Ushuhuda: Jinsi ninavyojenga nyumba ya ndoto yangu

Ushuhuda: Jinsi ninavyojenga nyumba ya ndoto yangu

Na hilo linafanya uzi huu uwe na umuhimu zaidi.

Gharama zingekuwa sawa kote, kusingekuwa na haja sana ya uzi kama huu.

Unaelewa hilo?

Zaidi, hata kama gharama ziko sawa, si kila mtu anayezijua. Wasiozijua watafaidika na uzi huu hata kama gharama ziko sawa.

Unaelewa hilo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kuna watu wanajifanya kuponda kumbe ni wivu tu.
 
Hongera mkuu
Binafsi natumia mfumo wa kuwekeza vifaa kwa hardware jirani na site.
Yaan hatua kwa hatua nilianza mwezi september mwaka juzi nashkuru hivi npo kwenye ujenzi wa fence, hapa lengo ni kuhamia nikiwa nimemaliza kila kitu.

Bado kuskim & Blandering
Ila kuna rafiki ameniunganisha na mafundi wanafanya gypsum za kituruki na wala hawahitaji blandering wao hutumia katani na gypsum powder yao special hivi nikirudi january ndio nataka wakanipigie hesabu zao niwakabidhi kazi.

Nilichojifunza ujenzi hautaki pupa unabidi ufanye hatua kwa hatua.
Ni kweli hata Mimi wazazi nyumba yetu walitumia takribani miaka 4 sisi watoto tukawa tunaona inachelewa, loooh siku tumehamia tu mzee akatuweka chini kutupa somo, kuwa kwenye maisha ujenzi wa makazi ya kudumu hauhitaji papara, inatakiwa hatua zifuatwe ili kipatikane kitu bora na kizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujenzi bana!
Nilijikuta najenga nyumba ambayo huwa najiuliza hivi hii hela niliitoa wapi!? Nashindwa kuamini, siku moja nkasema hebu nichukue kitabu changu cha gharama za hii project nifanye majumuisho! Ha ha ha aah! Sikuamini ile figure aisee ILA nikagundua kwamba ni kwa kuwa nilikuwa najenga kidogokidogo! Kujenga ka nyumba kadogo kazuri hata kama ni kaghorofa ni nafuu kuliko kununua gari!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wana JF.

Niliwahi kuahidi kule kwenye uzi wa ujenzi wa nyumba kuwa nitaleta ushuhuda wangu wa ujenzi kwa project ambayo bado naiendeleza ya ujenzi wa nyumba ya kuishi ambayo ni ghorofa moja.

A simple house; ghorofani ni chumba kimoja tu, master bedroom, chini kuna vyumba vitatu vya kulala, sebule, jiko, dinning, store na public toilet and bathroom. Hii nyumba iko Mbeya Mjini, sitaweka picha ili ku mantain anonymity. Source ya hizi taarifa zote ni notebook yangu ambayo nilijitahidi sana kuandika kila senti ninayotumia katika ujenzi huu.

Nilianza ujenzi rasmi tarehe 04/02/2017 nikiwa na jumla ya shilingi 6,000,000.

Matumizi ya kwanza kabisa yalikua jumla ya shilingi 2,218,000 kwa ajili ya maandalizi ya msingi kwa mchanganuo huu;

230,000-Kusafisha kiwanja
850,000-Mawe trip 10
43,500-Koleo,jembe na kamba
500,000-Advance labor charge ya fundi kujenga msingi
20,000-Makarai
150,000-Mchanga trip 1
170,000-Kokoto trip 1 (mende)
15,000-Mbao.
60,000-kuchimba kisima
40,000-Mbao.
Kibali-170,000

March 2017
Nikatoa tena Tshs 1,460,500 kwa ajili ya :Maji ya ujenzi, advance ya fundi,mchanga trip 1,simenti mifuko 20,nondo lola 20, ring beam 5,waya za kusukia 2, na misumari kg 1, mbao (1*10), misumari nchi 1 kg 4.

Nikatumia tena 370,000 kwa ajili ya advance ya fundi na mbao.

Nikatumia tena 1,232,000 kununua: simenti mifuko 34, nondo lola 19, ring beam 23, binding wire 12, misumari kg 3.

Nikatumia tena 498,0000 kununua kokoto, advance ya ufundi, maji,simenti mifuko 12, nondo lola 2.

Nikatoa tena 1,120,000 kununua: Mawe trip 3, kokoto trip 1 (mende), mchanga trip 1, na advance ya fundi.

Nikafunga mwezi wa tatu kwa kutumiaTshs 787,500 kununua Mbao za kuweka kwenye nguzo, mchanga,kokoto (mende) na kukata pamoja na kuranda mbao.

Hii ilikua ni hatua ya kumwaga zege la chini (kufunga mkanda wa chini). na kupandisha nguzo.

Nikavuta pumzi kwanza.

May 2017
Nikafungua mwezi kwa kutumia 651,000 kwenye kokoto, kumalizia hela ya ufundi ya kumwaga jamvi, na maji ya kumwagilia jamvi, pamoja na kununua mifuko 10 ya saruji (simenti)

Nikatoa 2,380,000 kununua matofali (nimetumia matofali ya kuchoma ya Mbozi-ni vitofali fulani vidogo, imara na vina mwonekano wa kupendeza sana).

Nikalipa 1,820,000 kwa ajili ya: Ufundi wa kupandisha boma,kununua damping membrane,chekecheo,mchanga,maji,na simenti mifuko 10.

Nikalipa tena 1,540,000 kwa ajili ya ufundi,mabanzi, mchanga,simenti mifuko 10, kuchekecha mchanga na maji.

June 2017
Nilitumia 1,000,000 kwa ajili ya malipo ya fundi na kununua simenti, nondo, kokoto, mchanga.

Mwezi ukaisha.

July 2017
Mwezi huu kazi ya kupiga jamvi la juu ilifanyika
nilitumia 2,365,000 kwa ajili ya kulipa hela ya ufundi (jamvi la juu), simenti, nondo, mbao, mirunda.

Nikalipa tena 1,522,500 kwa ajili ya misumari, ufundi,bao.

Tukafunga mwezi.

August 2017
Nikaanza mwezi kwa kulipa 1,660,000 ya ufundi, misumari kg 10, nondo lola 40, na milunda.

Nikalipa tena 1,065,000 ya fundi na maji.

Mwezi wa nane ukaisha.

September 2017
Nililipa 2,900,000 ya malipo ya fundi pamoja na mifuko 50 ya simenti.

Mwezi ukaisha.

November 2017
Nililipa 1,552,500 kuongeza matofali (ya kuchoma ya mbozi), pamoja na malipo ya ufundi.

Nikalipa tena 1,183,000 kwa ajili ya mchanga trip 1, misumari, mbao, maji, nondo, simenti.

Mwezi Novemba ukaisha kihivyo.

December 2017
Nililipa 3,705,500 kwa ajili ya ufundi, mchanga lori 2, Matofali (ya mbozi) 2,750, ikiwa ni pamoja na gharama za kusafirisha.

Nikafunga mwaka.

Nilifunga mwaka 2017 nikiwa nimetumia jumla ya shilingi 37,034,500 katika project hii ya Ujenzi.

Jan 2018

Nikafungua mwaka kwa kutumia 2,688,000 kwa ajili ya kununua mbao, kuranda mbao, milunda hard board pamoja na malipo ya ufundi.

Feb 2018
Nilitumia 1,037,500 kwa ajili ya malipo ya fundi na kununua milunda.

Hadi kufika hapa nikawa nimemaliza kupandisha boma na kufunga lenta.

Ikaanza kazi ya kumwaga zege la juu gorofani kabisa; Nilichagua style ya kuweka zege juu ya gorofa badala ya kupaua kwa bati.

Mwezi huu wa Feb pia nilianza kuwekeza kiwanda cha bati kwa kulipia shilingi 800,000; Kwani kuna sehemu zile ambazo hazina gorofa kwa juu, niliplan kupaua kwa bati.

Nikatumia tena 2,061,000 kwa ajili ya kununua kokoto (lori 2), ufundi kwa ajili ya zege la juu, simenti mifuko 50 kwa ajili ya zege la juu pia, maji, mashine ya kushindilia zege, PVC pipes, conduit pipe na round box (hivi ni vifaa vya umeme ambavyo vilihitajika kulazwa kabla zege halijamwagwa), pamoja na hela ya ufundi wa fundi umeme.

Nikawa nimefunga mwezi.

Baada ya hii shughuli, nikavuta pumzi kubwa.

July 2018
Baada ya kuvuta pumzi miezi mitano, shughuli ikaanza tena.

Mwezi huu ndio nilianza heka heka za kupaua.
Nilitumia shilingi 1,370,000 kwa ajili ya kununua mbao, misumari, pamoja na advance ya ufundi wa fundi wa kupaua.

Hapo hapo pia nikaanza shughuli ya kutandaza mabomba ya maji (plumbing). Nilitumia shilingi 1,665,000 katika hatua ya awali ya plumbing (vifaa, ufundi).

Nikaanza pia kupiga grill. Nikalipia shilingi 1,440,000 kwa ajili ya grills (madirisha na milango miwili), hii ni kununua pamoja na kupachika magrili.

Nikalipa 2,350,100 ya mabati pia (kumbuka huko nyuma, nilishatoa 800,000 kwa ajili ya mabati, misumari ya bati pamoja na usafiri).

Nikaanza pia harakati za plasta mwezi huo huo (mwanzoni nilitaka niache matofali wazi bila plasta, ukizingatia muonekano mzuri wa tofali za mbozi nilizotumia, ila baadae nikaona nichape plasta tu).

Kwa hiyo, nikalipa 830,000 ya simenti na ufundi kwa ajili ya plasta.

Hapo hapo pia nikaanza kujenga septic tank. Nikatumia 1,588,000.

Mwezi ukaisha.

August 2018
Nililipa 262,500 kwa ajili ya mchanga, kokoto (trip moja moja), na gharama za maji na kumwagilia.
Nikalipa na 2,550,000 ya ufundi wa plaster.

September 2019
Nilinunua milango na fremu (milango mitano ya mninga na fremu zake) kwa shilingi 1,345,000 (pamoja na usafiri)-Hii milango nilinunua tunduma nakumbuka.

Pia, nikaanza harakati za kuweka Alminium, ambapo nililipa 4,098,000 kwa ajili ya aluminium windows.

Nikanunua na simenti kwa 320,000 (mifuko 20).

Kufanya wiring ndani ya nyumba (vifaa + ufundi)- 2,000,000

Pia, nikanunua tiles kwa ajili ya kuweka chumbani kwangu (master bedroom) pamoja na kwenye public bathroom and toilet 1,009,000.

Nikahamia ndani ya nyumba ikiwa imekula jumla ya shilingi 64,448,100.

Baada ya hapo nikapumzika kwa sana, maana nilikua nime exhaust most of my resources kufanikisha kuhamia tu ndani ya nyumba.

Nilihamia katika hatua hii nikiwa bado sijafanya blandering, kuweka gypsum, sijafanya skimming, pia floor ilikua rough kwa upande wa sebule, vyumba vya watoto, jikoni. Sehemu yenye tiles ni kwenye master bedroom na bafuni na toilet public tu.

Sasa hivi niko kwenye hatua ya kufanya blandering (done), jana tu fundi gypsum alikuja kupiga makadirio ya gypsum. Pia, nimeshanunua vifaa vyote vya skimming, ni fundi kuja tu na kuanza kazi.

Sijaweka mahesabu haya kwa sasa, ila nitakuja kuyaweka pia nikimaliza hatua zote hizo.

Note:
Nimeweka huu uzi ili kuwatia moyo wale wapenzi wa ghorofa simple kama mimi, ambao wanatamani pia siku moja kujenga kagorofa simple ka kuishi. Niliona watu wanatishana sana humu, nikaona niweke ushuhuda wangu pia uweze kuwanufaisha wengine.

Pia hata wale wanaotamani kujenga tu nyumba za kuishi za kawaida ambazo sio gorofa. Usisubiri uwe na milioni au milioni 10 kuanza ujenzi, anza na ulicho nacho.

Cc Delight (aliomba nimtag nikileta hui uzi)
picha?
 
Wengi wanajenga maghorofa.

Sijaona mtu aliyeleta hesabu kwa detail kama kwenye uzi huu.

Kuna wengine wanafaidika kwa kuangalia gharama.

Hilo nalo hujaliona?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ataonaje hilo na roho yake imejaa wivu na kijiba?

Kuna watu wanadhani wakichukia na kuponda mambo waliofanya wenzao itawasaidia wao.
Ndio maana watu wengi hawapendi ku share details za aina hii, maana watu wenye vijiba vya aina hii wataanza kukandia na kuponda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu unajenga ghorofa bila mkandarasi aliyeizinishwa na bodi ya wakandarasi
Mkandarasi alikua anakuja kukagua ubora kila baada ya hatua fulani na kushauri. Pia, kuna hatua za muhimu mfano kumwaga zege (la chini,katikati na la juu) ambazo pia alikua anakwepo. Halafu nilikua namlipa kama "per diem" kwa siku hizo ambazo anakwepo.
Cost zake zimejumuishwa kwenye ufundi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom