Ushirikina mahospitalini

Ushirikina mahospitalini

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,102
Reaction score
828,974
b4fd8d31f56a738c27b7d8d17805de26.jpg
Niliahidi kuwa kipindi hiki cha Pasaka hatutakuwa na mada zetu zile , kwahiyo hii moja isifananishwe na zile japo ina muktadha unaofanana ni zile.....
Ni hili jambo la kubeba mitunguli na midubwana mingine na kumepelekea mgonjwa wako aliyelazwa kwenye hospital ya tiba za kisayansi, kwa nia ya kumkinga au kuwadhuru wengine.....
Kama huko alikotoka alikosa hii kinga na tiba mpaka akaumwa kufikia ya kulazwa kwenye hii tiba mbadala!faida gani sasa kuendelea kujidanganya kuwa huko kwingine bado kuna nguvu na msaada? ??
Siku hizi kwenye hospitali zetu kuna utaratibu mzuri sana wa kuwapekua ndugu jamaa na marafiki wanaokuja kutazama wagonjwa ni utaratibu mzuri kwakuwa umepunguza tatizo na wengi wamenyakwa
Lakini kuna la ziada serikali inapaswa kulifanya..kutafuta utaratibu wa kuwapekua hata watokao sio na magari tuu bali hata raia
Hospitali ni chimbo moja murua sana lenye utajiri wa malighafi za kufanyia ushirikina, kuanzia mabendeji yenye damu, mambo yote yanayohusika kwenye wodi za wazazi na watoto, wodi za wagonjwa wa ajali mpaka mochwari na mabaki yoyote yale ya mgonjwa au chochote alichokitumia mgonjwa hata kama ni chakula
Tunakumbuka vema sakata la Rama mla vichwa na kuku wenye hirizi Muhimbili.... Serikali ilitafakari hili
ae4d68b1f9eaa11c5519653d4d61272b.jpg
 
Huu ulimwengu una mambo ya ajabu sana, na watu wa ajabu sana
 
Kukagua watu kwa wingi ule wa wanaoingia muhimbili, napata ukakasi hapa kukubaliana na hoja hii
 
Hili ni janga kwa Kila kona ya nchi nakumbuka Kuna mama mmoja alikuja na vibuyu pamoja na pembe akaweka kwenye kitanda cha mgonjwa eti ni kinga kwa vtu vibaya tena mbaya zaid mgonjwa mwenyewe alikuwa kafanyiwa surgery hakukubali kuvitoa japo alipewa counseling juu ya madhara ya vitu hivyo ikiwemo kusababisha infection kwa sababu ni unsterile material.Elimu itolewe kwa jamii pia walinzi wafanye kaz kwa umakin ikiwemo kukagua vyema hii itasaidia kupunguza kero hii
 
Kukagua watu kwa wingi ule wa wanaoingia muhimbili, napata ukakasi hapa kukubaliana na hoja hii
Ndio maana nikasema uangaliwe utatatibu utakaofaa lakini bado kumbuka huu ni mtazamo unaoleta chagizo LA kufikirisha
 
Nachukia sana pyempyerera za ushirikina na uchawi kila siku!
 
Niliwahi kusikia dada mmoja nadhani kutoka Kenya alikuwa anahadithia yeye alipata utajiri wake kwa kulala na maiti wa kiume mochwari...Imagine na akawa anaadithia kwa ujasiri kabisa kwamba kabla mwili wa maiti haujapoa anapigiwa simu na wale ma-attendant wa mochwari dada anaenda kudo nao...
 
Dokta, hembu naomba unifafanulie kuhusu lile fuko la uzazi,maana Kuna wakati nilikuwa kenya nikaona wazazi wanalila
 
Over all ni kubadili mtazamo wetu na kutofautisha ushirikina na tiba za kisayansi

Mwaka jana mwezi wa 9 na mapema kabla ya hapo nilikutana na hii changamoto katika hospital moja huko mwanza.

Mgonjwa kapata tatizo baada ya upasuaji (tumbo zilijaa kama baada ya saa 3 hivi), madaktari wanadai ndugu au jamaa wametenda jambo la kishirikina. Ajabu na kweli.

Sasa kama hata wauguz madaktari na watu wengine wa karibu wanaamini ushirikina na kukiri hata pale usipokuwapo. Duh.

Nafahamu, Ni desturi ya mswahili kuusingizia ushirikina kila jambo asilo na maarifa nalo. Je, hata madaktari?

Tubadili mtazamo.
 
Niliwahi kusikia dada mmoja nadhani kutoka Kenya alikuwa anahadithia yeye alipata utajiri wake kwa kulala na maiti wa kiume mochwari...Imagine na akawa anaadithia kwa ujasiri kabisa kwamba kabla mwili wa maiti haujapoa anapigiwa simu na wale ma-attendant wa mochwari dada anaenda kudo nao...
mmmhhh!!!,eti nini???.
 
Mchana Jr......hivi MTU anapochukua nguo ya ndani ya MTU huwa ana kwenda kuifanyia nini.....na kama atafanya mambo je njia sahihi ya kutegua ni IPI.....
 
Yeah ni kwel hyo clip ninayo ya hiyo dada alie kuwa akilala na maiti nafikir ni frm Kenya according to her pronunciation
 
Mshana jr acha kuamini ushirikina.. Njoo katika uislamu umjue Mungu wa kweli. You still have a chance. Your life.your choice.
 
Mchana Jr......hivi MTU anapochukua nguo ya ndani ya MTU huwa ana kwenda kuifanyia nini.....na kama atafanya mambo je njia sahihi ya kutegua ni IPI.....
Hiyo ni catalyst muhimu kwenye ushirikina wa ndele na kutengeneza nuksi..Inategemea mlengwa anataka kutumia kwenye nini na anachanganya na dawa gani na ananuizia nini
 
Back
Top Bottom