mungu husaidia mambo flani flani au wakati flani flani ila siyo kwa janga kama hili la COVID19.

Nimeona nije na ushuhuda wa namna Mungu alivyowahi kunitendea kwa kila nilipomuomba na huenda ikaongeza kiwango chako cha imani na kupunguza hofu ya COVID 19. Kisha kuweka tumaini kwa Mungu zaidi na siyo hofu ya kifo kutokana na COVID19.

Bila kupoteza muda na nafasi, naanza moja kwa moja kama ifuatavyo;

1) Mwaka 2010 nikiwa nimekosa tumaini la kulipa ada ya shule na kutishiwa kutoendelea na masomo yangu, Mkuu wa shule aliniita ofisini kwake na kunipa muda wa kipindi cha wiki moja niwe nimelipa ada na michango yote niiliyokuwa nadaiwa shuleni hapo.

Kipindi hicho nilikuwa kidato cha sita. Muda mfupi kabla ya kuitwa na Mkuu huyo wa shule, nilikuwa katika kipindi cha maombi. Baada ya kutoka ofisini, dakika chache baadae, niliitwa tena kwa Mkuu huyo wa shule, nikamkuta Mama mmoja ambaye kumbe Mkuu wa shule alimsimlia maswahibu yangu.

Mama huyo alikuwa akihusika na Taasisi inayosaidia watoto walio katika mazingira magumu. Nilipofika Ofisini, Mama yule akajitolea kunilipia ada na madeni yangu yote. Mungu alijibu maombi yangu. Hakika.!

2) Mwaka 2014 baada ya kuhitimu Chuo. Sikuwa na kazi ya kuniingizia kipato. Siku moja nilikosa kabisa hata pesa kwa ajili ya chakula. Nikalia machozi na kumwambia Mungu kwa nini niteseke namna ile? Baada ya dakika kama 10 hivi, rafiki yangu mmoja alinipigia simu na kuniambia kuna kazi imepatikana Dar es Salaam, nijiandae kwa ajili ya interview kesho yake.

Mungu ni mwema, nilifaulu interview na kupata kazi ile japokuwa ilikuwa ni ya muda mfupi (Miezi 4). Chakushangaza, huyo rafiki yangu hakupata ila mimi nikapata.

3) Mwaka 2015 nikiwa natafuta kazi nyingine, rafiki yangu mmoja akanipigia tena simu na kuniambia kuna kazi naweza kuomba japokuwa muda wa kufanya maombi ulikuwa umekwishapita kwa saa kama 4 hivi. Nikamwambia asijali, anipe tu link nifanye application hivyohivyo, nikamuomba sana Mungu na kweli nikafanikiwa kuitwa kwenye Interview.

Inashangaza maana muda ulikuwa umekwishapita ila bado nikafanikiwa kuitwa. Chakushangaza zaidi, rafiki yangu aliyenipa connection hakuitwa kwenye interview ila mimi nikaitwa.

4) Siku ya interview, nilifunga na kuomba. Chakushangaza, kwakuwa ilikuwa ni Private company ya kutoka nje ya nchi, kulikuwa na vijana wengi waliosoma shule wanakofundisha kiingereza vizuri (achana na akina sisi tuliopitia shule za Saint Kayumba), na hivyo kuwa na chance kubwa ya kuchaguliwa kutokana na kujieleza vizuri kwa kimombo.

Wale jamaa walikuwa wanaongea English fluently mpaka nikaanza kuwaza, Je mimi mwenye ki-english cha kupinda pinda nitafanikiwa kweli? Isitoshe kampuni ilikuwa ya nje na Ki-English ilikuwa ni muhimu.

Cha ajabu ni kuwa, tulikuwa vijana kama 10 hivi, na kulikuwa na michujo miwili, yaani wenzangu wote niliowahofia hawakuendelea hata kwa interview ya pili ila mimi nikaendelea. Cha ajabu zaidi, katika wote tuliofanya interview (zaidi ya 10) siku hiyo katika mkoa huo tulifanikiwa vijana wawili pekee.

5) Mwaka huohuo 2015 mwishoni nikapata kazi mahala kwingine, kukawa na kila dalili za mimi kuwa team leader katika kituo chetu cha kazi. Sasa kulikuwa na kijana mmoja ambaye alikuwa ametangulia na alipenda sana kuwa Team leader, wakati huo alikuwa akiongoza kwa muda tu. Na ikawa kama kuna kinyongo flani kuwa nimeenda kuchukuwa nafasi yake maana nilimzidi elimu.

Sasa nikamuomba sana Mungu kuwa aniepushie na ugomvi na mafarakano mahali pangu pa kazi na kama kweli amekusudia mimi niwe team leader basi anipe nafasi hiyo kwa amani na upendo na siyo kwa chuki na mafarakano.

Kweli bwana, baada ya muda mfupi nikachaguliwa kuwa team leader. Chakushangaza yule ndugu niliyemkuta akakubali kwa roho safi na kuonesha ushirikiano kwangu mpaka mwisho.

6) Mwaka 2018 nikafanya application ya kupata scholarship, chakushangaza, sikuwa nimetuma passport maana kipindi hicho sikuwa nayo. Nikamwachia Mungu na kumuomba kuwa, kama ni mapenzi yake mimi kupata. Basi passport isiwe kikwazo japokuwa ilikuwa ni miongoni mwa requirement muhimu.

Siku moja kabla ya majina kutangaza, nikapata email kuwa natakiwa kuambatanisha passport ili maombi yangu yaweze kuzingatiwa. Nikajibu kuwa sina na nikaahidi kuwa endapo wao watanipatia nafasi hiyo, nipo tayari kushughulia ndani ya muda mfupi (wiki 2), sikuwa na uhakika wa kupata ila nikajipa matumaini kuwa katika Mungu yote yanawezekana.

Kumbuka wakati wote huo nilikuwa nikimuomba sana Mungu anisaidie nifanikiwe. Basi bwana, Mungu ni mwema sana, kesho yake yakatoka majina na nikachaguliwa.

7) Wiki hiyohiyo nikaanza mchakato wa kushughulikia passport. Kuipata si kazi rahisi, bila shaka ambao wanazo watatoa ushuhuda hapa ilivyo kazi ngumu kupata passport. Chakushangaza, nikaenda Uhamiaji makao makuu na kujieleza huku nikiwa na document zote muhimu (Ikumbukwe hata ukiwa na documents bado si rahisi kuipata kwa muda mfupi kama unavyodhani). Nikamuomba tena Mungu aingilie kati. Kama natania vile, nikapata passport ndani ya siku moja. Mungu ni mwema sana.

Noamba nifupishe tu kwa leo, hayo ni machache sana katika mengi niliyo nayo. Nikiamua kuandika kila kitu hapa nitajaza kitabu chenye maelfu ya kurasa. Natambua kuwa mimi siyo mcha Mungu na wala si mkamilifu kwa kiwango cha juu sana kama inavyopaswa kuwa, lakini, itoshe kusema kuwa Mungu amekuwa mwema sana na mambo mengi ambayo nimekuwa nikimuomba ananipa kama nilivyomuomba. Mpaka huwa najishangaa, inakuwaje haswa? Licha ya changamoto za hapa na pale ila kwa kiasi kikubwa naona Mungu akijibu maombi yangu mengi sana.

Kwa sasa nipo huku kwenye nchi za baridi ambako COVID 19 imepamba moto, achana na home ambako naona walioambukizwa ni 6. Huku niliko ni karibia kila mji watu wameambukizwa na maambukizi ni kuanzia maelfu ya watu na kuna baadhi wamepoteza maisha tayari.

Bado namuomba Mungu aendelee kunitetea na nina Imani atanivusha salama na siku moja nitakuja tena kuendeleza Ushuhuda kuanzia nilipokomea siku ya leo. Bila shaka ushuhuda huu unaweza kwa namna moja ama nyingine kuinua kiwango chako cha imani hasa kipindi hiki ambacho Ulimwengu mzima umekuwa na hofu ya COVID 19. Mungu atulinde.
unasali kanisa gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom