Ushuhuda kutoka kwa wanandoa waliowahi kuachana, hasa mliokuwa na watoto mkaamua kuacha kila kitu na kuanza upya

kissgarage

Member
Mar 28, 2009
80
139
Nawasalimu sana ndugu wana JF.

Kwakweli lengo la ndoa ni kuishi pamoja kwa uaminifu na upendo na kulea familia pamoja.

Nafahamu humu kuna watu wenye caliber tofauti na uwezo wa hali ya juu kupambanua mambo kutokana na experience...

Naomba experience yenu, je ilikuwa rahisi kuanza upya? Kwenda mahakamani kutoa talaka rasmi imeshindikana kabisa..ninachotaka ni kutengana kwa muda napo imeshindikana..hapo more than three children kwenye ndoa wapo involved, ten years na wengine below. Simchukii kabisa mume lakini forgiving and forgetting what happened nashindwa kabisa, imani haipo Yarabi tena...nimekata tamaa kabisa.

Imefikia kipindi natafuta kazi mikoani ili nipone moyo...jamani wenzangu mliwezaje...sijashare na ndugu yangu hata mmoja....nikiwaeleza kila kitu watamchukia na they will never forgive him.

Nimeamua kumstiri mume wangu..sijaandika kila kitu ila baadhi yenu ni wanaume ila mngeumia sana na kutoa chozi...ndoa yetu ni ya serikali...naomba experience yenu especially kwa nyie mliokua na watoto mkaamua kuacha kila kitu na kuanza upya.
 
Kwakweli kuelezea kila kilichotekea nitareaveal identity za watu...ila kikubwa ni usaliti uliovuka mipaka..na yaliyotokana na usaliti ndio mazito zaidi...naombeni msaaada juu ya uzoefu wenu, mimi na mume wangu hatuwezi kurudi kama mwanzo.
 
Kwakweli kuelezea kila kilichotekea nitareaveal identity za watu...ila kikubwa ni usaliti uliovuka mipaka..na yaliyotokana na usaliti ndio mazito zaidi...naombeni msaaada juu ua uzoefu wenu...mimi na mume wangu hatuwezi kurudi kama mwanzo...
Mhhh poleh mummy yaonekana mazito japo hujatueleza
Nashauri uende kwenye maombi ya imani yako
Ama kwa wale wa ushauri nasaha/therapist ushushe huo mzigo uliopo rohoni kwanza
 
Yaliyotokana na tukio yalipelekea tukio la ugomvi mkubwa mkubwa sana kama two weeks ago.. Ndio maana. Naogopa kueleza sana maana mashuhuda iam sure wengi ni jf members kutokana na neighbohood ugomvi uliotokea...wengine wanaweza kuja na hints hapa...mimi nimeamua kujitenga mbali na muhusika ili moyo upone..ila bado imekua ngumu kuna watoto
 
Watu wanataka tu umbea hawana chochote cha zaidi, ishia hapo hapo kuwa mmeachana inatosha, unachoulizia ni uzoefu wa wengine waliopitia njia kama yako kwahiyo kausha zako watakuja yaliyowakuta watakusimulia.

Hawa wanaotaka usimulie ilikuaje hawana lolote zaidi ya umbea na mwisho wakuvamie wewe wakwambie ndio ulizingua thread nzima igeuke kukuandama wewe.

Ila kama utapenda andika yaliyokutokea kama wanavyodai waja, andika ila jua hawatosaidia chochote zaidi ya kukwambia "pole sana"
 
Mhhh poleh mummy yaonekana mazito japo hujatueleza
Nashauri uende kwenye maombi ya imani yako
Ama kwa wale wa ushauri nasaha/therapist ushushe huo mzigo uliopo rohoni kwanza
Ahsante sana...nakufa ndani taratibu...ni degree holder sina kazi basi i am dying. Nimekata tamaa sana, mume wangu sio type ya wanaume wa kukaaa na kuafiki muafaka, ni mtu wa excuses so hatufikii conclusion. Sijaeleza ndugu yangu hata moja, hii ni kumstiri.
 
Cha msingi kuanchana na mtu ni maamuzi magumu labda kama unaweza take ur time hama nyumba kaa ufikirie don't rush to decision, kuachana kunauma sana hasa na Mme au mke. Na wanaoathirika ni watoto zaidi watapitia matatizo ya kisaikolojia mengi asikuambie mtu. Hata kama mama/baba ni mbovu kiasi gani uwepo wake unasiadia sana saikolojia ya ukuaji wa mtoto.

Hatua za divorce ni ngumu kidogo na huchukua muda na kila mtakapoanzia watajaribu sana kuwasuluhisha.

So for the mean time out kupata space kidogo ufikirie na ujitafakari na usifanye maamuzi yeyote yale kwa sasa kwa saana ni Adrenaline hormone ndiyo itakayoamua. Kaaa tulia jipe muda tafakari kwa undani sana shirikisha viongozi wa dini kabla ya wazazi maana wazazi kila mzazi atavutia upande wa mwanae na mara nyingi unaweza tokea msifikie muafaka wowote ule.
 
Najua ni gharama lakini wanaweza kukusaidia na ukapona kabisa

Kama umejariwa kipato tafuta wataalam wa saikolojia mfano wa kina Dr Elly waminiam (sijui spelln zipo sawa) au kina mauki watakusaidia pakubwa mno

Au wasiliana na mchungaji wako kama upo upande huo , au laa jipe muda kidogo
Kuacha familia na kuanza upya yahitaji moyo

Tena bora mtoto angekua mmoja
 
Back
Top Bottom