USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar...

Status
Not open for further replies.
Hii inchi hii ya ajabu sana yani mtu katoa tarifa kama hivi baada ya polisi kumkamata mlalamikaji aliyeenda kusemwa kazushiwa ili upelelezi ukamilike wanafuatwa jamii forum uwwi twafwaa
 
Mkuu Fuhrer nakupigia saluti. Hizi ndizo habari. Fanya juu chini zimfikie Mkulu
 
Mkuu Ambamba kama kweli una contact za Mkulu mpatie Fuhrer awasiliane naye
 
Ok kwenye kuibiwa nimeelewa bado hapa kwenye kuchakata gesi sijakusoma, nilivyoaminishwa ni kwamba gas tunayopikia majumbani kwenye mitungi ni LPG imported kwamba hatuna mitambo ya kichakata kua LPG sasa hapa kwenye post yako nimeona gas kuchakatwa plz fafanua kiongozi.
 
Duuh kumbe hii ndio posti iliyosababisha wakurugenzi wa JF wafunguliwe kesi?
Kweli hatutaendelea mtu anatoa taarifa nyeti kwa manufaa ya taifa anaonekana mhalifu?
 
Tufanyie uchunguzi nchi nzima Mali zilizopatikana kwa wizi zitaifishwe.
tuwaajiri kampuni ya ushauri toka UK watufanyie uchunguzi kwenye sekta mzima ya gesi na mafuta kubaini njia zote za wizi ikiwemo tenda zote .
Tanzania imeshaipita Nigeria kwa wizi na utapeli.
wale wote wanaotumia ofisi zao kuibia nchi wafungwe maisha.
 
Rais na Waziri wake mkuu watapata kazi sana kusafisha hii nchi,Ningewashauri kitu kimoja kama kweli wanataka kusafisha nchi hii na siyo "kuonekana wanasafisha" wakati ukweli hakuna kitu wanachofanya.

Wapo watu katika nchi hii wanazo taarifa za mifumo ya wizi katika sehemu mbalimbali jinsi inavyofanya kazi, either wao walishiriki na sasa hawapo kwenye hiyo mirija au wanashuhudia jinsi wizi unavyoendelea ingawa wao hawausiki. Rais angetengeneza utaratibu wa watu wema wenye taarifa ya madudu yanayofanyika katika taifa hili kupeleka hizo taarifa in details wakiwa wanajulikana au hawajulikani, iwe ni choice ya mtoa taarifa.

Nina uhakika wapo watu wangejitokeza kutoa hizo taarifa nikiwapo mimi.

Mimi nina uzoefu wa jinsi mafuta yanavyoibiwa bandarini:

Kwanza niweke wazi, mafuta hayaibiwi bandarini kwa kukadiria au sijui kwa sababu ya flow meters. Hakuna kitu kama hicho. Tena zile flow meter zilikuwa na capacity ndogo na zinaharibika mara kwa mara hivyo zikiharibika inabidi ku-bypass. Meli ikiwa inashusha mafuta inaweza kushusha kwa presha ya bar 16, zile flow meter zilikuwa hazihimili presha kubwa.

Mafuta yakishashushwa, kiwango cha mafuta kilichopokelewa kina pigiwa hesabu na ma-surveyor na wanatengeneza taarifa yao. Mchezo unaanzia hapo TRA, Mafuta yanayotakiwa kulipiwa ushuru ni ya local (yanayotumika humu nchini), na ya transit hayalipiwi ushuru. Sasa figure zinazoingizwa kwenye system ya TRA kwa ajili ya kulipiwa ushuru ndiyo hapo serikali inapoibiwa.

Na anayefanya mchezo huu ni afisa wa TRA kitengo cha mafuta akishirikiana na kampuni husika. Kuna makampuni ambayo yamekubuhu kwa mchezo huo. Makampuni ya watu binafsi yakiongozwa na yanayomilikiwa na waarabu. OILCOM ndio kinara, Lake oil, World oil, CAMEL Oil, etc.

Ipo mifano mingi ila natoa mmoja.

Kuna siku ilikuwa meli na mzigo mkubwa tu kana tani laki moja na nusu, Huo mzigo ulikuwa wa OILCOM. Kwenye Cargo manifesto ya meli ulikuwa umekuwa declared kama JET A1, (mafuta ya ndege) ya transit ya kwenda Zambia. Haya yana tax exemption.

Surveyor wa mzigo alikuwa kijana mmoja anaitwa ANDERSON kutoka Intertek. Akaenda kwenye meli akapima mzigo akaambiwa na wenye mzigo kuwa aandike kuwa ni JET A1 kwenye documents zake, ingawa mzigo ulikuwa ni diesel (GO), akaahidiwa dili ikishakamilika atapewa chake. Basi Anderson machale yakamcheza akaamua kutengeneza ducument set 2, moja akadiclare ule mzigo kuwa ni JET na nyingine kuwa ni GO.

Sasa kosa ambalo walilifanya hawakumuhusisha loading master wa pale manifold. Alipoambiwa afungue line ya kwenda oilcom, Yule mzee akafungua line ya JET ya kwenda OIL com. Sasa pale KOJ manifold kuna chujio za mafuta (Strainers) kwa ajili ya kila aina ya mafuta, na zina ukubwa tofauti kwaajili ya kuchuja mafuta. Mafuta yalipoanza kusukumwa, ile strainer ya JET ikaanza kupiga kelele yaani ikawa inapitisha mafuta kwa tabu.

Loading master akaamua kuangalia kwa nini inapiga kelele, akakuta mafuta yanayopita ni diesel tena ile diesel ya high sulphur (5000ppm). Akaita kwenye radio call, " We Anderson, hiyo mnayosukuma ni JET au DIESEL?", Hakuna mtu aliyejibu kenye radio, ikabidi pump za meli zizimwe washuke kwenye meli kwenda kuongea na loading master.

Sasa ile channel ya radio inayotumiwa kwa mawasiliano inasikiwa na watu wengi wakiwemo TRA, Usalama wa Taifa, Maofisa wa Bandari, n.k, baada ya kama nusu saa, watu zaidi ya 9 wakawa wamefika pale KOJ, wakiwemo maafisa wa usalama wa Taifa.

Kuona hivyo Underson akatoka na gari akakimbia, akamwacha Depot supervisor wa OILCOM, yule kijana wa oilcom ikabidi amtaarifu mzee ISLAM mwenyewe mwenye OILCOM kuwa kimesanuka. Ilikuwa ni Jumamosi, mzee Islam akaagiza watu wote walioenda kushuhudia ile saga waende OILcom, inavyosemekana kila mtu alipewa mil 80 cash palepale kwenye mifuko ya rambo. Na mzigo baadae ukashushwa kwenye line ya diesel.

Sasa ukiangalia wizi unaofanyika kwenye mafuta siyo wizi wa mafuta ila ni ukwepaji kodi, mafuta yanakuwa declared kama transit hayalipiwi ushuru ila yanauzwa local kwa bei ile ile. Na biashara hii ya kukwepa ushuru ilikuwa inasimamiwa na mwenyewe kamishna wa kodi ya forodha Bwana Masamaki.

Mafuta yakishaingiza kama transit yanatengenezewa document zote kuanzia za loading, Checkpoint zote za TRA, clearance ya Tunduma hadi upande wa pili wa boarder, na offloading documents na documents za ZRA(Zambia Revenue Authority). Na Bond clearance.

Hizi taarifa zote Usalama wa taifa wanazijua fika, kama Magufuli akitaka kusafisha, anatakiwa apate watu wa usalama wenye mtazamo kama wake. Laa sivyo, na wao watakuwa wanawashtua waalifu kwa meseji kama prof. Muhongo.

OIL COM ndio kinara.

Juzi nimefungua uzi wenye kichwa cha habari, "USHUHUDA: Jinsi kampuni za mafuta zinavyokwepa ushuru" nikatoa mfano mmoja wa kampuni ya OILCOM inavyokwepa ushuru. Kuna watu wameni-inbox vitisho.

Sasa natoa mfano mwingine wa OILCOM hiyohiyo.

Baada ya gas ya songosongo kuanza kuchakatwa ( Gas processing). Kampuni ya OILCOM ilipata tender ya kununua Naptha ambayo ni byproduct ya gas processing. Hii naptha ni mojawapo ya condensate katika Natural Gas Liquids (NGL) ambazo huwa zina-liquify katika surface separator. Kwa wasioijua hii Naptha ni ile thinner inayotumika kuchanganyia rangi. Sasa hii naptha inatumika katika viwandani kutengenezea Rangi. Sasa OILCOM ndio Dealer mkubwa wa hiyo naptha pale songosongo. Huwa anapeleka meli pale songosongo na kupakia mzigo wa kutosha na kuja kuushusha kwenye depot yake pale kurasini. Kwa mkataba wake OILCOM ni kwamba anaiuza kwenye viwanda vya rangi vya hapa nchini na nyingine ana-export nje ya nchi.

Anachokifanya kwenye depot yake pale kurasini ni kui-blend na Petrol (PMS) kwa ratio nzuri na kuongeza na octane boosters ili afikie viwango vinavyohitajika vya AKI (Anti Knocking Index) na anatuuzia kwenye service station zake kama petrol.
Parameter anayoi-monitor kwenye hii petrol anayotu-blendia ni hiyo OCTANE number tu kwa sababu anajua kuwa akikosea hiyo atauwa injini za magari yote yanayotumia petrol na effect yake watu wataiona immediately wakijaza kwenye station zake.

Parameter nyingine kama oxygen content na vapour pressure hashuguliki nazo kwa kuwa effect zake zipo kwenye ulaji wa mafuta wa injini na kutoa moshi. (Effects of low and high oxygen content)
Hii petrol yenye naptha ya songosongo tumeuziwa kwa muda mrefu sana na wakuu wanajua kuanzia ewura hadi TRA. Yupo afisa mmoja wa TRA wa kitengo cha mafuta ambaye alikuwa ndio kama Resident custom officer pale oilcom anaitwa GEORGE, yeye ndio alikuwa kiunganishi wa OILCOM kwenye haya magumashi
Ni hatar
 
Taarifa kama hizi husaidia kufichua maovu. Lakini kwetu sisi ndio kwanza unaonekana adui namba moja.
 
Dah sikupata kuusoma huu uzi toka mwaka jana ila kama madudu yenyewe ni haya lazma watu waajibishwe kwakweli na huu ndo uzalendo unaohitajika sio baadhi ya maofisa wa polisi kutaka kumkamata mtoa taarifa.
 
FUHRER una information nyingi kupita hata hizo.Nilicho jifunza inaonekana wapiga dili wakati wanapiga dili zao watu wanawaona na wanajua ila migao hawatoi kwa wote, wanakula wenyewe. Au ww pia kama ulivyo sema kuwa kuna watu waliokuwa wanashiriki awali kwa sasa wameacha sasa watu kama nyie ndio wakuwatumia kujua mbinu.

Hata mm najua mengi ila kwa kesi hii ya JF kuhusu faragha inafanya nizidi kuogopa kutoa info kama rais akaamua kusaidia website kama hizi zisifungiwe bali ziwe na jukwaa la kutoa taarifa kama hizi then zikafanyiwa uchunguzi bila ya kupendelea then tungefika mbali zaidi.

Hata hao usalama wa taifa bila ya raia kama sisi hawawezi, na itakuwa vigumu sana hasa kwa kesi kama za ugaidi, ufisadi, uhujumu na n.k kupata taarifa kama identity ya FUHRER itajulikana na atachukuliwa hatua
 
Rais na Waziri wake mkuu watapata kazi sana kusafisha hii nchi,Ningewashauri kitu kimoja kama kweli wanataka kusafisha nchi hii na siyo "kuonekana wanasafisha" wakati ukweli hakuna kitu wanachofanya.

Wapo watu katika nchi hii wanazo taarifa za mifumo ya wizi katika sehemu mbalimbali jinsi inavyofanya kazi, either wao walishiriki na sasa hawapo kwenye hiyo mirija au wanashuhudia jinsi wizi unavyoendelea ingawa wao hawausiki. Rais angetengeneza utaratibu wa watu wema wenye taarifa ya madudu yanayofanyika katika taifa hili kupeleka hizo taarifa in details wakiwa wanajulikana au hawajulikani, iwe ni choice ya mtoa taarifa.

Nina uhakika wapo watu wangejitokeza kutoa hizo taarifa nikiwapo mimi.

Mimi nina uzoefu wa jinsi mafuta yanavyoibiwa bandarini:

Kwanza niweke wazi, mafuta hayaibiwi bandarini kwa kukadiria au sijui kwa sababu ya flow meters. Hakuna kitu kama hicho. Tena zile flow meter zilikuwa na capacity ndogo na zinaharibika mara kwa mara hivyo zikiharibika inabidi ku-bypass. Meli ikiwa inashusha mafuta inaweza kushusha kwa presha ya bar 16, zile flow meter zilikuwa hazihimili presha kubwa.

Mafuta yakishashushwa, kiwango cha mafuta kilichopokelewa kina pigiwa hesabu na ma-surveyor na wanatengeneza taarifa yao. Mchezo unaanzia hapo TRA, Mafuta yanayotakiwa kulipiwa ushuru ni ya local (yanayotumika humu nchini), na ya transit hayalipiwi ushuru. Sasa figure zinazoingizwa kwenye system ya TRA kwa ajili ya kulipiwa ushuru ndiyo hapo serikali inapoibiwa.

Na anayefanya mchezo huu ni afisa wa TRA kitengo cha mafuta akishirikiana na kampuni husika. Kuna makampuni ambayo yamekubuhu kwa mchezo huo. Makampuni ya watu binafsi yakiongozwa na yanayomilikiwa na waarabu. OILCOM ndio kinara, Lake oil, World oil, CAMEL Oil, etc.

Ipo mifano mingi ila natoa mmoja.

Kuna siku ilikuwa meli na mzigo mkubwa tu kana tani laki moja na nusu, Huo mzigo ulikuwa wa OILCOM. Kwenye Cargo manifesto ya meli ulikuwa umekuwa declared kama JET A1, (mafuta ya ndege) ya transit ya kwenda Zambia. Haya yana tax exemption.

Surveyor wa mzigo alikuwa kijana mmoja anaitwa ANDERSON kutoka Intertek. Akaenda kwenye meli akapima mzigo akaambiwa na wenye mzigo kuwa aandike kuwa ni JET A1 kwenye documents zake, ingawa mzigo ulikuwa ni diesel (GO), akaahidiwa dili ikishakamilika atapewa chake. Basi Anderson machale yakamcheza akaamua kutengeneza ducument set 2, moja akadiclare ule mzigo kuwa ni JET na nyingine kuwa ni GO.

Sasa kosa ambalo walilifanya hawakumuhusisha loading master wa pale manifold. Alipoambiwa afungue line ya kwenda oilcom, Yule mzee akafungua line ya JET ya kwenda OIL com. Sasa pale KOJ manifold kuna chujio za mafuta (Strainers) kwa ajili ya kila aina ya mafuta, na zina ukubwa tofauti kwaajili ya kuchuja mafuta. Mafuta yalipoanza kusukumwa, ile strainer ya JET ikaanza kupiga kelele yaani ikawa inapitisha mafuta kwa tabu.

Loading master akaamua kuangalia kwa nini inapiga kelele, akakuta mafuta yanayopita ni diesel tena ile diesel ya high sulphur (5000ppm). Akaita kwenye radio call, " We Anderson, hiyo mnayosukuma ni JET au DIESEL?", Hakuna mtu aliyejibu kenye radio, ikabidi pump za meli zizimwe washuke kwenye meli kwenda kuongea na loading master.

Sasa ile channel ya radio inayotumiwa kwa mawasiliano inasikiwa na watu wengi wakiwemo TRA, Usalama wa Taifa, Maofisa wa Bandari, n.k, baada ya kama nusu saa, watu zaidi ya 9 wakawa wamefika pale KOJ, wakiwemo maafisa wa usalama wa Taifa.

Kuona hivyo Underson akatoka na gari akakimbia, akamwacha Depot supervisor wa OILCOM, yule kijana wa oilcom ikabidi amtaarifu mzee ISLAM mwenyewe mwenye OILCOM kuwa kimesanuka. Ilikuwa ni Jumamosi, mzee Islam akaagiza watu wote walioenda kushuhudia ile saga waende OILcom, inavyosemekana kila mtu alipewa mil 80 cash palepale kwenye mifuko ya rambo. Na mzigo baadae ukashushwa kwenye line ya diesel.

Sasa ukiangalia wizi unaofanyika kwenye mafuta siyo wizi wa mafuta ila ni ukwepaji kodi, mafuta yanakuwa declared kama transit hayalipiwi ushuru ila yanauzwa local kwa bei ile ile. Na biashara hii ya kukwepa ushuru ilikuwa inasimamiwa na mwenyewe kamishna wa kodi ya forodha Bwana Masamaki.

Mafuta yakishaingiza kama transit yanatengenezewa document zote kuanzia za loading, Checkpoint zote za TRA, clearance ya Tunduma hadi upande wa pili wa boarder, na offloading documents na documents za ZRA(Zambia Revenue Authority). Na Bond clearance.

Hizi taarifa zote Usalama wa taifa wanazijua fika, kama Magufuli akitaka kusafisha, anatakiwa apate watu wa usalama wenye mtazamo kama wake. Laa sivyo, na wao watakuwa wanawashtua waalifu kwa meseji kama prof. Muhongo.

OIL COM ndio kinara.

Juzi nimefungua uzi wenye kichwa cha habari, "USHUHUDA: Jinsi kampuni za mafuta zinavyokwepa ushuru" nikatoa mfano mmoja wa kampuni ya OILCOM inavyokwepa ushuru. Kuna watu wameni-inbox vitisho.

Sasa natoa mfano mwingine wa OILCOM hiyohiyo.

Baada ya gas ya songosongo kuanza kuchakatwa ( Gas processing). Kampuni ya OILCOM ilipata tender ya kununua Naptha ambayo ni byproduct ya gas processing. Hii naptha ni mojawapo ya condensate katika Natural Gas Liquids (NGL) ambazo huwa zina-liquify katika surface separator. Kwa wasioijua hii Naptha ni ile thinner inayotumika kuchanganyia rangi. Sasa hii naptha inatumika katika viwandani kutengenezea Rangi. Sasa OILCOM ndio Dealer mkubwa wa hiyo naptha pale songosongo. Huwa anapeleka meli pale songosongo na kupakia mzigo wa kutosha na kuja kuushusha kwenye depot yake pale kurasini. Kwa mkataba wake OILCOM ni kwamba anaiuza kwenye viwanda vya rangi vya hapa nchini na nyingine ana-export nje ya nchi.

Anachokifanya kwenye depot yake pale kurasini ni kui-blend na Petrol (PMS) kwa ratio nzuri na kuongeza na octane boosters ili afikie viwango vinavyohitajika vya AKI (Anti Knocking Index) na anatuuzia kwenye service station zake kama petrol.
Parameter anayoi-monitor kwenye hii petrol anayotu-blendia ni hiyo OCTANE number tu kwa sababu anajua kuwa akikosea hiyo atauwa injini za magari yote yanayotumia petrol na effect yake watu wataiona immediately wakijaza kwenye station zake.

Parameter nyingine kama oxygen content na vapour pressure hashuguliki nazo kwa kuwa effect zake zipo kwenye ulaji wa mafuta wa injini na kutoa moshi. (Effects of low and high oxygen content)
Hii petrol yenye naptha ya songosongo tumeuziwa kwa muda mrefu sana na wakuu wanajua kuanzia ewura hadi TRA. Yupo afisa mmoja wa TRA wa kitengo cha mafuta ambaye alikuwa ndio kama Resident custom officer pale oilcom anaitwa GEORGE, yeye ndio alikuwa kiunganishi wa OILCOM kwenye haya magumashi
CCM ni ukoo wa panya—babu mwizi, baba mwizi, watoto wezi, wajukuu wezi, vitukuu wezi, vilembwe wezi na vining’ina wezi! Ukoo huu wa panya walikuwa wanasafiri katika boti la muhogo, lakini kwa sababu ya uroho wao, walianza kulitafuna boti! Kilichofuata ni ukoo mzima wa kizazi cha panya kuzama na kuangamia.

CCM wameanza kuitafuna nchi tangu mwaka 1961 lakini ukomo wao wa kutafuna rasilimali za nchi ni mwaka 2020 kwani hakuna mtanzania mwenye hamu ya kuongozwa na chama cha kifisadi kama CCM ambacho kimeshindwa kuboresha maisha na ustawi wa watanzania. Wananchi wamechoka kubebeshwa ‘magunia ya misumari’ ya bei ya juu ya umeme, mfumuko wa bei wa kutisha, elimu duni, maisha duni, ufisadi wa kutisha, EPA na matatizo lukuki yanayosababishwa na panya (CCM) hawa wasiokuwa na haya! Kizazi kizima cha CCM kinakaribia kuzama na kusahaulika kabisa katika ardhi ya Tanzania.

It’s a matter of time before CCM dynasty comes to an end, and that’s when magambas will apprehend the significance and power of the people. Desolately, CCM have been ignoring and looking down their noses at common Tanzanians for many years. Time has now come when citizens can no longer endure CCM’s tyranny and corrupt rule. Everybody is tired of living like a slave on a land endowed with an assortment of natural wealth which only benefits minority fisadis and a few elites in power while majority Tanzanians lead very miserable lives.

What comes around goes around. Let CCM go to hell for good because they have absolutely failed to uplift the living standards of millions of Tanzanians at the expense of a few fisadis whose gargantuan stomachs never fill up! And no one should be blamed for the hatred and grudge that many Tanzanians hold against CCM and their crooked government except fisadis themselves who, horrendously, decided to gnaw the cassava-made boat by which they were sailing!
 
Tufanyie uchunguzi nchi nzima Mali zilizopatikana kwa wizi zitaifishwe.
tuwaajiri kampuni ya ushauri toka UK watufanyie uchunguzi kwenye sekta mzima ya gesi na mafuta kubaini njia zote za wizi ikiwemo tenda zote .
Tanzania imeshaipita Nigeria kwa wizi na utapeli.
wale wote wanaotumia ofisi zao kuibia nchi wafungwe maisha.

Makampuni ya kizungu ndo yanaongoza Kwa kuiba raslimali za mataifa ya afrika kama gesi, mafuta na madini. Hao jamaa ni nuksi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom