Ushuhuda: Jinsi ninavyojenga nyumba ya ndoto yangu

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
2,858
7,846
Habari wana JF.

Niliwahi kuahidi kule kwenye uzi wa ujenzi wa nyumba kuwa nitaleta ushuhuda wangu wa ujenzi kwa project ambayo bado naiendeleza ya ujenzi wa nyumba ya kuishi ambayo ni ghorofa moja.

A simple house; ghorofani ni chumba kimoja tu, master bedroom, chini kuna vyumba vitatu vya kulala, sebule, jiko, dinning, store na public toilet and bathroom. Hii nyumba iko Mbeya Mjini, sitaweka picha ili ku mantain anonymity. Source ya hizi taarifa zote ni notebook yangu ambayo nilijitahidi sana kuandika kila senti ninayotumia katika ujenzi huu.

Nilianza ujenzi rasmi tarehe 04/02/2017 nikiwa na jumla ya shilingi 6,000,000.

Matumizi ya kwanza kabisa yalikua jumla ya shilingi 2,218,000 kwa ajili ya maandalizi ya msingi kwa mchanganuo huu;

230,000-Kusafisha kiwanja
850,000-Mawe trip 10
43,500-Koleo,jembe na kamba
500,000-Advance labor charge ya fundi kujenga msingi
20,000-Makarai
150,000-Mchanga trip 1
170,000-Kokoto trip 1 (mende)
15,000-Mbao.
60,000-kuchimba kisima
40,000-Mbao.
Kibali-170,000

March 2017
Nikatoa tena Tshs 1,460,500 kwa ajili ya :Maji ya ujenzi, advance ya fundi,mchanga trip 1,simenti mifuko 20,nondo lola 20, ring beam 5,waya za kusukia 2, na misumari kg 1, mbao (1*10), misumari nchi 1 kg 4.

Nikatumia tena 370,000 kwa ajili ya advance ya fundi na mbao.

Nikatumia tena 1,232,000 kununua: simenti mifuko 34, nondo lola 19, ring beam 23, binding wire 12, misumari kg 3.

Nikatumia tena 498,0000 kununua kokoto, advance ya ufundi, maji,simenti mifuko 12, nondo lola 2.

Nikatoa tena 1,120,000 kununua: Mawe trip 3, kokoto trip 1 (mende), mchanga trip 1, na advance ya fundi.

Nikafunga mwezi wa tatu kwa kutumiaTshs 787,500 kununua Mbao za kuweka kwenye nguzo, mchanga,kokoto (mende) na kukata pamoja na kuranda mbao.

Hii ilikua ni hatua ya kumwaga zege la chini (kufunga mkanda wa chini). na kupandisha nguzo.

Nikavuta pumzi kwanza.

May 2017
Nikafungua mwezi kwa kutumia 651,000 kwenye kokoto, kumalizia hela ya ufundi ya kumwaga jamvi, na maji ya kumwagilia jamvi, pamoja na kununua mifuko 10 ya saruji (simenti)

Nikatoa 2,380,000 kununua matofali (nimetumia matofali ya kuchoma ya Mbozi-ni vitofali fulani vidogo, imara na vina mwonekano wa kupendeza sana).

Nikalipa 1,820,000 kwa ajili ya: Ufundi wa kupandisha boma,kununua damping membrane,chekecheo,mchanga,maji,na simenti mifuko 10.

Nikalipa tena 1,540,000 kwa ajili ya ufundi,mabanzi, mchanga,simenti mifuko 10, kuchekecha mchanga na maji.

June 2017
Nilitumia 1,000,000 kwa ajili ya malipo ya fundi na kununua simenti, nondo, kokoto, mchanga.

Mwezi ukaisha.

July 2017
Mwezi huu kazi ya kupiga jamvi la juu ilifanyika
nilitumia 2,365,000 kwa ajili ya kulipa hela ya ufundi (jamvi la juu), simenti, nondo, mbao, mirunda.

Nikalipa tena 1,522,500 kwa ajili ya misumari, ufundi,bao.

Tukafunga mwezi.

August 2017
Nikaanza mwezi kwa kulipa 1,660,000 ya ufundi, misumari kg 10, nondo lola 40, na milunda.

Nikalipa tena 1,065,000 ya fundi na maji.

Mwezi wa nane ukaisha.

September 2017
Nililipa 2,900,000 ya malipo ya fundi pamoja na mifuko 50 ya simenti.

Mwezi ukaisha.

November 2017
Nililipa 1,552,500 kuongeza matofali (ya kuchoma ya mbozi), pamoja na malipo ya ufundi.

Nikalipa tena 1,183,000 kwa ajili ya mchanga trip 1, misumari, mbao, maji, nondo, simenti.

Mwezi Novemba ukaisha kihivyo.

December 2017
Nililipa 3,705,500 kwa ajili ya ufundi, mchanga lori 2, Matofali (ya mbozi) 2,750, ikiwa ni pamoja na gharama za kusafirisha.

Nikafunga mwaka.

Nilifunga mwaka 2017 nikiwa nimetumia jumla ya shilingi 37,034,500 katika project hii ya Ujenzi.

Jan 2018

Nikafungua mwaka kwa kutumia 2,688,000 kwa ajili ya kununua mbao, kuranda mbao, milunda hard board pamoja na malipo ya ufundi.

Feb 2018
Nilitumia 1,037,500 kwa ajili ya malipo ya fundi na kununua milunda.

Hadi kufika hapa nikawa nimemaliza kupandisha boma na kufunga lenta.

Ikaanza kazi ya kumwaga zege la juu gorofani kabisa; Nilichagua style ya kuweka zege juu ya gorofa badala ya kupaua kwa bati.

Mwezi huu wa Feb pia nilianza kuwekeza kiwanda cha bati kwa kulipia shilingi 800,000; Kwani kuna sehemu zile ambazo hazina gorofa kwa juu, niliplan kupaua kwa bati.

Nikatumia tena 2,061,000 kwa ajili ya kununua kokoto (lori 2), ufundi kwa ajili ya zege la juu, simenti mifuko 50 kwa ajili ya zege la juu pia, maji, mashine ya kushindilia zege, PVC pipes, conduit pipe na round box (hivi ni vifaa vya umeme ambavyo vilihitajika kulazwa kabla zege halijamwagwa), pamoja na hela ya ufundi wa fundi umeme.

Nikawa nimefunga mwezi.

Baada ya hii shughuli, nikavuta pumzi kubwa.

July 2018
Baada ya kuvuta pumzi miezi mitano, shughuli ikaanza tena.

Mwezi huu ndio nilianza heka heka za kupaua.
Nilitumia shilingi 1,370,000 kwa ajili ya kununua mbao, misumari, pamoja na advance ya ufundi wa fundi wa kupaua.

Hapo hapo pia nikaanza shughuli ya kutandaza mabomba ya maji (plumbing). Nilitumia shilingi 1,665,000 katika hatua ya awali ya plumbing (vifaa, ufundi).

Nikaanza pia kupiga grill. Nikalipia shilingi 1,440,000 kwa ajili ya grills (madirisha na milango miwili), hii ni kununua pamoja na kupachika magrili.

Nikalipa 2,350,100 ya mabati pia (kumbuka huko nyuma, nilishatoa 800,000 kwa ajili ya mabati, misumari ya bati pamoja na usafiri).

Nikaanza pia harakati za plasta mwezi huo huo (mwanzoni nilitaka niache matofali wazi bila plasta, ukizingatia muonekano mzuri wa tofali za mbozi nilizotumia, ila baadae nikaona nichape plasta tu).

Kwa hiyo, nikalipa 830,000 ya simenti na ufundi kwa ajili ya plasta.

Hapo hapo pia nikaanza kujenga septic tank. Nikatumia 1,588,000.

Mwezi ukaisha.

August 2018
Nililipa 262,500 kwa ajili ya mchanga, kokoto (trip moja moja), na gharama za maji na kumwagilia.
Nikalipa na 2,550,000 ya ufundi wa plaster.

September 2019
Nilinunua milango na fremu (milango mitano ya mninga na fremu zake) kwa shilingi 1,345,000 (pamoja na usafiri)-Hii milango nilinunua tunduma nakumbuka.

Pia, nikaanza harakati za kuweka Alminium, ambapo nililipa 4,098,000 kwa ajili ya aluminium windows.

Nikanunua na simenti kwa 320,000 (mifuko 20).

Kufanya wiring ndani ya nyumba (vifaa + ufundi)- 2,000,000

Pia, nikanunua tiles kwa ajili ya kuweka chumbani kwangu (master bedroom) pamoja na kwenye public bathroom and toilet 1,009,000.

Nikahamia ndani ya nyumba ikiwa imekula jumla ya shilingi 64,448,100.

Baada ya hapo nikapumzika kwa sana, maana nilikua nime exhaust most of my resources kufanikisha kuhamia tu ndani ya nyumba.

Nilihamia katika hatua hii nikiwa bado sijafanya blandering, kuweka gypsum, sijafanya skimming, pia floor ilikua rough kwa upande wa sebule, vyumba vya watoto, jikoni. Sehemu yenye tiles ni kwenye master bedroom na bafuni na toilet public tu.

Sasa hivi niko kwenye hatua ya kufanya blandering (done), jana tu fundi gypsum alikuja kupiga makadirio ya gypsum. Pia, nimeshanunua vifaa vyote vya skimming, ni fundi kuja tu na kuanza kazi.

Sijaweka mahesabu haya kwa sasa, ila nitakuja kuyaweka pia nikimaliza hatua zote hizo.

Note:
Nimeweka huu uzi ili kuwatia moyo wale wapenzi wa ghorofa simple kama mimi, ambao wanatamani pia siku moja kujenga kagorofa simple ka kuishi. Niliona watu wanatishana sana humu, nikaona niweke ushuhuda wangu pia uweze kuwanufaisha wengine.

Pia hata wale wanaotamani kujenga tu nyumba za kuishi za kawaida ambazo sio gorofa. Usisubiri uwe na milioni au milioni 10 kuanza ujenzi, anza na ulicho nacho.

Cc Delight (aliomba nimtag nikileta hui uzi)

10/04/2020
UPDATE
Nimeona niuendeleze huu uzi, nimefanya maendeleo zaidi kwa kuweka gypsum ndani (hatua ya kwanza)....
Pia, kulikuwa na maombi ya watu wengi kuwa niweke picha... Nimeona niweke baadhi ya picha za ndani na chache za nje; Naona wengine walifikia hatua hadi ya kudhani kuwa ni uzushi....
Anyways, lengo langu ni kuwapa moyo wapambanaji humu ndani wenye ndoto, msikate tamaa... It is not over so long as bado unapumua.
Michael Mkwanzania troublemaker Joowzey copernicucci98
Sky Eclat
 
Aisee hongera sanaa mzee kwa kujitahidi kujenga "kakibanda" kako.

Ila kwa mishahara minono mnayolipana huko yuueni🙄 sishangai ulivyoweza kujenga fasta fasta namba hiyo!!

Anyway,hongera tena kwa Mara nyingine clap clap👏👏
 
Dr. Wansegamila,

Hongera sana mkuu.

Conclusion yangu ni moja siku zote. Mipango huanzia kichwani mwa mtu. Kuna ambaye angeweza kufikia hatua hiyo kwa zaidi ya 200m.. Kuna mwingine 300m.

Ungeamua kupitia mlengo wa kuezeka kwa vigae vya Nabaki Africa.. (Mbao za kuezeka vigae ni nyingi, kigae kimoja ni zaidi ya 23,000/= na pengine ungehitaji zaidi ya 600, na vile vikolokolo vyake vingine); ukiamua kutumia spanish tiles, ungeamua kujenga nyumba ya mawe tupu, ungeamua kusema ratio yangu ya cement kwa mchanga nataka iwe kali sana... Definately gharama zingeongezeka mara dufu.

So kila mtu apange kichwani mwake anachohitaji.

Tunashukuru sana kwa ushuhuda wako na kututia moyo.
 
Back
Top Bottom