USHUHUDA: Namna ambavyo Mungu amekuwa akijibu maombi yangu

Heaven Seeker

JF-Expert Member
May 12, 2017
478
1,046
Kipindi hiki ambacho kumeibuka taharuki Ulimwenguni kote kutokana na COVID 19, ambapo imefikia hatua hata wale ambao siku zote husema tunamtegemea Mungu kwa kila jambo, nasi tunaanza kukosa matumaini na kujawa na hofu, na kudhani huenda Mungu husaidia mambo flani flani au wakati flani flani ila siyo kwa janga kama hili la COVID19.

Nimeona nije na ushuhuda wa namna Mungu alivyowahi kunitendea kwa kila nilipomuomba na huenda ikaongeza kiwango chako cha imani na kupunguza hofu ya COVID 19. Kisha kuweka tumaini kwa Mungu zaidi na siyo hofu ya kifo kutokana na COVID19.

Bila kupoteza muda na nafasi, naanza moja kwa moja kama ifuatavyo;

1) Mwaka 2010 nikiwa nimekosa tumaini la kulipa ada ya shule na kutishiwa kutoendelea na masomo yangu, Mkuu wa shule aliniita ofisini kwake na kunipa muda wa kipindi cha wiki moja niwe nimelipa ada na michango yote niiliyokuwa nadaiwa shuleni hapo.

Kipindi hicho nilikuwa kidato cha sita. Muda mfupi kabla ya kuitwa na Mkuu huyo wa shule, nilikuwa katika kipindi cha maombi. Baada ya kutoka ofisini, dakika chache baadae, niliitwa tena kwa Mkuu huyo wa shule, nikamkuta Mama mmoja ambaye kumbe Mkuu wa shule alimsimlia maswahibu yangu.

Mama huyo alikuwa akihusika na Taasisi inayosaidia watoto walio katika mazingira magumu. Nilipofika Ofisini, Mama yule akajitolea kunilipia ada na madeni yangu yote. Mungu alijibu maombi yangu. Hakika.!

2) Mwaka 2014 baada ya kuhitimu Chuo. Sikuwa na kazi ya kuniingizia kipato. Siku moja nilikosa kabisa hata pesa kwa ajili ya chakula. Nikalia machozi na kumwambia Mungu kwa nini niteseke namna ile? Baada ya dakika kama 10 hivi, rafiki yangu mmoja alinipigia simu na kuniambia kuna kazi imepatikana Dar es Salaam, nijiandae kwa ajili ya interview kesho yake.

Mungu ni mwema, nilifaulu interview na kupata kazi ile japokuwa ilikuwa ni ya muda mfupi (Miezi 4). Chakushangaza, huyo rafiki yangu hakupata ila mimi nikapata.

3) Mwaka 2015 nikiwa natafuta kazi nyingine, rafiki yangu mmoja akanipigia tena simu na kuniambia kuna kazi naweza kuomba japokuwa muda wa kufanya maombi ulikuwa umekwishapita kwa saa kama 4 hivi. Nikamwambia asijali, anipe tu link nifanye application hivyohivyo, nikamuomba sana Mungu na kweli nikafanikiwa kuitwa kwenye Interview.

Inashangaza maana muda ulikuwa umekwishapita ila bado nikafanikiwa kuitwa. Chakushangaza zaidi, rafiki yangu aliyenipa connection hakuitwa kwenye interview ila mimi nikaitwa.

4) Siku ya interview, nilifunga na kuomba. Chakushangaza, kwakuwa ilikuwa ni Private company ya kutoka nje ya nchi, kulikuwa na vijana wengi waliosoma shule wanakofundisha kiingereza vizuri (achana na akina sisi tuliopitia shule za Saint Kayumba), na hivyo kuwa na chance kubwa ya kuchaguliwa kutokana na kujieleza vizuri kwa kimombo.

Wale jamaa walikuwa wanaongea English fluently mpaka nikaanza kuwaza, Je mimi mwenye ki-english cha kupinda pinda nitafanikiwa kweli? Isitoshe kampuni ilikuwa ya nje na Ki-English ilikuwa ni muhimu.

Cha ajabu ni kuwa, tulikuwa vijana kama 10 hivi, na kulikuwa na michujo miwili, yaani wenzangu wote niliowahofia hawakuendelea hata kwa interview ya pili ila mimi nikaendelea. Cha ajabu zaidi, katika wote tuliofanya interview (zaidi ya 10) siku hiyo katika mkoa huo tulifanikiwa vijana wawili pekee.

5) Mwaka huohuo 2015 mwishoni nikapata kazi mahala kwingine, kukawa na kila dalili za mimi kuwa team leader katika kituo chetu cha kazi. Sasa kulikuwa na kijana mmoja ambaye alikuwa ametangulia na alipenda sana kuwa Team leader, wakati huo alikuwa akiongoza kwa muda tu. Na ikawa kama kuna kinyongo flani kuwa nimeenda kuchukuwa nafasi yake maana nilimzidi elimu.

Sasa nikamuomba sana Mungu kuwa aniepushie na ugomvi na mafarakano mahali pangu pa kazi na kama kweli amekusudia mimi niwe team leader basi anipe nafasi hiyo kwa amani na upendo na siyo kwa chuki na mafarakano.

Kweli bwana, baada ya muda mfupi nikachaguliwa kuwa team leader. Chakushangaza yule ndugu niliyemkuta akakubali kwa roho safi na kuonesha ushirikiano kwangu mpaka mwisho.

6) Mwaka 2018 nikafanya application ya kupata scholarship, chakushangaza, sikuwa nimetuma passport maana kipindi hicho sikuwa nayo. Nikamwachia Mungu na kumuomba kuwa, kama ni mapenzi yake mimi kupata. Basi passport isiwe kikwazo japokuwa ilikuwa ni miongoni mwa requirement muhimu.

Siku moja kabla ya majina kutangaza, nikapata email kuwa natakiwa kuambatanisha passport ili maombi yangu yaweze kuzingatiwa. Nikajibu kuwa sina na nikaahidi kuwa endapo wao watanipatia nafasi hiyo, nipo tayari kushughulia ndani ya muda mfupi (wiki 2), sikuwa na uhakika wa kupata ila nikajipa matumaini kuwa katika Mungu yote yanawezekana.

Kumbuka wakati wote huo nilikuwa nikimuomba sana Mungu anisaidie nifanikiwe. Basi bwana, Mungu ni mwema sana, kesho yake yakatoka majina na nikachaguliwa.

7) Wiki hiyohiyo nikaanza mchakato wa kushughulikia passport. Kuipata si kazi rahisi, bila shaka ambao wanazo watatoa ushuhuda hapa ilivyo kazi ngumu kupata passport. Chakushangaza, nikaenda Uhamiaji makao makuu na kujieleza huku nikiwa na document zote muhimu (Ikumbukwe hata ukiwa na documents bado si rahisi kuipata kwa muda mfupi kama unavyodhani). Nikamuomba tena Mungu aingilie kati. Kama natania vile, nikapata passport ndani ya siku moja. Mungu ni mwema sana.

Noamba nifupishe tu kwa leo, hayo ni machache sana katika mengi niliyo nayo. Nikiamua kuandika kila kitu hapa nitajaza kitabu chenye maelfu ya kurasa. Natambua kuwa mimi siyo mcha Mungu na wala si mkamilifu kwa kiwango cha juu sana kama inavyopaswa kuwa, lakini, itoshe kusema kuwa Mungu amekuwa mwema sana na mambo mengi ambayo nimekuwa nikimuomba ananipa kama nilivyomuomba. Mpaka huwa najishangaa, inakuwaje haswa? Licha ya changamoto za hapa na pale ila kwa kiasi kikubwa naona Mungu akijibu maombi yangu mengi sana.

Kwa sasa nipo huku kwenye nchi za baridi ambako COVID 19 imepamba moto, achana na home ambako naona walioambukizwa ni 6. Huku niliko ni karibia kila mji watu wameambukizwa na maambukizi ni kuanzia maelfu ya watu na kuna baadhi wamepoteza maisha tayari.

Bado namuomba Mungu aendelee kunitetea na nina Imani atanivusha salama na siku moja nitakuja tena kuendeleza Ushuhuda kuanzia nilipokomea siku ya leo. Bila shaka ushuhuda huu unaweza kwa namna moja ama nyingine kuinua kiwango chako cha imani hasa kipindi hiki ambacho Ulimwengu mzima umekuwa na hofu ya COVID 19. Mungu atulinde.
 
Waache wasio amini waendelee kupambana kivyao kwa akili zao na nguvu zao ambazo zinakikomo
Sisi tuendelee kumuita huyu ambaye amekuwa wonderful to us afanye pale Ambapo sisi hatuwezi na kutupa wepesi wa maisha

Utukufu ni kwake yeye aliyefanya hayo Naamini ni mengi zaidi ya hayo kwa kuwa MUNGU yu hai na anaishi na ataendelea kuishi
 
Faith can move mountains...
I have seen more than that.

Mungu yupo!kama huamini we ni mwehu tu fulan,ila Mungu yupo na ukimwomba kwa uaminifu unapata...

Huyu mungu hutazama uaminifu wa moyo wa mtu wala si sura,dini na kabila...huwapa wote waovu na wasio waovu...

Ili jina lake libaki kuitwa MUngu
 
Kipindi hiki ambacho kumeibuka taharuki Ulimwenguni kote kutokana na COVID 19, ambapo imefikia hatua hata wale ambao siku zote husema tunamtegemea Mungu kwa kila jambo, nasi tunaanza kukosa matumaini na kujawa na hofu, na kudhani huenda Mungu husaidia mambo flani flani au wakati flani flani ila siyo kwa janga kama hili la COVID19, nimeona nije na ushuhuda wa namna Mungu alivyowahi kunitendea kwa kila nilipomuomba na huenda ikaongeza kiwango chako cha imani na kupunguza hofu ya COVID 19. Kisha kuweka tumaini kwa Mungu zaidi na siyo hofu ya kifo kutokana na COVID19.

Bila kupoteza muda na nafasi, naanza moja kwa moja kama ifuatavyo;

1) Mwaka 2010 nikiwa nimekosa tumaini la kulipa ada ya shule na kutishiwa kutoendelea na masomo yangu, Mkuu wa shule aliniita ofsin kwake na kunipa muda wa kipindi cha wiki moja niwe nimelipa ada na michango yote niliyokuwa nadaiwa shuleni hapo. Kipindi hicho nilikuwa kidato cha sita. Muda mfupi kabla ya kuitwa na Mkuu huyo wa shule, nilikuwa katika kipindi cha maombi. Baada ya kutoka ofsin, dakika chache baadae, niliitwa tena kwa Mkuu huyo wa shule, nikamkuta Mama mmoja ambaye kumbe Mkuu wa shule alimsimlia maswahibu yangu. Mama huyo alikuwa akihusika na Taasisi inayosaidia watoto walio katika mazingira magumu. Nilipofika Ofsin, Mama yule akajitolea kunilipia ada na madeni yangu yote. Mungu alijibu maombi yangu. Hakika.!

2) Mwaka 2014 baada ya kuhitimu Chuo. Sikuwa na kazi ya kuniingizia kipato. Siku moja nilikosa kabisa hata pesa kwa ajili ya chakula. Nikalia machozi na kumwambia Mungu kwa nini niteseke namna ile? Baada ya dakika kama 10 hivi, rafiki yangu mmoja alinipigia simu na kuniambia kuna kazi imepatikana Dar es Salaam, nijiandae kwa ajili ya interview kesho yake. Mungu ni mwema, nilifaulu interview na kupata kazi ile japokuwa ilikuwa ni ya muda mfupi (Miezi 4). Chakushangaza, huyo rafiki yangu hakupata ila mimi nikapata.

3) Mwaka 2015 nikiwa natafuta kazi nyingine, rafiki yangu mmoja akanipigia tena simu na kuniambia kuna kazi naweza kuomba japokuwa muda wa kufanya maombi ulikuwa umekwishapita kwa saa kama 4 hivi. Nikamwambia asijali, anipe tu link nifanye application hivyohivyo, nikamuomba sana Mungu na kweli nikafanikiwa kuitwa kwenye Interview. Inashangaza maana muda ulikuwa umekwishapita ila bado nikafanikiwa kuitwa. Chakushangaza zaidi, rafiki yangu aliyenipa connection hakuitwa kwenye interview ila mimi nikaitwa.

4) Siku ya interview, nilifunga na kuomba. Chakushangaza, kwakuwa ilikuwa ni Private company ya kutoka nje ya nchi, kulikuwa na vijana wengi waliosoma shule wanakofundisha kiingereza vizuri (achana na akina sisi tuliopitia shule za Saint Kayumba), na hivyo kuwa na chance kubwa ya kuchaguliwa kutokana na kujieleza vizuri kwa kimombo. Wale jamaa walikuwa wanaongea English fluently mpaka nikaanza kuwaza, Je mimi mwenye ki-english cha kupinda pinda nitafanikiwa kweli? Isitoshe kampuni ilikuwa ya nje na Ki-English ilikuwa ni muhimu. Cha ajabu ni kuwa, tulikuwa vijana kama 10 hivi, na kulikuwa na michujo miwili, yaani wenzangu wote niliowahofia hawakuendelea hata kwa interview ya pili ila mimi nikaendelea. Cha ajabu zaidi, katika wote tuliofanya interview (zaidi ya 10) siku hiyo katika mkoa huo tulifanikiwa vijana wawili pekee.

5) Mwaka huohuo 2015 mwishoni nikapata kazi mahala kwingine, kukawa na kila dalili za mimi kuwa team leader katika kituo chetu cha kazi. Sasa kulikuwa na kijana mmoja ambaye alikuwa ametangulia na alipenda sana kuwa Team leader, wakati huo alikuwa akiongoza kwa muda tu. Na ikawa kama kuna kinyongo flani kuwa nimeenda kuchukuwa nafasi yake maana nilimzidi elimu. Sasa nikamuomba sana Mungu kuwa aniepushie na ugomvi na mafarakano mahali pangu pa kazi na kama kweli amekusudia mimi niwe team leader basi anipe nafasi hiyo kwa amani na upendo na siyo kwa chuki na mafarakano. Kweli bwana, baada ya muda mfupi nikachaguliwa kuwa team leader. Chakushangaza yule ndugu niliyemkuta akakubali kwa roho safi na kuonesha ushirikiano kwangu mpaka mwisho.

6) Mwaka 2018 nikafanya application ya kupata scholarship, chakushangaza, sikuwa nimetuma passport maana kipindi hicho sikuwa nayo. Nikamwachia Mungu na kumuomba kuwa, kama ni mapenzi yake mimi kupata. Basi passport isiwe kikwazo japokuwa ilikuwa ni miongoni mwa requirement muhimu. Siku moja kabla ya majina kutangaza, nikapata email kuwa natakiwa kuambatanisha passport ili maombi yangu yaweze kuzingatiwa. Nikajibu kuwa sina na nikaahidi kuwa endapo wao watanipatia nafasi hiyo, nipo tayari kushughulia ndani ya muda mfupi (wiki 2), sikuwa na uhakika wa kupata ila nikajipa matumaini kuwa katika Mungu yote yanawezekana. Kumbuka wakati wote huo nilikuwa nikimuomba sana Mungu anisaidie nifanikiwe. Basi bwana, Mungu ni mwema sana, kesho yake yakatoka majina na nikachaguliwa.

7) Wiki hiyohiyo nikaanza mchakato wa kushughulikia passport. Kuipata si kazi rahisi, bila shaka ambao wanazo watatoa ushuhuda hapa ilivyo kazi ngumu kupata passport. Chakushangaza, nikaenda Uhamiaji makao makuu na kujieleza huku nikiwa na document zote muhimu (Ikumbukwe hata ukiwa na documents bado si rahisi kuipata kwa muda mfupi kama unavyodhani). Nikamuomba tena Mungu aingilie kati. Kama natania vile, nikapata passport ndani ya siku moja. Mungu ni mwema sana.

Noamba nifupishe tu kwa leo, hayo ni machache sana katika mengi niliyo nayo. Nikiamua kuandika kila kitu hapa nitajaza kitabu chenye maelfu ya kurasa. Natambua kuwa mimi siyo mcha Mungu na wala si mkamilifu kwa kiwango cha juu sana kama inavyopaswa kuwa, lakini, itoshe kusema kuwa Mungu amekuwa mwema sana na mambo mengi ambayo nimekuwa nikimuomba ananipa kama nilivyomuomba. Mpaka huwa najishangaa, inakuwaje haswa? Licha ya changamoto za hapa na pale ila kwa kiasi kikubwa naona Mungu akijibu maombi yangu mengi sana.

Kwa sasa nipo huku kwenye nchi za baridi ambako COVID 19 imepamba moto, achana na home ambako naona walioambukizwa ni 6. Huku niliko ni karibia kila mji watu wameambukizwa na maambukizi ni kuanzia maelfu ya watu na kuna baadhi wamepoteza maisha tayari. Bado namuomba Mungu aendelee kunitetea na nina Imani atanivusha salama na siku moja nitakuja tena kuendeleza Ushuhuda kuanzia nilipokomea siku ya leo. Bila shaka ushuhuda huu unaweza kwa namna moja ama nyingine kuinua kiwango chako cha imani hasa kipindi hiki ambacho Ulimwengu mzima umekuwa na hofu ya COVID 19. Mungu atulinde.
NAKWAMBIA HIVI "HATA MPAGANI ANAZO SHUHUDA KAMA HIZI ZAKO" JIpange uje tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

96 Reactions
Reply
Back
Top Bottom