USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar...

USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar...

Status
Not open for further replies.
Nmeikuta ofisini kwa Rais asubuhi ya jana

Naamin Mzee keshaanza kuifanyia kazi thread hii

Asante sana mtoa uzi

Na wengine wenye critic stories & evidences kama hizi, karibuni sana tujenge nchi
 
Mfumo wa usalama wa Taifa, hasa wa uajiri inabidi ufumuliwe na uundwe upya. Kwa mfumo wa sasa, wanaojiunga na TISS ni watoto mabosi wa Askari Polisi, Magereza, Uhamiaji, Wanajeshi na TISS wenyewe. Wakikutana katika vikao vyao vya ulinzi na usalama wilaya/mkoa ndiko hupeana hayo mapande. Ni nadra kwa mtoto wa maskini asiye na jina serikalini kuajiliwa na hicho kitengo. Ni watoto wa wakubwa tu. Kwa mfumo wa namna hiyo kuwajibishana inakuwa ngumu sana maana kila mtu anakuwa na Godfather wake wa kumlinda.

Kwa maslahi yetu wote na taifa kwa ujumla, nafasi za utumishi TISS zitangazwe ili watu wote waombe na mabo mengine yaanzie hapo. Angalau kuwe na uwazi, japo kidogo. Kuna kazi za kitaaluma ambazo hazihitaji afisa kuonana na watu, mfano mtaalamu wa mawasiliano, huyu anaweza kuwa IT professional yeyote na haihitaji usiri katika kumpata mtu wa namna hiyo. Tunaweza tukaelewa kama wakusanya inteligensia wanapatikana kwa usiri, lakini haileti maana kwa professionals wengine kuwa siri.

Pili, TISS iwajibike kwa kamati ya ulinzi na usalama ya bunge. Kamati iwe na haki ya kuwahoji wakuu wa TISS kuhusiana na mambo mbalimbali yahusuyo majukumu yao. Mkurugenzi wa usalama wa Taifa aidhinishwe na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge. Iwe hivyo hivyo kwa wakuu wengine wa vyombo vya usalama.

Wakati tunalilia mabadiliko hayo, tunatambua TISS imewahi kuwa ktk kiwango cha juu cha utendaji-hasa wakati wa harakati za ukombozi wa bara la Afrika na tunawapongeza kwa hilo. Lakini ktk zama hizi za vyama vingi, wameacha weledi wamekuwa kama polisi wetu wanavyotuzingua mtaani. Wamekuwa mwiba mkali kwa wapinzani wa CCM. CCM sio Taifa.
 
Mfumo wa usalama wa Taifa, hasa wa uajiri inabidi ufumuliwe na uundwe upya. Kwa mfumo wa sasa, wanaojiunga na TISS ni watoto wa Askari Polisi, Magereza, Uhamiaji, Wanajeshi na TISS wenyewe. Wakikutana katika vikao vyao vya ulinzi na usalama wilaya/mkoa ndiko hupeana hayo mapande. Ni nadra kwa mtoto wa maskini asiye na jina serikalini kuajiliwa na hicho kitengo. Ni watoto wa wakubwa tu. Kwa mfumo wa namna hiyo kuwajibishana inakuwa ngumu sana maana kila mtu anakuwa na Godfather wake wa kumlinda.

Kwa maslahi yetu wote na taifa kwa ujumla, nafasi za utumishi TISS zitangazwe ili watu wote waombe na mabo mengine yaanzie hapo. Angalau kuwe na uwazi, japo kidogo. Kuna kazi za kitaaluma ambazo hazihitaji afisa kuonana na watu, mfano mtaalamu wa mawasiliano, huyu anaweza kuwa IT professional yeyote na haihitaji usiri katika kumpata mtu wa namna hiyo. Tunaweza tukaelewa kama wakusanya inteligensia wanapatikana kwa usiri, lakini haileti maana kwa professionals wengine kuwa siri.

Pili, TISS iwajibike kwa kamati ya ulinzi na usalama ya bunge. Kamati iwe na haki ya kuwahoji wakuu wa TISS kuhusiana na mambo mbalimbali yahusuyo majukumu yao. Mkurugenzi wa usalama wa Taifa aidhinishwe na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge. Iwe hivyo hivyo kwa wakuu wengine wa vyombo vya usalama.

Wakati tunalilia mabadiliko hayo, tunatambua TISS imewahi kuwa ktk kiwango cha juu cha utendaji-hasa wakati wa harakati za ukombozi wa bara la Afrika na tunawapongeza kwa hilo. Lakini ktk zama hizi za vyama vingi, wameacha weledi wamekuwa kama polisi wetu wanavyotuzingua mtaani. Wamekuwa mwiba mkali kwa wapinzani wa CCM. CCM sio Taifa.
Siyo kosa lako kufikiria usiyoyajua,kwa taarifa yako wale jamaa hawako hivyo ufikiriavyo wewe
 
Siyo kosa lako kufikiria usiyoyajua,kwa taarifa yako wale jamaa hawako hivyo ufikiriavyo wewe
Kama unataka kuwatetea wewe watetee tu, lakini niliyoyaandika hapa ni kutokana na first-hand experience. Tatizo la maafisa wetu wa usalama hawapendi kukosolewa. Wote tunajua wao wangekuwa makini haya yote yasingetokea. Jiulize kwanini walimshughulikia Ulimboka, lakini wanaohujumu uchumi Bandarini wanawachekea. Ni kwasababu wanakula nao.

Wangekuwa makini, wangekuwa na black ops kwa ajili ya kazi hiyo tu. Mtu anayehujumu uchumi wa nchi anapotezwa. Lakini sasa wanaoneana aibu kwakuwa maofisa watoto wa wakubwa ndo wanapelekwa vitengo 'vinono' kama bandari ambako wanapiga hela na hakuna wa kuuliza maswali.
 
Ukisema ukweli hakuna wanachofanya napingana na wewe kwa asilimia elfu,kwanza wapongeze maana hata mtt akizaliwa kuna hatua zake mpaka kutembea,hapa viongozi wetu walipoanzia ni pazuri maana wanachfanya kinaonekana na watanzania wote,sijui wewe ndugu kwa nini unasema amna wanachofanya?
Vipi mangimeli, umenielewa lakini?
 
mleta mada kaka yako kufukuzwa uhasibu mkuu pale OILCOM unakazi ya kusambaza umbea huku mtandaon watanzania wajinga wanakupigia makofi bila kujiridhisha na ulichokitunga ksho ntaweka hapa mikataba ya mauzo kati ya OILCOM na SONGASGAS na ntakuabisha
 
NIMEZOEA KU COPY NA KU PEST HABARI LAKINI HII NAKAMATIKA LABDA N MM NINGEKUWA INVISIBLE
 
KUMEKUWA NA UMILIKI WA KUWEKWA KWENYE HAYA MAKAMPUNI, Ya kwamba kabuni ni mali mali ya bwana X lakini Memorandum of association na ducument zote zinasema wamiliki waarabu..
hapa ndipo msingi mkubwa wa kwanini makampuni yanafanya madudu ya ajabu lakini tunaendelea kuona yakifubmiwa macho tuu
 
Yaani ni aibu kubwa, hao watu tunawarembea sana, inabidi mtu akibainika, hakuna kumuonea huruma, unanyonga mpaka anafariki, ukifanya hivyo kwa watu watatu tu, hawatochezea mali ya umma, shenzi sana....
 
Tanzania MAADILI YAMEPOROMOKA SANA,Yaani KILA MTU ANATAKA KUIBAIBA TUUUUUUUUUUUU,WIZIIIII,UJANJAUJANJA MWINGIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII
 
Mfumo wa usalama wa Taifa, hasa wa uajiri inabidi ufumuliwe na uundwe upya. Kwa mfumo wa sasa, wanaojiunga na TISS ni watoto mabosi wa Askari Polisi, Magereza, Uhamiaji, Wanajeshi na TISS wenyewe. Wakikutana katika vikao vyao vya ulinzi na usalama wilaya/mkoa ndiko hupeana hayo mapande. Ni nadra kwa mtoto wa maskini asiye na jina serikalini kuajiliwa na hicho kitengo. Ni watoto wa wakubwa tu. Kwa mfumo wa namna hiyo kuwajibishana inakuwa ngumu sana maana kila mtu anakuwa na Godfather wake wa kumlinda.

Kwa maslahi yetu wote na taifa kwa ujumla, nafasi za utumishi TISS zitangazwe ili watu wote waombe na mabo mengine yaanzie hapo. Angalau kuwe na uwazi, japo kidogo. Kuna kazi za kitaaluma ambazo hazihitaji afisa kuonana na watu, mfano mtaalamu wa mawasiliano, huyu anaweza kuwa IT professional yeyote na haihitaji usiri katika kumpata mtu wa namna hiyo. Tunaweza tukaelewa kama wakusanya inteligensia wanapatikana kwa usiri, lakini haileti maana kwa professionals wengine kuwa siri.

Pili, TISS iwajibike kwa kamati ya ulinzi na usalama ya bunge. Kamati iwe na haki ya kuwahoji wakuu wa TISS kuhusiana na mambo mbalimbali yahusuyo majukumu yao. Mkurugenzi wa usalama wa Taifa aidhinishwe na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge. Iwe hivyo hivyo kwa wakuu wengine wa vyombo vya usalama.

Wakati tunalilia mabadiliko hayo, tunatambua TISS imewahi kuwa ktk kiwango cha juu cha utendaji-hasa wakati wa harakati za ukombozi wa bara la Afrika na tunawapongeza kwa hilo. Lakini ktk zama hizi za vyama vingi, wameacha weledi wamekuwa kama polisi wetu wanavyotuzingua mtaani. Wamekuwa mwiba mkali kwa wapinzani wa CCM. CCM sio Taifa.
Una uhakika..??? Hujui unenalo
 
Halafu swala jingine inaonekana kuna vitu huvijui vizuri as per TBS requirement for Diesel au Gasoil inayotakiwa ni low sulpher 500 ppm na sio hiyo uliyoitaja na ilianza kutumika January 2015 before hapo tulikuwa tunatumia 50ppm. Mafuta yote yanayoingia nchini yanakuja kwa Bulk supply na kusimamiwa na PIC zamani sasa ni PBPA as government agency ambazo tangu waanze kuleta mafuta hakuna meli iliyoleta mafuta 150 KT haijawah kutokea na unatakiwa kufahamu delivery zinakuwa tano(sawa na meli nne mpka tano kulingana na mahitaji ya mwezi huo) kwa supply ya mwez mmoja meli za Gasoil au diesel 2 zenye uwezo wa kubeba 70 KT to 100 KT na hizi zote hushushia SPM ambayo ipo deep sea na KOJ hushusha Motor Spirit Premium/Unleaded petroleum/Petrol na Jet A1/IK na meli inayobeba Jet A1 huwa inakuwa Comb of Either petrol and Jet A1 au Gasoil & Jet A1 na meli hizo hazizidi kwa product zote 30KT to 38KT. As per shipping and supply contract.
Huu ni utetezi pia wenye nguvu.. kama mtoa mada au yeyote mwenye ushawishi mbadala amjibu huyu mtoa hoja.. pia napata shida kidogo, muanzisha mada hajazungumza ni mwaka gani hasa sakata hilo lilitokea. Ila tujue kama ni kabla ya kuanzishwa kwa bulk procurement system au baada
 
mkuu nitakupa namba ya simu au email ya Mh. Rais ili umfafanulie vizuri na kwa lugha rahisi zaidi ili ajue pa kuanzia.

Asante.

Mkuu nadhani kwakuwa rais alisoma kemia, na kwa kuwa lugha ya mtoa mada ni ya kikemia, sina shaka Magufuli ataelewa. Kikubwa tumuombe Magufuli atumbue majipu hayo haraka.
 
Ulinzi unahitajika kwa mzalendo huyu,wasisubiri mpaka wamtulize Kwa vitendo maana wameanza na maneno(vitisho)
 
ndio maana humu hakuna wauza sura asee, ingekua insta au facebook ningejuaje
ebana mimi pia naapriciate sn jf mana akuna usharabaro umu wakuuza sura yani wajuzi wasomi wwnye vipaji wenye uwezo wa kudadavua mambo mbalimbali watu wwnye utu wooote wapo umu
 
Uzi mrefu but sijutii kuusoma wote na kuna kitu kinaingia akilini yaani nchi hii kuna watu unaweza kuwapiga risasi akisha kufa ndo unawauliza maswali.Hili suala la kutokuwa waadilifu watu wa nyanja hizo linajulikana ila watu wengi hatukujua ni kwa kiasi hiki!
Kweli kula nchi sio kulamba udongo kuna watu wanaishi maisha ya kifahari kwa mali zetu.
 
Wazalendo wako wengi nchi hii, lakini tatizo liko kwenye mambo ya itikadi tuu. Mfano mleta mada akijulikana itikadi yake iko tofauti na chama tawala basi hata ushauri wake utatupwa kule kwani ataonekana sio mzalendo.
Wanachosahau ni kuwa hao wakina Masamaki ndio wana pea hata kumi za mashati ya kijani na kwenye michango ya kujenga chama wanatoa mamilioni
Kwa taarifa yako Masamaki ni CHADOMO mzuri tuu hata mamvi kamsaport sana tuu
 
Tusitegemee miujiza hapa kama tuna vyama tawala ambavyo vinategemea kuomba hela kwa watu kama hawa ili vikaonge wapiga kura.
Hivi mmesahau ya Dodoma ya Watanzania kutaka kununuliwa viongozi na Wageni?.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom