Ishi maisha kwa uhuru

Richard mtao

JF-Expert Member
May 13, 2018
209
236
Hivi karibuni wimbi kubwa sana la watu especially vijana wanapitia wakati mgumu sana kuishi maisha yao.

Idadi kubwa ya watu wamedanganywa na kupumbazwa na mtindo mpya wa maisha unaosukumwa/kuchochewa na ukuaji wa mitandao ya kijamii.

Unakuta mtu ni maskini sana lakini kwakua anataka kuionesha jamii yeye ni mtu mwenye mafanikio kiasi gani anajikuta anaishi maisha ya watu wenye mafanikio hali ambayo inamfanya mtu huyu aishi kwa mateso makubwa au kuwaza kufanya matukio ya kiharifu( wizi, kuloga, usagaji, urawiti, utapeli, kuuza mali za familia ki wizi na n.k) ilimradi apate mshiko wa kuendelea kuvimbia mademu, na wana huko mtaani.

Lengo la uzi huu ni:
1. Kuwasihi vijana wenzangu kuacha ulimbukeni. Mitandao ipo na itaendelea kuepo. Tufanye kazi kwa bidii na tushukuur kwa kidogo tulichopata na tukitumie vzr ili kuzalisha zaidi.

2. Jikubali the way ulivyo.
Kama kipato chako ni kidogo kubali na uishi kulingana na hicho kipato, acha kutumia nguvu kubwa kuaminisha watu kwamba wewe ni tajiri badala yake tumia nguvu izo kufanya vibarua au kazi yoyote halali ili upate zaidi.

3. Jijenge kimaadili, imani na kielimu.
'Biblia inasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa'

'Biblia inasema asiefanya kazi na asile'

Mwaljmu wangu aliwahi kusema elimu haina mwisho na elimu ni kile kinachobaki kichwani baada ya mtihani. Pia alisema elimu inafanya mtu astarabike yaan ajue kuishi na jamii na watu wake wote.

Kwaiyo ndugu zangu mitandao isitumalizie akili mpka kufikia hatua unafake maisha kisa mtandao wa kijamii.

Ishi maisha yako ya kawaida, huku ukichase ndoto zako kila kitu kinawezekana. Lakini ukichagua maisha ya kufake basi utateseka saan katika maisha haya. Hakuna raha kama kuishi maisha ya kawaida na maisha yako halisi ni raha sana.
 
Ivi karibuni wimbi kubwa sana la watu especially vijana wanapitia wakati mgumu sana kuishi maisha yao.

Idadi kubwa ya watu wamedanganywa na kupumbazwa na mtindo mpya wa maisha unaosukumwa/kuchochewa na ukuaji wa mitandao ya kijamii...
labda ushauri huu uzingatiwe na hawa u20 but above apo ushauri umechelewa kidogo. wa umri huo na kwa mafanikio ya kubeti vijana hawaambiliki hawashauriki,🐒
 
Usiku mwema acha nilale zangu Mimi sitaki tabu na Maisha, Maisha yenyewe mafupi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom