Ushuhuda Kwa tuliowahi kupata mauza uza kwenye maisha

Manifestation

Senior Member
Jan 22, 2020
193
315
Kabla sijaleta stori yangu, kila ambaye mtu wake wa karibu (mke/Mme/ndugu/rafiki/mfanyakazi) ambaye huwa unamsaidia Mambo mengi kuanzia ushauri fedha na kumwambia Siri zako nyingi za maisha kama mipango yako ya maendeleo kama kununua Kiwanja/ gari/ nyumba kupata kazi na baadae kukugeuka Kwa kukufanyia madhilla Kwa kwenda Kwa mganga au kufanyia uchawi ili kuugua magonjwa ya ajabu kama ukichaa, uvimbe, kufukuzwa kazi, kufilisika, kupata ajali, kuibiwa, kuunguliwa na nyumba/gari, tupeane ushuhuda ulichomokaje kwenye Hilo jaribu na kama unaendeleza nalo ni hatua zipi umeshachukua na unaendeleza kuchukua.

True story kuna rafiki yangu alikuwa na kazi nzuri kwenye ofisi za madini , alikuwa akipata hela sana na kuweza kusapoti ndugu jamaa na marafiki, Ila baada ya muda alipata ugonjwa uliomsababishia akashindwa kufanya kazi kabisa, baada ya hapo kaachishwa kazi akaanza kuhudhuria sehemu mbalimbali za maombi hapa Tanzania kwa muda wa kama miezi sita Ila hakupata majibu.

Baadae akapata nafasi kwenda Kwa nabii mmoja nje akapona na kuambiwa akirudi Tanzania akazane na maombi maana huko urudipo utapata Vita kubwa sana kama hutosimama, baada ya hapo akarudi akaanza tafuta sehemu ambayo ni ya kiroho akaanza kuwa anaomba kweli kweli, Hana kazi na mume Hana kazi wanakomaa wote anaitwa kwenye usaili kwenye taasisi kubwa ikifikia wakati wakumaliza dili anaachwa, siku Moja yupo kwenye maombi makali akasikia sauti inamwambia mfanyakazi wa ndani, ikabidi ibada inayofuata aende na mfanya kazi wake kanisani, anafika Tu muda wa maombi mfanyakazi kaanza kufunguka.

Mimi ndo ninatumiwa na rafiki yako kuhakikisha hupati kazi, ndo tulikuwekea ugonjwa Ila tokea umetoka nje unaomba sana hatukuwezi, hata kazi ukiomba tunajua ila tunazuia usipate kwani tunateka fikra za waajiri kila inapotokea unataka kusaini dili tunazuia, mwisho WA siku akawa amefunguliwa na mfanyakazi akafunguliwa rafiki anaogopa kumtafuta, maisha yamerudi vizuri anapata madili ya maana, usafiri anao tayari na wote na Mme wake Kwa SASA Wana kazi na maisha yanaenda vizuri.

Stori yangu inakuja Karibuni Kwa ushuhuda wa jinsi ulivyoweza ruka viunzi na hatua ulizochukua kuweza kushinda Mambo ambayo hayaeleweki kwenye maisha.

Nilichojifunza mpaka sasa usijiweke karibu na watu wanaweza kujua mipango yako na njia zako za maisha kumbuka hii ni Africa, (Africa ni sehemu pekee MTU anaweza kutaka kuomba mkopo ili ajue mashambulizi ya uchumi wako yanafika?, Au anakupgia simu kukujulia Hali ajue ugonjwa aliokutumia umeupata?)
 
Naomba mawasiliano yake mkuu
Kabla sijaleta stori yangu, kila ambaye mtu wake wa karibu (mke/Mme/ndugu/rafiki/mfanyakazi) ambaye huwa unamsaidia Mambo mengi kuanzia ushauri fedha na kumwambia Siri zako nyingi za maisha kama mipango yako ya maendeleo kama kununua Kiwanja/ gari/ nyumba kupata kazi na baadae kukugeuka Kwa kukufanyia madhilla Kwa kwenda Kwa mganga au kufanyia uchawi ili kuugua magonjwa ya ajabu kama ukichaa, uvimbe, kufukuzwa kazi, kufilisika, kupata ajali, kuibiwa, kuunguliwa na nyumba/gari, tupeane ushuhuda ulichomokaje kwenye Hilo jaribu na kama unaendeleza nalo ni hatua zipi umeshachukua na unaendeleza kuchukua.

True story kuna rafiki yangu alikuwa na kazi nzuri kwenye ofisi za madini , alikuwa akipata hela sana na kuweza kusapoti ndugu jamaa na marafiki, Ila baada ya muda alipata ugonjwa uliomsababishia akashindwa kufanya kazi kabisa, baada ya hapo kaachishwa kazi akaanza kuhudhuria sehemu mbalimbali za maombi hapa Tanzania kwa muda wa kama miezi sita Ila hakupata majibu.

Baadae akapata nafasi kwenda Kwa nabii mmoja nje akapona na kuambiwa akirudi Tanzania akazane na maombi maana huko urudipo utapata Vita kubwa sana kama hutosimama, baada ya hapo akarudi akaanza tafuta sehemu ambayo ni ya kiroho akaanza kuwa anaomba kweli kweli, Hana kazi na mume Hana kazi wanakomaa wote anaitwa kwenye usaili kwenye taasisi kubwa ikifikia wakati wakumaliza dili anaachwa, siku Moja yupo kwenye maombi makali akasikia sauti inamwambia mfanyakazi wa ndani, ikabidi ibada inayofuata aende na mfanya kazi wake kanisani, anafika Tu muda wa maombi mfanyakazi kaanza kufunguka,

Mimi ndo ninatumiwa na rafiki yako kuhakikisha hupati kazi, ndo tulikuwekea ugonjwa Ila tokea umetoka nje unaomba sana hatukuwezi, hata kazi ukiomba tunajua ila tunazuia usipate kwani tunateka fikra za waajiri kila inapotokea unataka kusaini dili tunazuia, mwisho WA siku akawa amefunguliwa na mfanyakazi akafunguliwa rafiki anaogopa kumtafuta, maisha yamerudi vizuri anapata madili ya maana, usafiri anao tayari na wote na Mme wake Kwa SASA Wana kazi na maisha yanaenda vizuri

Stori yangu inakuja Karibuni Kwa ushuhuda wa jinsi ulivyoweza ruka viunzi na hatua ulizochukua kuweza kushinda Mambo ambayo hayaeleweki kwenye maisha.

Nilichojifunza mpaka sasa usijiweke karibu na watu wanaweza kujua mipango yako na njia zako za maisha kumbuka hii ni Africa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom