UShirikina wa Mapenzi na Wanawake

UShirikina wa Mapenzi na Wanawake

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2008
Posts
1,943
Reaction score
1,015
Ni baada ya mjadala mrefu tuliokuwanao kuhusu "Imani za Kishirikina na Mahusiano ya Kimapenzi" ndipo nilipofikia uamuzi wa kuileta mada hii hapa.

Nukuu za wachunguzi wa masuala ya mahusiano ni kuwa:

1. Wanawake wanaongoza kwenda kwa waganga kuzidi wanaume.

2. Wanawake wazuri kwa sura au umbo siku hizi ndiyo wanaongoza kwenda kwa waganga wa kienyeji ukilinganisha na wale wa kawaida.

3. Dawa zinazoongozwa kutafutwa ni; Kummiliki mpenzi, Kumrejesha mpenzi wa zamani na Kusafisha nyota ya mapenzi.

4. Hata wanawake wasomi (walioko vyuoni na wale wa makazini) wanashiriki ushirikina huu sana tu.

(Kwa lugha nyepesi ni washirikina sana)

Nilipoanza kufuatilia kiini chake ni nini, nimegundua yafuatayo:
a. Hawajiamini
b. Wanajazana ujinga kufikiri kuwa "uzuri wao" ndiyo maisha.
c. Wanashindwa kuelewa kuwa mapenzi ni zaidi ya uzuri wa umbo.
d. Wakihisi uzuri wao unapungua hufanya viroja na ni wepesi kukata tamaa (kauli zao, iwe katika utani au akimaanusha, huwa zinaakisi kilichopo mioyoni mwao)

Tafadhali nakaribisha maoni yako.
 
Ukigundua tu unasepa zako haraka sana tena bila hata kuaga.
 
Tabia za wanaume ndio zinapelekea kuroga

Sio Mara zote. Wengi hufanya ivyo ili kucontrol akili na kipato cha mume. Dah nimewakumbuka kaka zangi watatu ktk familia wote wemepigwa juju za uhakika hata wazazi wao wamewasahau
 
Kaka mapenzi yana run dunia na wanawake wana run maisha na starehe za waganga. Exclude mwaJ
 
Last edited by a moderator:
mtotohirzi.jpg
 
Ukigundua tu unasepa zako haraka sana tena bila hata kuaga.
Hahahahaha hutakiwi kusepa unagangamala tu mpaka kielewe. Kama umempenda unamshauri kwamba hayo makitu wewe haufagilii nafikiri anaweza akaelewa na pengine akaacha kabisa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mhhhhh!!! Inahitaji moyo kuendelea naye maana saa zote una wasiwasi tu, hata msosi unaanza kuukagua kwa kina kabla hujautia kinywani ukiona kitu ambacho si cha kawaida unamwita, "huu msosi wako sili" lol!!!! Hahahaha kama alivyosema farkhina mbona yako maurozi chungu nzima ya kumroga njemba bila hata ya kwenda kwa akina Nyamwicho!? Wengine urozi imeshakuwa kwenye damu yao hawajiamini kabisa kama wanaweza kupendwa kwa penzi la kweli bila kutumia mizizi na makitu mengine ya ajabu ajabu.

Hahahahaha hutakiwi kusepa unagangamala tu mpaka kielewe. Kama umempenda unamshauri kwamba hayo makitu wewe haufagilii nafikiri anaweza akaelewa na pengine akaacha kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Mhhhhh!!!! Hahahahaha lol!!! Hii mpaka ya kusahau jina kali sana....sasa akiulizwa jina lako nani anajibuje!? Silijui Hahahahaha lol!!! Hii kali dah!!!!


Mwanamme harogwi kwa mganga....

Anarogwa kwa mengi tena tena anaweza sahau hadi jina lake🙄🙄🙄....
 
Mhhhhh!!! Inahitaji moyo kuendelea naye maana saa zote una wasiwasi tu, hata msosi unaanza kuukagua kwa kina kabla hujautia kinywani ukiona kitu ambacho si cha kawaida unamwita, "huu msosi wako sili" lol!!!! Hahahaha kama alivyosema farkhina mbona yako maurozi chungu nzima ya kumroga njemba bila hata ya kwenda kwa akina Nyamwicho!? Wengine urozi imeshakuwa kwenye damu yao hawajiamini kabisa kama wanaweza kupendwa kwa penzi la kweli bila kutumia mizizi na makitu mengine ya ajabu ajabu.
Unajua kuna wengine ulozi upo kwenye damu hivyo ni vigumu hata kuwabadilisha watu wa aina hiyo. Nakumbuka baada ya kuanza kutoa tongo tongo niliwahi sema wanaume wana kazi sana yaani kujua huyu mlozi na huyu sio wakati wa mwanzo inahitaji neema mno.

Hii kitu hata mtu akulie wapi kama ana watu wanaofanyaga hayo makitu na kama akili yake ya kushikilia basi lazima afanye tu. Ninachoweza kusema hii yote inasababishwa na kutojiamini kwani kama unajiamini huwezi kushiriki hii mambo hata kidogo. Si unajua hata majiniaz huwa kwao kama ni washirikina lazima aingie na dawa siku ya mtihani mpaka unajiuliza mbona mtu huyu yuko safi tu kwanini anaendekeza hii.

Umezungumzia ya kuwekewa kwenye msosi je zingine utazibaini vipi
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom